Zhule, umeongea makubwa na yaliyo kweli mtupu. Mi binafsi nakuunga mkono 100%. Sisi waafrika tunahitaji KUJIKOMBOA KIFIKRA. Bado kasumba za kikoloni zinatutafuna, na zitaendelea kututafuna. Tunapenda kuwa mabwana tukipata nafasi, na kupalilia ubinafsi - ufamilia badala ya Utaifa. Huko tutatoka lini? Kazi ipo kwelikweli.Tatizo letu weusi nafikiri ni ile ubwana tuliyorithishwa na wakoloni.watu waliyopata unyapara walikura daraja la pili. wazungu walikuwa daraja la kwanza. walipoondoka wazungu watawala wakawa ndo daraja la kwanza.hii hali haijatoweka miongoni mwa watu weusi, bado inatutafuna.watumishi wanadhani wao ni bora kuliko wengine kwaiyo wanahitaji vingi kuliko wengine.Watumishi hawajibiki kwa umma kama ilivyokuwa enzi za ukoloni. Kikwete na watu wake wanajifanya mabwana na si watumishi.Mkuu wa jeshi mwanasheria mkuu, usalama, makatibu wa kuu, mawaziri,wakurugenzi, wabunge, wote ni mabwana.Kwaiyo mwananchi yupoyupo tu kupiga kura basi. Mikataba ya mali ya umma ni siri. Dhana ya mali ya umma iko wapi?Ni mali ya mabwana.Wananchi hatuna chetu. Kama mali ni yetu mikataba isingekuwa siri. Kwaiyo wakina kikwete na mawaziri kwa sababu ni mabwana mikataba kwanza lazima iwafaidi wao basi na si umma. Tuanze upya.Kila mwananchi anakijanawake lazima naye awe na maisha mazuri siyo kijana wako kuwa mtumishi wa kijana wa mwanamke mwingine.Vita vya iddi amini watanzania wote walishiriki kwa kutoa maisha yao na mali yao na siyo mrisho kikwete,RA, lowasa,mramba, peke yao.haitawezekana kamwe. NIMEWAKILISHA