Kikwete, tafadhali fuata nyayo za Pervez Musharraf

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Shikamoo,

LEO nimeamua kuandika waraka huu kwako Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka inayokaribia mitatu sasa tangu ushinde na kuapishwa mwaka 2005 baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu.

Napenda kutumia fursa hii kukupa pole kwa kazi ngumu ya kuongoza kundi la watu wengi wenye njaa ya tumbo, njaa ya ubongo na njaa ya tiba bora.

Hakika njaa zinazowakabili Watanzania ni nyingi na hazina ukomo, hasa zikiainishwa kwa nafasi binafsi, kaya, kata, kijiji, miji, majiji na taifa kwa ujumla wake.

Ni mnafiki pekee anayeweza kukudanganya, au wewe mwenyewe kudanganyika (ingawa hili najua siyo rahisi kwako kwa kuwa umeyaishi maisha ya wengi wetu), kwamba mambo ni shwari kila mahala. Kwamba HAKUNA MATATA.

Nakumbuka vyema, na bahati nzuri bado ninaendelea kuirejea hotuba yako ya mara ya kwanza Bungeni Dodoma ambayo ilisheheni ahadi na namna nzuri ya kumpunguzia Mtanzania ufukara (unaojumuisha njaa zote alizonazo).

Kila Mtanzania aliyekusikia siku ile ukiwa umetulia na kuisoma vyema, atakubaliana nami kwamba hotuba ile ndiyo ilikuwa dira yenye mwanga wenye miali ya kuchoma na kuunguza kero nyingi za watu wako waliokuchagua, hata wale wasiokipenda chama chako – CCM, kwa kura za kishindo.

Ni hotuba ile iliyohuisha hatma ya maisha yao iliyokuwa imefikia mahali pa kuonyesha kukata tamaa, hata kama waliokutangulia walikuwa wakitamba kwa hadithi za kukua na kuimarika kwa uchumi mkuu, ilhali maisha ya watu yakiendelea kudhoofika.

Kadri miaka ilivyokuwa ikisonga, hasa ule mwaka wa kwanza, matumaini ya watu wako yaliendelea kukupa muda kwamba neema ya kweli yaja. Hakuna aliyeonekana kuwa na haraka ya hiyo neema iliyoonekana katika hotuba yako na hata dhamira yako iliyojionyesha kuchukizwa na umaskini wao.

Hata hivyo, ikiwa miaka mitatu inakaribia kukatika, asilimia kubwa ya matumaini waliyokuwa nayo watu wako wengi, kwamba wewe ndiye mkombozi aliyepo, inapungua kwa kasi ya kutisha, hata kama wasaidizi wako, hasa wale wanafiki na wanaojipendekeza watakueleza vinginevyo.

Uhakika ni kwamba hata wewe unalitambua hilo kupitia kwa watu wako wengine wa karibu, wale wanaoitwa –mawaziri wa jikoni wa rais-hasa wanafamilia uliowapa jukumu la kukusanya ‘maneno’ ya watu wako huku kwetu mitaani.

Kasi ya kupungua kwa asilimia kubwa ya matumaini ya watu wako yanajiegemeza katika matukio mabaya yaliyoikumba nchi yetu, yakiwa yanafanywa ama na wasaidizi wako, uliowachagua kwa imani kubwa, au wafanyabiashara wenye kuhusiana nao.

Hilo halina kificho na wala hakuna haja ya kukueleza vinginevyo, kwani hata wao wenyewe walitambua na sina uhakika kama walijutia kuhusika kwao na dhambi za kuongeza ufukara kwa Watanzania, lakini angalau waliamua kuachia ngazi kwenye madaraka uliyowapa na wengine kuikimbia nchi, wakijificha huko walikotanguliza ‘vijisenti’ walivyowaibia watu wako.

Ufisadi. Ufisadi. Ufisadi. Hii ni dhambi ambayo imekuwa ikilaaniwa na wapenda nchi yao, ikiwa inabeba na dhambi nyingine nyingi, ambazo zimekuwa, siyo kero tu, bali mzigo mzito wa gharama za maisha kwa watu wako.

