Kikwete - Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete - Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Oct 21, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kikwete: Wakataeni wanaohubiri udini

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Lindi;
  Source: Habari leo


  Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameonya kuwa umwagaji damu na migawanyiko ya kidini inayohubiriwa na Chadema kutokea baada ya uchaguzi, vitakuwa yenye majuto makubwa zaidi nchini kwa sababu migawanyiko ya kidini itamhusu kila Mtanzania.

  Aidha, Rais Kikwete amesema migawanyiko ya kidini itakuwa na athari kubwa zaidi kuliko hata ya kikabila.

  "Ile ndiyo itakuwa siku ya giza, siku ya majuto wakati migawanyiko ya kidini itakapotawala katika nchi kwa sababu itamhusu kila mwananchi wa Tanzania," alisema hayo jana katika mkutano wa kampeni eneo la Nyangao, Mtama, mkoani Lindi.

  "Migawanyiko ya ukabila itakuwa kati ya kabila moja na lingine ama kati ya kabila moja na makabila mengine, lakini mgawanyiko wa dini utamhusu kila mwananchi wa Tanzania. Ni mgawanyiko hatari sana," alisema Rais Kikwete ambaye alifanya kampeni Nyangao, Mchinga na Lindi Mjini.

  Alisema mashindano ya sasa kwenye uchaguzi mkuu si ya nani yuko dini gani, au nani anatoka kabila gani. "Yetu ni mashindano ya hoja za kisiasa … ni mashindano kuhusu elimu, barabara, afya, maji … haya ndiyo maeneo ambako vyama vya siasa vinastahili kupambana si kwenye udini, ukabila, vitisho na umwagaji damu."

  Rais aliwataka wananchi kukataa viongozi wa kisiasa na kijamii wanaohubiri ulevi wa umwagaji damu na udini katika kampeni.

  "Wakataeni, hata kama ni wakubwa kiasi gani katika uongozi wa siasa ama wa kijamii. Ni watu hawana maana na hatari wa ustawi wa Taifa letu," alisisitiza.

  Alisema ni dhahiri kuwa viongozi wanaohubiri umwagaji damu na udini ni watu ambao wameshindwa siasa na wanarukia dini na ukabila.

  Alisisitiza kuwa CCM itaendelea kuhubiri amani, utulivu na upendo miongoni mwa wananchi wa Tanzania, kwa sababu sifa hizo ni muhimu sana ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.

  "Sisi si chama kinachohangaika kutuma vimeseji vya kupandikiza chuki za kidini kama wanavyofanya wenzetu."

  Kwa kufanya kampeni Lindi, mgombea huyo wa CCM sasa amemaliza rasmi kampeni zake katika mikoa yote ya Tanzania – kampeni ambayo ilifunguliwa rasmi Agosti 21 mwaka huu, kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

  Baada ya Dar es Salaam, alikwenda Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Dodoma kabla ya kuingia mzunguko wa tatu ambao ulimfikisha Iringa, Mara, Mwanza tena, Shinyanga, Tabora, Singida na Dodoma tena.

  Mgombea huyo wa CCM pia ametembelea visiwa vya Pemba na Unguja, Ruvuma, Mtwara, Pwani na Lindi.

  My Take:

  Walianza kukoment kwa mafumbo, chinichini na sasa wameibuka. Kumbe hata zile sms very likely ni mwongozo kutoka kwa JK.

  JK sasa ameishiwa, yaani yeye bado ni raisi, Amiri jeshi mkuu halafu anaacha tu watu wanahubiri kumwaga damu na udini??????? Ina maana huyu jamaa haelewi kwamaba anapata upinzani kwa sababu ya poor perfomance na badala yake anaamini ni kwa sababu ya dini yake??????? Poor JK, come on this is too low!!!!!!!!!!!!

  Hao chadema anaowatuhumu ni akina nani? kwa nini hawachukuliwi hatua? JK pls njoo kwenye mdahalo uwaeleze watz unachoamini na wewe ujibiwe kwa hoja.
   
 2. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu hapo kwa "MY TAKE" ndipo kulIkonifanya nikakutwangia senksi. Sasa kama amemaliza kampeni, aanze kutekeleza ahadi sasa!
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  ccm bwana/bibi wana hubiri kupinga rushwa, amani, maendeleo nk, lakini matendo yao yapo tofauti na wanavyo sema.
  Naona Kikwete kama kweli Mstaarabu nk ajitoe tu kwenye uchaguzi wa Mwaka Huu awaachie Lipumba na Slaa.
  Angalau atabakisha heshima kidogo kwa wananchi na kwa Nchi yetu.
   
 4. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  anawaogopesha watu sasa hivi
   
 5. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  JK hoi bin taabani
   
 6. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawakujipanga vizuri, walijua watu bado hawajaipata ile sumu ya ufisadi, mikataba mibovu, tena wakafanya makosa yanayowamaliza makosa hayo ni KURAAAAAAAAAAAAAAAA ZA MAOOOOOOOOOOOOOOONI. Wanataka kukifanya chama kuwa cha genge fulani la wateule wachache wakiwasahau wananchi wa kawaida.
  Kama haitoshi, wakaanza siasa za majitaka. Its too bad you know.
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  wasisingizie udini - yeye na makamba ndiyo wamekiharibu chama, pia aelewe watanzania wa 2010 si wale wa 1980 - Watu wame rate peformance yake na CCM kwa ujumla kwa miaka 5 iliyopita kuwa ni dhaifu mno.

