Bila kujali kwamba unachosema ni cha kweli au hapana, tukirudi kwenye kauli yake ya kukemea udini ni ya kuungwa mkono na sisi wana JF bila kisingizio chochote kwani bila kufanya hivyo tutakuwa hatujashiriki kuukemea udini ndani na nje ya JF
kama nimemwelewa vizuri ndugu kikwete alipokemea udini alikuwa ametoa mfano, lakini ametoa angalizo kwa watanzania wa dini zote kwa maana na vyombo vya habari kama hivyo vya kiislamu au na kikiristo pia.
Mkuu hapo kwa "MY TAKE" ndipo kulIkonifanya nikakutwangia senksi. Sasa kama amemaliza kampeni, aanze kutekeleza ahadi sasa!
Ahadi sijui zimeisha sasa amehamia kuwapaka matope wapinzani wake, lakini licha ya juhudi zao zote lakini wapiga kura bado wapo makini na wanachuja kila wanaloambiwa. Huyu jamaa asipoangalia atakufa kwa presha!![/QUOTE]
Imeshapand sana, ndiyo maana akili sasa inayeyuka!
Alienda Mafia , akasahau kwamba amerudia ahadi zile zile za mwaka 2005, na akawaambia kwamba pesa alizotoa za maendeleo TZS 200M zimeliwa na wajanja. Bahati mbaya mmoja wa wajanja aliokuwa anawasema ndo mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, amabaye pia ndiye mbunge aliyemaliza kipindi kilichopita.
Sasa mafia almost wote ni waisilamu, na wamemshitukia kwamba kawafanya mabwege...hivyo hawampi kura! Nawashauri Slaa na Lipumba wakaziombe hizo kura za Mafia Island, JK hazipati hata iweje.........