Ni ufisadi huo ambao umeongeza bei ya umeme, bei ya vyakula, ada kwa watoto wetu, nauli kupanda na hakika umegusa kila sehemu ya maisha ya wananchi wa Tanzania, kiasi kwamba serikali nzima unayoiongoza ikaonekana inachusha kwa kila mtu, isipokuwa mafisadi wenyewe, wake zao, watoto wao na hata vimada wao.

Sasa leo wakati utakapokuwa ukilihutubia Bunge, mjini Dodoma, watu wako wenye kukata tamaa, wanataka uongee. Wanataka uzungumzie masuala yanayowakera kila uchao kwa sasa. Hawataki siasa ambazo tumezizoea zinazotolewa na viongozi wetu wanasiasa.

Wananchi wanataka kusikia namna unavyochukia ufisadi kwa dhati ya moyo wako. Wanataka kukusikia na kukuona ukikunja ndita kuwalaani na kutoa amri kuu ya kuwachukulia hatua kali mafisadi wote wanaofifisha juhudi binafsi ulizoanza kuzionyesha mwanzo wa uongozi wako.

Binafsi, msema kweli mpenzi wa Mungu, nikushangae kidogo kwa kushindwa hadi sasa kuwakemea wakuu wafuatao; Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kwa kushindwa hadi sasa kuwakamata watu walioandikwa katika ripoti uliyokabidhiwa majuzi juu ya uchunguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya je (EPA).

Kwamba kwanini hadi sasa hawajawaadabisha mafisadi wake wakati timu yao imekamilisha kazi? N’nachojua mimi ni kwamba wao kwa kazi zao wangekuwa wamewakamata watu hao kwanza na ndipo baadaye wakupe ripoti hiyo.

Polisi wanatakiwa kuwakamata wahalifu hao, baada ya Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Takukuru kuthibitisha kuwa walihusika na wizi huo, sasa wanasubiri nini au mpaka uwaeleze wawakamate watu hao? Wao wanafanya kazi gani, yaani kukupa ripoti basi? Wanasubiri nini? Au nao tuseme wako pamoja nao kama tulivyoshuhudia baadhi yao wakitetea wizi ambao bado unasumbua kupatikana kwa neema ya Tanzania?

Kama hawajawakamata tuseme hawajawatambua hadi sasa. Ikiwa ripoti hiyo imejaa maneno matupu kama ya ukasuku wa wanasisa, tafadhali achana nayo kabisa na usiisome kwani itakuondolea zaidi asilimia za imani kwa wananchi wako.

Idadi kubwa huku mitaani tunakopita na kuzungumza na wapiga kura wako, wengi wanaonekana kushangaa timu hiyo uliyoiunda, kwamba inasubiri nini.

Mbali na hilo, wananchi wanatarajia kuwa utazungumzia na kutoa msimamo juu ya ‘mgogoro’ wa Muungano, hatma ya maslahi kwa wafanyakazi na zaidi sana suala zima la neema kwa kila Mtanzania.

Rais Kikwete, vitabu vitakatifu, ambavyo naamini unavithamini na ndiyo mwongozo wako, kabla ya Katiba, vinasema kuwa ukiona maovu yanatendeka, basi yazuie hata kwa upanga ili yasiendelee, ukishindwa yakemee hata kwa ulimi na ukishindwa kabisa, basi onyesha kuchukizwa na kuchukua hatua, hata kwa kupitia wengine.

Hatua za namna hii, zimetumiwa zaidi na Rais wa Rwanda Paul Kagame na hatimaye sasa nchi hiyo iliyokuwa imegubikwa na vita, inapanda kwa kasi katika chati yake ya kuwaletea neema wananchi wake.

Utakapofaya hivyo, hakika utakuwa umemtendea haki Mungu Mkuu na waja wake Watanzania na thawabu zitarundikana katika fungu lako.

Nakutakia kila jema uwapo Dodoma na unapojiandaa kwa safari yako ya Marekani.

Wasalaam

Simon Martha Mkina
Simu: 0754 020880
Email: smkina@gmail.com
Blog:www.mkina.bloghspot.com

(Waraka huu umechapishwa katika gazeti la Kulikoni la leo) Tumeiweka hapa kwa hisani ya gazeti.
 
Bwana Kikwete,

Sijui ni kitu gani ulichoropoka Bungeni wala sijakaa chini kuhoji umesema nini, lakini nafikiri wazo nililokuwa nalo siku 5 zilizopita lilikuwa sahihi na nisingepupa japo nafasi moja nyingine kujisahihisha.

