Kikwete: Tanzania ipo katika mikono salama

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,100
2,000
RAIS wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameeleza namna alivyopata ugumu kupokea taarifa kuhusu kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, lakini akasema wananchi wasiwe na hofu kwa kuwa Tanzania ipo katika mikono salama.

Kikwete aliyasema hayo jana kupitia ukurasa wake wa twitter.

Alisema jambo la faraja kubwa kwa Watanzania ni kuwa mrithi wa Hayati Magufuli, Rais Samia Suluhu Hassan, alikuwa Makamu wa Rais wa Rais Magufuli tangu mwaka 2015 hadi umauti ulipomkuta Magufuli, hivyo anajua undani wa yale yaliyofanyika na yanayohitaji kukamilishwa.

Rais mstaafu huyo alisema Rais Samia anayajua yaliyopangwa kufanyika katika miaka mitano ijayo, hivyo hana shaka kuwa Tanzania ipo katika mikono salama.

“Nampongeza Rais Samia kwa hotuba fupi na nzuri aliyoitoa baada ya kuapishwa na yenye kujenga imani na kuleta matumaini. Tumuombee Rais wetu kwa Mwenyezi Mungu amuongoze vyema kwa kila uamuzi atakaochukua na kila hatua atakayopiga,” alisisitiza Kikwete.

Aliongeza: “Niwaombe Watanzania wenzangu tumpe ushirikiano ili aweze kuongoza Tanzania kwa ufanisi na mafanikio zaidi.”

Alitoa salamu za mkono wa pole na rambirambi kwa mjane wa marehemu, Mama Janet Magufuli na familia yake nzima.

Kuhusu namna alivyoandika ujumbe huo katika ukurasa wa twita, Kikwete alisema: “Nimepata tabu kuandika kwa kifupi kuelezea simanzi na masikitiko yangu kwa msiba mkubwa ulioukumba nchi yetu kwa kuondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Rais Magufuli, nimelazimika kuyaambatanisha hapa chini, Mwenyezi Mungu amuwekea mahali pema, peponi.”

Akaongeza: “Ni pigo kubwa, tena ni kubwa lisilomithilika. Rais wetu mpendwa John Magufuli ametutoka ghafla bila ya kutazamia. ‘I never saw this coming’ (Sikulitarajia hili). John Pombe Magufuli ametutoka wakati ambapo uongozi wake ulikuwa unahitajika sana.”

Kwa mujibu wa Rais Mstaafu Kikwete, bado Watanzania walikuwa wanamhitaji kiongozi huyo kukamilisha aliyoyaanza na kufanya mazuri mengi aliyokuwa amepanga kuifanyia nchi na wananchi wake.

“Tungetamani John Magufuli tuendeee kuwa naye leo na miaka mingi ijayo, lakini mapenzi ya Mungu hatuna uwezo wa kuyabadili… Wajibu wetu ni kumuombea kwa Mola ampe mapumziko. Daima tutamkumbuka Rais Magufuli kwa mema mengi aliyoifanyia nchi yetu. Hakika Tanzania imepoteza kiongozi mzalendo wa dhati, shupavu, mahiri na makini,” alisema.
 
Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,127
2,000
Sawa Mkuu!
Kwasasa ni vema akae mbali na mama ili mama aendelee kutekeleza mipango iliyopo labda akiombwa ushauri maana wazee wa kuchomekea tunawajua!
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,212

SSH = JK
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,274
2,000
Siamini kama itakuja kutokea tena siku moja kuja kutawaliwa na Rais aina ya Magufuli!! Aisee Udikteta uusikie tu kwa wenzako!

Yaani ndani ya miaka michache tu ya utawala wake, alijigeuza kuwa Alfa na Omega! Mungu ni mwema sana. Ametupa funzo! Sidhani kama kuna mtu atakuja kuleta tena masihara kwenye uteuzi wa mgombea Urais!
 
kookaburra

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
223
1,000

Amen! Tunamshukuru Mungu sana kwa kutuondolea hili balaa
Mungu anatupenda sana watz
 
secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
5,712
2,000
Siamini kama itakuja kutokea tena siku moja kuja kutawaliwa na Rais aina ya Magufuli!! Aisee Udikteta uusikie tu kwa wenzako!

