Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Asante sana mwanakijiji kwa mamala yako iliyotulia. Hakika Mungu lazime awe na wateule wake kama wewe ambao wako tayari kusema ukweli kwa ajili ya taifa lake. Mukngu akubariki na kukulinda. Wanajidangana, hata waibe vipi, hawataishi milele, na siku moja hesabu yake watalipa hata mbele za Mungu. Big up!
 
Kama taifa kuna sehemu tulipotoka. Tuliwapa uongozi watu wanafiki wenye kujipendekeza kwa wakuu wao wakiwapiga vita na umbeya watu waadilifu. Tukasimamisha minara mingi iliyokuwa inapiga kelele kama madebe matupu. Haiingii akilini kuona watu waliokuwa mstari wa mbele kutekeleza ujamaa wamegeuka na kuwa wasaliti wakubwa wa taifa na wasio hata na chembe ya uzalendo kiasi hiki. Ninachosikitika zaidi ni kuona jinsi watu hao wanavyotumia resources za umma kuendeleza uongo ili kulinda maovu wanayofanya.Ukristu unatuambia wazi kuwa kitu chochote tunachojaribu kukisimamisha katika misingi ya uongo, lazima kitaanguka.Wanasiasa sasa n muhimu kuwa makini.Watu wanaona na kujua yote mnayofanya mkifikiri ni siri.
Namkumbuka Sani Abacha na mabavu yake Nigeria.Inasemekana alikuwa na walinzi lukuki hivyo hakuna mkono wa mpinzani ulioweza kufika karibu yake. Lakini siku moja mkono wa mungu ulibadilisha equation..na NIgeria ikabadilka.
Trust me, CCM wasipoamua kubadilika watajilaumu wenyewe. Iko siku watanzania wataamua na wataamua waziwazi kuwakataa CCM.Hakuna system itakayoweza kuwazuia watanzania kuamua wanachotaka.Huu muda ulipo mi muafaka kujisahihisha. Hizi habari za kukosa uadilifu zimekuwa kero na kusababisha hudhuni kubwa miongoni mwa watanzania.
 
Sijui kwanini tunazungushana na kudai watu wote walioatajwa kwenye orodha ya Ufisadi wanastahili isipokuwa Rais Kikwete! Hata viongozi wanaotambua baadhi ya uzito wa tuhuma zilizotolewa na wanaodai kuwa zitiliwe maanani hujikuta wanajing'ata ng'ata kuhusu Rais Kikwete. Baadhi ya watu wamefikia mahali pa kulaumu kina Dr. Slaa kumuweka Kikwete katika kundi hilo kwani JK ni safi! Hata hivyo ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa JK siyo safi na yeye ndiyo awe wa kwanza kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake!

a. Mkataba wa IPTL ulisainiwa yeye akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Hakuna mkataba mbovu kama huo. Kushindwa kwake kutetea maslahi ya nchi akiwa Waziri na kulisababishia Taifa hasara kubwa ilikuwa ni kilele cha kutokuwajibika na kushindwa kuongoza. Akiwa Waziri mwenye dhamana ya nishati Ndg. Kikwete alitakiwa kuhakikisha kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inaingia kwenye mkataba ambayo inaweza kujitoa pasipo kupata adhabu kubwa. Alishindwa hivyo na hivyo kuoneshe kutokuweza kusimamia maslahi ya nchi.

b. Wakati Rada ya bilioni 50 inanunuliwa, Ndg. Kikwete alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa na wakati sakata lenyewe linaanza alikuwa ni Waziri wa Fedha. Akiwa Waziri mwenye dhamana hiyo alishindwa kabisa kufuatilia ukweli kuwa kampuni ya BAE siyo mali ya serikali ya Uingereza na ya kuwa rada yenyewe ilikuwa imeongezwa kwa asilimia 24. Kiasi hicho kinakaribiana kabisa na wastani wa asilimia 20 za fedha za umma zinazopotea katika manunuzi ya serikali (public procurement).

Alishindwa kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa letu yanalindwa na alipopata nafasi ya kuonesha busara aling'aka na kusema "kwanini sisi ni idara ya Benki ya Dunia? ni kututukana kudai kuwa tusubiri Benki ya Dunia kutuamulia nini kinatufaa".

Ndio maana leo hii anapokuja na kuzungumza kuwa hawezi kuamini kuwa nchi kama Uingereza inaweza kuacha kampuni "yake" kurusha rada hiyo kwa bei hiyo wengine tunamshangaa kwani alikuwa na nafasi zaidi ya 20 ya kuweza kupinga ununuzi huo lakini alikuwa ni kinara wa kutetea tenda hiyo ya rushwa! Ni kuelewa hilo ndio utaona ni kwanini hakutaka watu wamuulize Rais Mkapa juu ya suala la rada, kwani miongoni mwa wahusika wakubwa ni yeye mwenyewe Kikwete.

c. Kama nilivyoonesha hapo juu kuwa Rais Kikwete aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Kwa hivyo nina uhakika kabisa alikuwa anajua kabisa jinsi mikataba inavyoingiwa na alikuwa na kila sababu ya kuhakikisha kuwa mikataba inalinda maslahi ya nchi na kunufaisha nchi wakati inawapatia wawekezaji faida ya kibiashara. Kwa kitendo chake yeye mwenyewe kuwa ukaribu na wafanyabiashara hao hasa swahiba wake ambaye ni mmiliki mkubwa wa ardhi yenye vito na madini Bw. James Sinclair, Rais Kikwete tangu akiwa Waziri wa Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje amekuwa mtu aliyetiwa upofu na "dhahabu".