  Sasa waajiri wake ambao ni wananchi wa tanzania wameamua kubadilisha upepo kumpa mtu mwenye uwezo na kazi hiyo. mwaka huu watu hawahongeki. Tena akizidi kupenyeza udini ndiyo anawaudhi zaidi wapiga kura.

  CCM wanavuna walichopanda.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Jana nilisema DR akamatwe lao natamka Rasmi JK akamatwe kwa kueneza mambo ya udini! HAKULA HURUMA JK AJIBU SHUTUMA HIZI!
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  huyu mzee atakufa kwa presha sasa hapo kaongela nini?
  Huyu zee naona anafuata nyayo za kibaki
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi ni kwanini HabariLeo na CCM wasidhitishe? CHADEMA pelekeni hili kwa NEC/Tendwa. Najua hawatasema chochote cha maana ila just to keep record.
   
 11. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi sijawahi kuwasikia wagombea wengine wakihubiri udini kwa nguvu kama wanavyofanya makada wa CCM, na hawa ndio wanapiga kelekele kuliko wote. Walidhani kuwa kutumia udini ungeliwabeba lakini naona mambo yanaanza kuwaendea mrama na sasa wanatapatapa, hawajui pa kushika.
   
 12. M

  Mikomangwa Senior Member

  #12
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani huo udini na ukabila unaohubiriwa na Chadema mbona wengine hatuusikii? Sijawahi kusikia DR wa ukweli akitamka maneno yanayohubiriwa. Kweli mfa maji haachi kutapatapa. JK ndiye anayewapandikizia waTZ misamiati ambayo hawajaizoea. Kwani vipi gunia la ahadi limeisha sasa amebadili mikakati ya ushindi? GOD'S JUSTICE WILL ALWAYS PREVAIL!!!
   
 13. d

  dotto JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  SIJWAHI KUSIKIA CHADEMA WANAHUTUBIA WATU JUU YA ITIKADI YA DINI YA MTU BALI CCM WANAOBAGUA WATU KWA RANGI .MFANO: BASHE N.K.

  WATAKULA MATAPISHI KWA SANA!!!

  YANA MWISHO by KULI.
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ahadi sijui zimeisha sasa amehamia kuwapaka matope wapinzani wake, lakini licha ya juhudi zao zote lakini wapiga kura bado wapo makini na wanachuja kila wanaloambiwa. Huyu jamaa asipoangalia atakufa kwa presha!!
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kwa sasa BORA liende amechelewa kujitoa, Angesingizia anaumwa kwenye kamati ya chama!
   
 16. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jk,yeye ndie mwasisi, wa kampeni za familia kwanza ,unafuata mtandao , unafuta udini, inafuata ujeshi, ndio chama na mwisho taifa.
   
 17. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa nini huyu anaropoka mambo ya uongo namna hii na wananchi hawamzomei? Kwa nini anashindwa kumtaja mtu anayehubiri umwagaji damu au ukabila? Anawadanganya wananchi huku akitumia magazeti ya kijinga kama HabariLeo kueneza hii propaganda yake. It really gets on my nerves... Grhhhh
   
 18. Nyabwire

  Nyabwire Member

  #18
  Oct 21, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na kama anafuata vyema maadili ya dini yake nisimchague pia?je,wanaoambia watu waache uzinzi kwani dini zao zinakataa wakati wao ndio wazinzi wakubwa?????ccm bwana!!!!!
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kumbe zile meseji za Rashid Shamte hazikuwa za ccm....kweli amesahau au ndo alivyo...
  Afu ndo aongezewe miaka 5.....!Mkuu be seriuos sometimes
   
 20. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  JK achana na mambo hiyo!!!!! Utajimaliza mwenyewe????? Radio na magazeti ya kiislamu(radio imani, magazeti ya annoor na alhuda) yanahubiri udini mkubwa mno huku yakimchafua waziwazi Dr. Slaa(ambaye wao humwita Padre Slaa)!!!! na wakati huohuo yakimpa JK sifa kemkem(hata ambazo hana)....Vyombo hivi vya habari vimediriki kuwaaminisha waislam kuwa makosa yaliyofanywa na marais wastaafu wa kiislam walisingiziwa tu ila hawakufanya wao bali yalifannywa na wasaidizi(au viongozi wenzao) wa kikristo....mfano ni mauaji ya Pemba, na yale ya Mwembe Chai!!!!!! Mbegu hii mbaya ya udini inayopandwa na wenzetu waislam haijawahi kukemewa na serikali hata mara moja!!!!!!! Badala yake, serikali na CCM wamekuwa ikikejeli matamshi yoyote yanayotolewa na viongozi wa dini ya kikristo (e.g., Kakobe and more recently Malasusa) hata kama yanatoa angalizo la kawaida juu ya uchaguzi lisilo na udini wowote!!!!!

  Hii inatoa taswira kuwa serikali ya CCM haikerwi na udini unaoipa CCM competitive advantage ya forthcoming election....ila wanakerwa na udini ambao hauifagilii CCM..... Jicho hili la kengeza la JK lidhibitiwe mapema kabla halijaleta mazara kwa taifa.....
   
Loading...