Yaani ndani ya miaka michache tu ya utawala wake, alijigeuza kuwa Alfa na Omega! Mungu ni mwema sana. Ametupa funzo! Sidhani kama kuna mtu atakuja kuleta tena masihara kwenye uteuzi wa mgombea Urais!
Maendeleo aliyoleta tumeyaona.....
chema hakidumu.....
miaka mitano ya kupambana na majizi na kujenga nchi at the same time sio mchezo
ila ww mwenye kisirani......
nadhani ulikuwa upande wa majizi au wauza ngada....
 
Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,780
2,000
RAIS wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameeleza namna alivyopata ugumu kupokea taarifa kuhusu kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, lakini akasema wananchi wasiwe na hofu kwa kuwa Tanzania ipo katika mikono salama.

Kikwete aliyasema hayo jana kupitia ukurasa wake wa twitter.

Alisema jambo la faraja kubwa kwa Watanzania ni kuwa mrithi wa Hayati Magufuli, Rais Samia Suluhu Hassan, alikuwa Makamu wa Rais wa Rais Magufuli tangu mwaka 2015 hadi umauti ulipomkuta Magufuli, hivyo anajua undani wa yale yaliyofanyika na yanayohitaji kukamilishwa.

Rais mstaafu huyo alisema Rais Samia anayajua yaliyopangwa kufanyika katika miaka mitano ijayo, hivyo hana shaka kuwa Tanzania ipo katika mikono salama.

“Nampongeza Rais Samia kwa hotuba fupi na nzuri aliyoitoa baada ya kuapishwa na yenye kujenga imani na kuleta matumaini. Tumuombee Rais wetu kwa Mwenyezi Mungu amuongoze vyema kwa kila uamuzi atakaochukua na kila hatua atakayopiga,” alisisitiza Kikwete.

Aliongeza: “Niwaombe Watanzania wenzangu tumpe ushirikiano ili aweze kuongoza Tanzania kwa ufanisi na mafanikio zaidi.”

Alitoa salamu za mkono wa pole na rambirambi kwa mjane wa marehemu, Mama Janet Magufuli na familia yake nzima.

Kuhusu namna alivyoandika ujumbe huo katika ukurasa wa twita, Kikwete alisema: “Nimepata tabu kuandika kwa kifupi kuelezea simanzi na masikitiko yangu kwa msiba mkubwa ulioukumba nchi yetu kwa kuondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Rais Magufuli, nimelazimika kuyaambatanisha hapa chini, Mwenyezi Mungu amuwekea mahali pema, peponi.”

Akaongeza: “Ni pigo kubwa, tena ni kubwa lisilomithilika. Rais wetu mpendwa John Magufuli ametutoka ghafla bila ya kutazamia. ‘I never saw this coming’ (Sikulitarajia hili). John Pombe Magufuli ametutoka wakati ambapo uongozi wake ulikuwa unahitajika sana.”

Kwa mujibu wa Rais Mstaafu Kikwete, bado Watanzania walikuwa wanamhitaji kiongozi huyo kukamilisha aliyoyaanza na kufanya mazuri mengi aliyokuwa amepanga kuifanyia nchi na wananchi wake.

“Tungetamani John Magufuli tuendeee kuwa naye leo na miaka mingi ijayo, lakini mapenzi ya Mungu hatuna uwezo wa kuyabadili… Wajibu wetu ni kumuombea kwa Mola ampe mapumziko. Daima tutamkumbuka Rais Magufuli kwa mema mengi aliyoifanyia nchi yetu. Hakika Tanzania imepoteza kiongozi mzalendo wa dhati, shupavu, mahiri na makini,” alisema.
Duh, ila JK akisema salama mie napokea kauli zake kwa tahadhari sana, siyo kwa mchwa wake uliotutafuna wakati anachekacheka kuwa tupo salama!
 
Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
122
250
JAKAYA KIKWETE: TANZANIA IPO KWENYE MIKONO SALAMA

- Rais Mstaafu wa awamu ya 4 asema amepokea taarifa ya kifo cha Rais Magufuli kwa ugumu

- Asema, Rais Samia anayajua yaliyopangwa kufanyika miaka mitano ijayo, hivyo Tanzania ipo salama

IMG_20210321_131413_434.JPG
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Poa 2

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
865
1,000
Siamini kama itakuja kutokea tena siku moja kuja kutawaliwa na Rais aina ya Magufuli!! Aisee Udikteta uusikie tu kwa wenzako!

Yaani ndani ya miaka michache tu ya utawala wake, alijigeuza kuwa Alfa na Omega! Mungu ni mwema sana. Ametupa funzo! Sidhani kama kuna mtu atakuja kuleta tena masihara kwenye uteuzi wa mgombea Urais!
Tukiendelea kuikumbatia katiba hii inayompa raisi u mungu mtu ipo siku inakuja tutaumizwa zaidi ya hapa ni Mungu ru ameamua nafasi nyingine tubadishe mfumo wetu
 
Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,213
2,000
RAIS wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameeleza namna alivyopata ugumu kupokea taarifa kuhusu kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, lakini akasema wananchi wasiwe na hofu kwa kuwa Tanzania ipo katika mikono salama.

Kikwete aliyasema hayo jana kupitia ukurasa wake wa twitter.

Alisema jambo la faraja kubwa kwa Watanzania ni kuwa mrithi wa Hayati Magufuli, Rais Samia Suluhu Hassan, alikuwa Makamu wa Rais wa Rais Magufuli tangu mwaka 2015 hadi umauti ulipomkuta Magufuli, hivyo anajua undani wa yale yaliyofanyika na yanayohitaji kukamilishwa.

Rais mstaafu huyo alisema Rais Samia anayajua yaliyopangwa kufanyika katika miaka mitano ijayo, hivyo hana shaka kuwa Tanzania ipo katika mikono salama.

“Nampongeza Rais Samia kwa hotuba fupi na nzuri aliyoitoa baada ya kuapishwa na yenye kujenga imani na kuleta matumaini. Tumuombee Rais wetu kwa Mwenyezi Mungu amuongoze vyema kwa kila uamuzi atakaochukua na kila hatua atakayopiga,” alisisitiza Kikwete.

Aliongeza: “Niwaombe Watanzania wenzangu tumpe ushirikiano ili aweze kuongoza Tanzania kwa ufanisi na mafanikio zaidi.”

Alitoa salamu za mkono wa pole na rambirambi kwa mjane wa marehemu, Mama Janet Magufuli na familia yake nzima.

Kuhusu namna alivyoandika ujumbe huo katika ukurasa wa twita, Kikwete alisema: “Nimepata tabu kuandika kwa kifupi kuelezea simanzi na masikitiko yangu kwa msiba mkubwa ulioukumba nchi yetu kwa kuondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Rais Magufuli, nimelazimika kuyaambatanisha hapa chini, Mwenyezi Mungu amuwekea mahali pema, peponi.”

Akaongeza: “Ni pigo kubwa, tena ni kubwa lisilomithilika. Rais wetu mpendwa John Magufuli ametutoka ghafla bila ya kutazamia. ‘I never saw this coming’ (Sikulitarajia hili). John Pombe Magufuli ametutoka wakati ambapo uongozi wake ulikuwa unahitajika sana.”

Kwa mujibu wa Rais Mstaafu Kikwete, bado Watanzania walikuwa wanamhitaji kiongozi huyo kukamilisha aliyoyaanza na kufanya mazuri mengi aliyokuwa amepanga kuifanyia nchi na wananchi wake.

“Tungetamani John Magufuli tuendeee kuwa naye leo na miaka mingi ijayo, lakini mapenzi ya Mungu hatuna uwezo wa kuyabadili… Wajibu wetu ni kumuombea kwa Mola ampe mapumziko. Daima tutamkumbuka Rais Magufuli kwa mema mengi aliyoifanyia nchi yetu. Hakika Tanzania imepoteza kiongozi mzalendo wa dhati, shupavu, mahiri na makini,” alisema.
Kikwete awekwe kando, maana naona kama anaisogelea IKULU. Hatuhitaji Tanzania ya akina Rostam, tunahitaji Tanzania iliyo huru na UFISADI. Tanzania inayotumia kodi za wananchi ipasavyo kwa faida ya wananchi kama ujenzi wa barabara, flyover, kuboresha kiwango cha maisha ya mwananchi, Kilimo, afya, vyombo vya ulinzi vinavyojali wananchi, mikataba ya madini yenye tija kwa taifa n.k. Na kubwa zaidi ni upatikanaji wa KATIBA MPYA - Ktiba ya Warioba ipatikane katika uhai wa mzee Muasisi wa katiba hiyo - Mzee Warioba.

Ili kufanikisha hayo ni lazima kumuweka Kikwete kando, Hakuweza kukamilisha katiba mpya hatoweza kushauri chochote cha maendeleo kwa manufaa ya Umma.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom