BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,117
Kikwete tangaza hali ya hatari - Kiula
na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
WAZIRI wa zamani wa Ujenzi, Nalaila Kiula, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutangaza hali ya hatari ili kulinusuru taifa na wimbi la ufisadi.
Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumapili nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam, Kiula alisema kutangaza hali ya hatari ndiyo njia pekee itakayomsaidia Rais Kikwete kuanza kuwashughulikia watu ambao sasa wanaonekana kuwa matajiri wa kupindukia.
Napenda kumshauri Rais Kikwete kutangaza hali ya hatari kwa kipindi hiki ikiwa ana lengo dhidi ya viongozi wote wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kifisaidi hii itamsaidia kuelewa mbaya ni yupi, alisema Kiula.
Alisema kama Rais Kikwete hatachukua hatua za makusudi, taifa linaweza kuingia kwenye machafuko yasiyotarajiwa kwa vile kumekuwa na matabaka mawili ya matajiri na maskini.
Tusipoangalia tutajikuta taifa linaingia kwenye machafuko, hivi sasa tayari kuna matabaki ya matajiri na maskini, jambo hili ni baya na linapaswa kuchukuliwa hatua haraka. Siku wananchi wakikasirika matokeo yake yataonekana, alisema Kiula.
Alisema vita ya kupamba na mafisadi itafinikiwa iwapo Rais Kikwete atakubali mtangulizi wake, Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuhojiwa na vyombo vya dola kwa kuwa anatuhumiwa sana kuhusika na kuwepo kwa vitendo vya ufisadi miongoni mwa watumishi wa umma wakati wa utawala wake.
Tutakuwa tunajidanganya kama Rais mstaafu Mkapa asipofukuliwa maovu yake yeye ndiye aliyetufikisha hapo tulipo mpaka sasa, tunaandamwa na mafisadi kwa sababu yake, kwa vile kuna mikataba mingi yenye utata iliyosainiwa wakati wa utawala wake, alisisitiza Kiula.
Alisema kama Rais Kikwete anataka kujiweka katika hali nzuri ya utawala anatakiwa kutoa haraka orodha ya majina ya watu wanaohusishwa na upoteaji wa fedha Benki Kuu (BoT) kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya Nje (EPA).
Sasa hivi hali inatia kinyaa, kila kona mafisadi, hapa njia pekee ni Rais Kikwete kutoa kibali cha kukamatwa wale wote wanaotajwa majina yao katika kashfa hii ili liwe fundisho kwa wengine, alisema Kiula.
Katika hatua nyingine, Kiula aliwataka Watanzania kwa imani zao kumwombea Rais Kikwete kila siku ili aweze kupambana na hali ngumu inayomkabili kuhusu wasaidizi wake.