Kikwete; Spare the back benchers!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Mheshimiwa Rais Kikwete,

Ombi rasmi mkuu. Unapounda baraza lako jipya, tuachie wale Wabunge wetu maarufu kama bakibencha. Usiwa-Bangusilo na kuwapa Uwaziri.

Twaomba wafuatao wasiwemo katika baraza lako jipya: Anna Kilango, Harrison Mwakyembe, Lucas Seleli, Manyanga, Zitto, Slaa na wengine ambao wameonekana kuisulubu Serikali!

Mimi Raia Mkosoaji wa Serikali yako,
 
Nafikiri jambo busara hawo wakipewa nyadhifa za uwaziri itakuwa motivation kwa new backbenchers kuwa ukiwa mkosoaji basi utapewa uwaziri...lakini ukiwacha bila kuwapandisha cheo watafikiri kuwa wako penalised.
 
Hawa watu akina Zitto, Mwakyebe Dr.Slaa tunawahitaji sana maana bado kuna hii ngoma nzito ya KIWIRA inayomkabili huyu fisadi maarufu MKAPA BEN ambaye alishasema yeye hababaishi na mtu. Wakati umefika wakumwosha kuwa Tanzania ni mali ya watanzania wala sio ya walio wachache tu.Mkapa alisahau kuwa nchi hii ina sheria na wanasheria ambao wanaijua sheria na wako tayari kuitetea na kuilinda. In fact he is above the law how can someone like him register his own company using State House as his principal office for his business kama sio kudharau wantanzania?
 
Rev. Kishoka,

Sitashangaa akiwapandisha na kuwapa uwaziri. Kwa Tanzania ukitaka kupanda inatakiwa uikosoe sana serikali bungeni na wala sio kuwajibika kwa nguvu
kwa wananchi waliokuchagua.

Hata hawa wakichaguliwa kuwa mawaziri tutaona yale yale ya siku zote, wataanza kutetea uozo mbalimbali wa serikali na pia utendaji wao kuwa mbovu.

Kuna haja ya kuwa na back benchers wenye nguvu ili vyombo vyote viwili (bunge na serikali vifanye kazi zake kwa ufanisi).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom