Kikwete tenda wema uende zako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete tenda wema uende zako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Oct 21, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Takribani miaka mitatu na nusu imebaki sasa kuwepo madarakani, usipoangalia kwa makini utafikiri ni mingi mno lakini nakukumbusha kuwa muda wako u karibu kwisha kama ni jua ni la magharibi. Kwenye utawala wako kuna mengi mazuri umeyafanya lakini vile vile kuna mengi mabaya umeyafanya kubali usikubali. Kwa kulitambua hilo sasa ni wakati mwafaka kwako kujiandaa na maisha mapya ya ustaafu. Najua kipindi hiki ni kigumu sana kwako hasa kwa vile unajaribu kubalance kati ya matarajio ya wananchi na kuwaridhisha waliofanikisha uwepo wako hapo ulipo. Kwenye kipindi chake cha pili kama hiki Mh. Mkapa alijaribu hayo unayotaka kuyafanya kwa kusema 'liwalo na liwe kwa vile sigombei tena', nakushauri usifikirie hivyo. Tenda wema kwa watu wote wapinzani na wasio wapinzani bila kujali nani alikusaidia na yupi alikupinga utaishi kwa amani. Kuwa kiongozi wa kuigwa ili kuepusha migongano utakayorithisha vile vile kuepuka yanayowapata viongozi wengi wa kiafrika wanaokumbatia waliowazunguka na kuwasahau wananchi wake.

  Natumai ujumbe huu utakufikia. Feedback.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,621
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Unampigia mbuzi gitaa mkuu.
   
 3. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  atoke tu jana kazomewa next time watu watam "poke" na "midofinga" mazafanta
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2017
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nimerudi tena hapa JF baada ya likizo ya muda mrefu, natoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa rais mstaafu kwa vile ujumbe wangu aliuzingatia, asante sana kweli wewe ni tunu ya kuigwa.
   
Loading...