Kwa heshima na taadhima nakuomba ufuate nyayo za aliyekuwa Rais wa Pakistani, Bwana Pervez Musharaff kubwaga manyanga na kuingia mitini! Kazi imekushinda, mbwembwe ulizokuja nazo, majigambo na kujisifu umethibitisha tena kuwa huna uwezo kuongoza Taifa letu.
 
Rev nyie si ndio mlimwita mwokozi , chaguo la mungu , nabii na majina mengine mengi sana ambayo yanatia aibu kuyataja hapa nyie viongozi wa dini mligeuza makanisa yenu sehemu ya kumtukuza nabii huyu wa uwongo .

Nyie ndio mlimpandisha katika mlima kilimanjaro wa uwongo pale kanisani katika kuchangia matumbo yenu sasa hivi hamumtaki nashindwa kuamini nyie wapiga kura
 
...Its bad ... its bad... Our president is not metabolic at all...can not cause any digestion for ...to be assimilated to the country....is the peolple pleaser...its very bad..!
 
Rev nyie si ndio mlimwita mwokozi , chaguo la mungu , nabii na majina mengine mengi sana ambayo yanatia aibu kuyataja hapa nyie viongozi wa dini mligeuza makanisa yenu sehemu ya kumtukuza nabii huyu wa uwongo .

Nyie ndio mlimpandisha katika mlima kilimanjaro wa uwongo pale kanisani katika kuchangia matumbo yenu sasa hivi hamumtaki nashindwa kuamini nyie wapiga kura

Shy,

Umekuwa ukiongea kana kwamba unanifahamu na hii si mara ya kwanza kunizushia kuwa nilimpamba Kikwete na kumpandisha chati.

Hata majuzi nilikuuliza ni nani nilimpigia kura 2005, ukatoa majibu kama uliyoyasema hapa juu.

Kwa miaka miwili uliyokuwa unanisoma hapa JF, labda hata kama ulikuwa kule BCS, je ni kipi kilichokupa hoja kudai kuwa mimi nilimpa baraka Kikwete?

Kuna mawili, ama unatafuta mtu mpya kujibishana au kama si hivyo, basi una upeo mdogo kuelewa ninachoandika na maandiko yangu yoote uliyoyasoma!
 
Nadhani kwa vile unaitwa Reverend/ Mchungaji basi yeye anakuweka ktk lile kundi la wahudumu wa Mungu waliosema Kikwete ni chaguo la Mungu....
 
Huyo jamaa Musharraf, alikuwa na kitu cha kujibu huko kwenye Bunge lake, Je Kikwete alikuwa ana kitu gani cha kujibu toka kwa wabunge wa TZ?
 
Shy,

Umekuwa ukiongea kana kwamba unanifahamu na hii si mara ya kwanza kunizushia kuwa nilimpamba Kikwete na kumpandisha chati.

Hata majuzi nilikuuliza ni nani nilimpigia kura 2005, ukatoa majibu kama uliyoyasema hapa juu.

Kwa miaka miwili uliyokuwa unanisoma hapa JF, labda hata kama ulikuwa kule BCS, je ni kipi kilichokupa hoja kudai kuwa mimi nilimpa baraka Kikwete?

Kuna mawili, ama unatafuta mtu mpya kujibishana au kama si hivyo, basi una upeo mdogo kuelewa ninachoandika na maandiko yangu yoote uliyoyasoma!

Rev.Pole sana naona umevamiwa na ebola .Huyu kijana ndivyo alivyo achana naye wewe mwaga nyeti tu .Nakuunga mkono kwamba it is time JK to step down .Niko Dodoma nimemuona LIVE lakini I was shocked na ushahidi ni huu kwamba ndiyo naanza kuandika sasa .Sijajua kwa nini anaogopa hadi anatumia Bunge kupiga Kampeni kama kuna maendeleo ya ahadi zake sisi tunaweza kusema lakini kulia lia sidhani kama msaada .Tuko macho
 
REV:

Hapana si kikwete bali mbunge mwenye machungu ange resign leo ubunge wake nakaenda kuanzisha movement ya ukombozi.

Mbunge mwenye MACHUNGU yani (LULU) hawezi changamana na Nguruwe ktk zinzi moja na kupokea posho kutoka serikali asiyoridhika nayo.

Maana kama ni lulu usizitupie nguruwe maana watazikanyaga kanyaga lulu na kuwageukia na kuwalalua.

Hao wabunge wote humo hakuna kitu, lao moja tu posho na umaarufu. Kama Rais kashindwa ajiuzulu pia na wabunge wote wajiuzulu hakuna lolote wanalofanya humo bungeni.
 
Hamna lolote kwa huyu jamaa JK, tumechoka sana na utawala wa hovyo wa huyu jamaa. Hadi vitumbua ambavyo vilikuwa vinauzwa sh 20 kwa sasa sh 100. Jamani kuna kazi hapa?
 
mkamap,

Hizi comments zako ni za kwenye Dunia ya kufikirika zaidi kuliko ya kweli. Wenye nia na uwezo wanaweza kufanikisha mambo kutoka ndani ya System, hawahitajiki ku-resign. Ni vigumu kujaribu kufanya mabadiliko ukiwa nje ya System.
 
Hamna lolote kwa huyu jamaa JK, tumechoka sana na utawala wa hovyo wa huyu jamaa. Hadi vitumbua ambavyo vilikuwa vinauzwa sh 20 kwa sasa sh 100. Jamani kuna kazi hapa?

kasema mafuta juu ama hukumsikia ? That was a justification ya ugumu wa maisha na yeye kukwepa jukumu la maisha bora kwa kila Mtanzania .Unajua mimi sijaelewa kwa nini leo Rais aliamua kuhutubia Bunge and from the start he was looking so nervous .Hivi alikuwa na sababu gani ya kukagua kwanza gwaride pale nje ama ni mikwara ile kwa wale wana Zanzibar walio kuwa wanalia lia ?
 
Date::8/21/2008
Mabilionea wa EPA wapewa muda wa kuendelea kupumua
*Waongezewa muda kulipa fedha fedha walizopora Benki Kuu

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amewaongezea muda watuhumiwa wa ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT) kwamba hadi Oktoba 31 wawe wamelipa fedha hizo.

Katika hotuba hiyo ya pili kutolewa na Rais kwa Bunge tangu ile aliyotoa Desemba 30 mwaka 2005, kwa sehemu kubwa imegusa maeneo mengi yaliyotarajiwa.

Katika hotuba yake hiyo ilichukuwa zaidi ya matatu, Rais alionyesha huruma dhidi ya mafisadi wa EPA kwa kisingizio cha haki za binadamu, aliwapa muda wa mwisho wa kulipa fedha walizoiba ambao ni Oktoba 31, vinginevyo Novemba Mosi watafikishwa mahakamani. :(:(

Hata hivyo, akijaribu kuonyesha ukali, Rais akiwa ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, alisema tayari watuhumiwa wengi wa Sh 90.3 bilioni kati ya 133 ambazo uchunguzi wake umekamilika, wamezuiliwa hati zao za kusafiria, magari na nyumba zao kukamatwa.

"Sasa nizungumzie EPA..., Agosti 18 nilipokea ripoti kutoka katika timu niliyounda, nimeipitia, lakini kuna mambo nimeagiza, moja ni kwamba wote waliopata fedha hizo wawe wamelipa ifikapo Oktoba 31, vinginevyo Novemba Mosi ni mahakamani tu," alionya na kuongeza.

"Msione ma-gentle men wanapita mitaani wamefunga tai, tayari wengine tumewafilisi, tayari magari, hati za kusafiria na hata nyumba zao zimekamatwa, matajiri wa EPA wana hali mbaya kweli".
:(

Rais alifafanua kwamba, katika uchunguzi huo ulihusu maeneo mawili, ufisadi wa Sh90.3 bilioni uliofanywa na makampuni 13, ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati batili na makampuni tisa, ambayo yalilipwa Sh 42 bilioni ambazo uhalali wake una mashaka.

Aliongeza kwamba, uchunguzi kuhusu Sh 90.3 umekamilika, lakini ule wa Sh 42 umekamilika kwa ndani nje ukiwa bado na kuongeza kwamba, hadi sasa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kupata taarifa zaidi za watuhumiwa.

Rais alisema Jeshi la Polisi kwa kutumia utaratibu wa kusaidiana na majeshi ya nchi nyingine, ilituma taarifa zaidi katika nchi ambazo wahusika wa makampuni hayo wanaelezwa kuwepo, lakini hadi uchunguzi unamalizika hawakuwa wamepata majibu.

Hata hivyo, bado wingu limetanda kwani takwimu za fedha alizopewa Rais zinapingana na zile ambazo timu hiyo ilitoa miezi mitatu baada ya kuanza kazi kwani ilisema ilikusanya Sh60 bilioni na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM)kilisema zimerudishwa Sh64 milioni tofauti na Sh53 ilizotolewe katika ripoti aliyopelekewa rais Agosti 18. :(:(

Akizungumzia historia ya fedha za EPA, pia alitangaza kwamba fedha zote za akaunti hiyo zitakuwa chini ya mikono ya serikali ili kuondoa uwezekano wa kutokea ufisadi kama wa awali na kuongeza kwamba, baada ya timu kueleza kwamba hadi sasa zimepatikana zaidi ya Sh53 bilioni, alihoji vipi haziwekwi katika mfuko mkuu wa Serikali, lakini aliambiwa kuwa si za serikali.

"Kumekuwa na maneno ya hapa na pale, hizi fedha ni za nani, za serikali au si za serikali, hizi ni fedha za watu, hata timu iliponikabidhi ripoti nikauliza, mmepata kiasi gani wakaniambia Sh53 bilioni, nikawauliza mnazo, wakasema ndiyo," alisema na kuongeza:

"Niuliza mbona hamjaziwea katika Mfuko Mkuu, wakasema si za serikali, zitakuwa za serikali labda ikizichukua, hadi sasa zipo katika akaunti maalumu hazina".

Rais alifahamisha kuwa serikali haiwezi kufanya makosa zaidi kwa fedha za EPA kwani wizi wa awali ulitokana na kukosekana uangalizi zilipohamishiwa BoT kutokea iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hapo mwaka 1985.

Alitangaza kwamba, fedha hizo sasa zitakuwa chini ya mikono ya serikali na zitaelekezwa katika utoaji mbolea ya ruzuku na uimarishaji wa Benki ya TIB na kuongeza kwamba, ndani ya BoT zipo zaidi ya Sh200 bilioni.

Rais alisema serikali itazichukua na kuzitumia huku kila mwaka ikitenga bajeti ambayo italenga kuweka mazingira sawa ya malipo kwa wahusika pindi wakijitokeza. na kuongeza kwamba, inawezekana wasijitokeze wadai kutokana na kwamba tayari wengine wamekufa, lakini akasema serikali itaweka bajeti kwa tahadhari pindi wakijitokeza wenyewe.

Takwimu za serikali zinaonyesha, mwaka 1999 deni katika EPA lilifikia dola 623 milioni, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na 298 ni riba na baadaye deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.

Hata hivyo, chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai, wapo waliokubali na wengine na hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.

Ufisadi katika EPA ulibainika baada ya ukaguzi wa awali wa Kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini, ambayo iliibua katika malipo ya Sh 40 bilioni kwa Kampuni ya Kagoda, hata hivyo BoT ikasitisha mkataba.

Baadaye, baada ya tuhuma hizo kuibuliwa bungeni, serikali ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta Kampuni ya kimataifa ya Ernst&Young, kufanya ukaguzi ambao ulibaini ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika hesabu za mwaka 2005/06 ndani ya BoT.

Kufuatia ufisadi huo, Januari 9 Rais alitangazia umma kuunda timu chini ya Mwanyika na kuipa miezi sita ambayo ilimkabidhi ripoti Agosti 18.
 
Shikamoo,

LEO nimeamua kuandika waraka huu kwako Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka inayokaribia mitatu sasa tangu ushinde na kuapishwa mwaka 2005 baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu.

Napenda kutumia fursa hii kukupa pole kwa kazi ngumu ya kuongoza kundi la watu wengi wenye njaa ya tumbo, njaa ya ubongo na njaa ya tiba bora.

Hakika njaa zinazowakabili Watanzania ni nyingi na hazina ukomo, hasa zikiainishwa kwa nafasi binafsi, kaya, kata, kijiji, miji, majiji na taifa kwa ujumla wake.

Ni mnafiki pekee anayeweza kukudanganya, au wewe mwenyewe kudanganyika (ingawa hili najua siyo rahisi kwako kwa kuwa umeyaishi maisha ya wengi wetu), kwamba mambo ni shwari kila mahala. Kwamba HAKUNA MATATA.

Nakumbuka vyema, na bahati nzuri bado ninaendelea kuirejea hotuba yako ya mara ya kwanza Bungeni Dodoma ambayo ilisheheni ahadi na namna nzuri ya kumpunguzia Mtanzania ufukara (unaojumuisha njaa zote alizonazo).

Kila Mtanzania aliyekusikia siku ile ukiwa umetulia na kuisoma vyema, atakubaliana nami kwamba hotuba ile ndiyo ilikuwa dira yenye mwanga wenye miali ya kuchoma na kuunguza kero nyingi za watu wako waliokuchagua, hata wale wasiokipenda chama chako – CCM, kwa kura za kishindo.

Ni hotuba ile iliyohuisha hatma ya maisha yao iliyokuwa imefikia mahali pa kuonyesha kukata tamaa, hata kama waliokutangulia walikuwa wakitamba kwa hadithi za kukua na kuimarika kwa uchumi mkuu, ilhali maisha ya watu yakiendelea kudhoofika.

Kadri miaka ilivyokuwa ikisonga, hasa ule mwaka wa kwanza, matumaini ya watu wako yaliendelea kukupa muda kwamba neema ya kweli yaja. Hakuna aliyeonekana kuwa na haraka ya hiyo neema iliyoonekana katika hotuba yako na hata dhamira yako iliyojionyesha kuchukizwa na umaskini wao.

Hata hivyo, ikiwa miaka mitatu inakaribia kukatika, asilimia kubwa ya matumaini waliyokuwa nayo watu wako wengi, kwamba wewe ndiye mkombozi aliyepo, inapungua kwa kasi ya kutisha, hata kama wasaidizi wako, hasa wale wanafiki na wanaojipendekeza watakueleza vinginevyo.

Uhakika ni kwamba hata wewe unalitambua hilo kupitia kwa watu wako wengine wa karibu, wale wanaoitwa –mawaziri wa jikoni wa rais-hasa wanafamilia uliowapa jukumu la kukusanya ‘maneno’ ya watu wako huku kwetu mitaani.

Kasi ya kupungua kwa asilimia kubwa ya matumaini ya watu wako yanajiegemeza katika matukio mabaya yaliyoikumba nchi yetu, yakiwa yanafanywa ama na wasaidizi wako, uliowachagua kwa imani kubwa, au wafanyabiashara wenye kuhusiana nao.

Hilo halina kificho na wala hakuna haja ya kukueleza vinginevyo, kwani hata wao wenyewe walitambua na sina uhakika kama walijutia kuhusika kwao na dhambi za kuongeza ufukara kwa Watanzania, lakini angalau waliamua kuachia ngazi kwenye madaraka uliyowapa na wengine kuikimbia nchi, wakijificha huko walikotanguliza ‘vijisenti’ walivyowaibia watu wako.

Ufisadi. Ufisadi. Ufisadi. Hii ni dhambi ambayo imekuwa ikilaaniwa na wapenda nchi yao, ikiwa inabeba na dhambi nyingine nyingi, ambazo zimekuwa, siyo kero tu, bali mzigo mzito wa gharama za maisha kwa watu wako.

Ni ufisadi huo ambao umeongeza bei ya umeme, bei ya vyakula, ada kwa watoto wetu, nauli kupanda na hakika umegusa kila sehemu ya maisha ya wananchi wa Tanzania, kiasi kwamba serikali nzima unayoiongoza ikaonekana inachusha kwa kila mtu, isipokuwa mafisadi wenyewe, wake zao, watoto wao na hata vimada wao.

Sasa leo wakati utakapokuwa ukilihutubia Bunge, mjini Dodoma, watu wako wenye kukata tamaa, wanataka uongee. Wanataka uzungumzie masuala yanayowakera kila uchao kwa sasa. Hawataki siasa ambazo tumezizoea zinazotolewa na viongozi wetu wanasiasa.

Wananchi wanataka kusikia namna unavyochukia ufisadi kwa dhati ya moyo wako. Wanataka kukusikia na kukuona ukikunja ndita kuwalaani na kutoa amri kuu ya kuwachukulia hatua kali mafisadi wote wanaofifisha juhudi binafsi ulizoanza kuzionyesha mwanzo wa uongozi wako.

Binafsi, msema kweli mpenzi wa Mungu, nikushangae kidogo kwa kushindwa hadi sasa kuwakemea wakuu wafuatao; Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kwa kushindwa hadi sasa kuwakamata watu walioandikwa katika ripoti uliyokabidhiwa majuzi juu ya uchunguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya je (EPA).

Kwamba kwanini hadi sasa hawajawaadabisha mafisadi wake wakati timu yao imekamilisha kazi? N’nachojua mimi ni kwamba wao kwa kazi zao wangekuwa wamewakamata watu hao kwanza na ndipo baadaye wakupe ripoti hiyo.

Polisi wanatakiwa kuwakamata wahalifu hao, baada ya Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Takukuru kuthibitisha kuwa walihusika na wizi huo, sasa wanasubiri nini au mpaka uwaeleze wawakamate watu hao? Wao wanafanya kazi gani, yaani kukupa ripoti basi? Wanasubiri nini? Au nao tuseme wako pamoja nao kama tulivyoshuhudia baadhi yao wakitetea wizi ambao bado unasumbua kupatikana kwa neema ya Tanzania?

Kama hawajawakamata tuseme hawajawatambua hadi sasa. Ikiwa ripoti hiyo imejaa maneno matupu kama ya ukasuku wa wanasisa, tafadhali achana nayo kabisa na usiisome kwani itakuondolea zaidi asilimia za imani kwa wananchi wako.

Idadi kubwa huku mitaani tunakopita na kuzungumza na wapiga kura wako, wengi wanaonekana kushangaa timu hiyo uliyoiunda, kwamba inasubiri nini.

Mbali na hilo, wananchi wanatarajia kuwa utazungumzia na kutoa msimamo juu ya ‘mgogoro’ wa Muungano, hatma ya maslahi kwa wafanyakazi na zaidi sana suala zima la neema kwa kila Mtanzania.

Rais Kikwete, vitabu vitakatifu, ambavyo naamini unavithamini na ndiyo mwongozo wako, kabla ya Katiba, vinasema kuwa ukiona maovu yanatendeka, basi yazuie hata kwa upanga ili yasiendelee, ukishindwa yakemee hata kwa ulimi na ukishindwa kabisa, basi onyesha kuchukizwa na kuchukua hatua, hata kwa kupitia wengine.

Hatua za namna hii, zimetumiwa zaidi na Rais wa Rwanda Paul Kagame na hatimaye sasa nchi hiyo iliyokuwa imegubikwa na vita, inapanda kwa kasi katika chati yake ya kuwaletea neema wananchi wake.

Utakapofaya hivyo, hakika utakuwa umemtendea haki Mungu Mkuu na waja wake Watanzania na thawabu zitarundikana katika fungu lako.

Nakutakia kila jema uwapo Dodoma na unapojiandaa kwa safari yako ya Marekani.

Wasalaam

Simon Martha Mkina
Simu: 0754 020880
Email: smkina@gmail.com
Blog:www.mkina.bloghspot.com

(Waraka huu umechapishwa katika gazeti la Kulikoni la leo) Tumeiweka hapa kwa hisani ya gazeti.

Kamanda siku za nyuma nilikuja hapa na nikasema niliyo yaona Rwanda , Tanzania hayawezekani hata mara moja na hasa kwa jina la Umoja na Amani na Utawala Bora .Hii ni kinga tu na hakuna atakalo weza JK na Kagame ni mwisho kabisa hata JK hamkaribii hata kidogo .
 
nigekuwa mmiliki wa wagazeti nisinge andika hizi pumba za mweshimiwa,kesho magazeti yote yangekuwa na habari za kawaida tu.
 
Rais anamuogopa rostam Aziz. Ukiona kwa undani Rostam yumo kwenye ile makampuni ambayo wanangoja taarifa kutoka nje.

HAYUMO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lakini angekuwa JKN msingeweza hata kuandika hivi tunavyoandika! Kulikwa hamna uhuru wa vyombo vya habari na hamna uhuru wa mawazo. Shukuruni JK ameruhusu hili.
 
ndio sababu wa bongo tutakufa na umasikini porojo zetu zimezidi. Hivi njaa magojwa ujinga uzembe kwetu sio adui eeeeeeeeh
 
Back
Top Bottom