Wakati Rais Mkapa na Yona wanajipatia tenda ya Kiwira, Rais Kikwete na Msabaha walikuwa wanajisogeza karibu na Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration ambapo kuna madai (yanayothibitishwa na taarifa za SEC na EDGAR) kuwa Msabaha na Kikwete walikuwa na "hisa" za kiasi fulani. Kampuni hiyo ya TRE iliingia mkataba na Barrick Gold kuwa inapovumbua madini katika ardhi inayomiliki basi Barrick wanakuwa wanunuaji wa kwanza.

Ni wao TRE waliouzia Buzwagi kwa Barrick na maeneo mengine kadhaa kwa makampuni mengine. TRE inaponufaika kwa mikataba mibovu ambayo serikali inaingia na makampuni ya uchimbaji kuna watanzania wawili ambao nao wananufaika (ni wazi wapo wengine na wengine ni vigogo wengine) na dili hizo.

Ni kwanini Barrick walikuwa wa kwanza kukubali mabadiliko ya vipengele vya mikataba yao? jibu ni ushawishi wa James Sinclair na Kikwete ili kutetea kilicho chao. Kwa yale makampuni ambayo hayana ukaribu wa James Sinclair na Kikwete (JK alimualika JS kwenye kuapishwa kwake na mara nyingi amekuwa mgeni wake akija US, na binti ya JS aliyeko Tanzania ni rafiki wa karibu...) basi imekuwa vigumu kuwashawishi kubadili vipengele hivyo.

Ndio maana hadi leo hii si kweli kuwa kupitia vipengele na kuzungumza na "wakubwa" hao kuhusu mikataba kumekoma kama alivyodai mjasiriamali mwingine Nazir Karamagi alipokuwa akijaribu kupangua hoja za Zitto. Ukweli ni kwamba kamba waliitundika wenyewe serikali na ni wenyewe walioziweka shingo zao humo! wawekezaji wanatishia kuondoa kigoda!! Serikali inabembeleza!!

Anapozungumzia matatizo ya mikataba Rais Kikwete anazungumzia kana kwamba tatizo ni kipengele kimoja tu! Hajachukua muda kufuatilia uzito wa hoja hizo kwani kwake ni kelele!

d. Kikwete si Safi kwani amewalinda watu wachafu! Waswahili walisema ukiwa na urafiki na wezi, usishangae watu wakakuhisi na wewe mwizi! Rais Mkapa anapomlinda mjasiriamali Mkapa, aliposhindwa kumsimamisha kazi mara moja Ditto na kuamua kumuacha ajiuzulu huku akiendelea kupata mafao yake alionesha udhaifu mkubwa wa uongozi!

Rais Kikwete amekuwa mtetezi wa wabadhirifu akikesha kutoa vitisho hewa akijaribu kutetemesha mabua na kuangusha vichuguu huku milima ikiendelea kuganda theluji! Ukimya wake kama ule wa Mkapa ni ishara wazi kuwa walifeli darasa la Mwalimu!

Anapoona kuwa madai ya ubadhirifu Benki Kuu, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, n.k kuwa "kelele za upinzani" na kuwa "ndiyo demokrasia" anaonesha udhaifu mkubwa usiomstahili kiongozi wa nchi. Haiwezekani upotevu wa mabilioni ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka kuwa viwe ni "kelele" tu!

Rais ni lazima we mtu ambaye hapuuzii masuala mazito na hayafanyi kuwa ni ya kijinga. Kwa mtu kuwa mpinzani hakuifanyi hoja yake kuwa "kelele". Leo hii wana CCM wenzake wanazungumza wazi kuhusu tuhuma hizi na kudai kuwa wanaotuhumiwa (akiwemo yeye mwenyewe) wajibu siyo suala la kupuuzia!

e. Rais Kikwete ameonesha na anaendelea kuonesha udhaifu mkubwa wa maamuzi hasa kwa kuwa mtu wa kusita sita na ambaye yuko tayari kutumia uwezo wake wote kutofanya lolote. Hivi hadi nini kitokee ndipo Rais Kikwete atajua kuwa mambo haya si ya kupuuzia? Wakati Lowassa ameenda kukutana na Karamagi kule London na mkataba wa Buzwagi ukasainiwa je Rais Kikwete alifahamu ujio wa Waziri wake Mkuu? Je walikutana? Kama Rais hakujulishwa kutiwa saini kwa mkataba mkubwa namna hiyo na Waziri Mkuu anakutana na Waziri mwingine pasipo ujuzi wa Rais je haoni ni ukosefu mkubwa wa kiutawala!? Lowassa alifuata nini London na kukutana na Karamagi badala ya kukutana na Rais?

Leo hii watu wakihoji mazingira ya kusainiwa mkataba huo kwanini hiyo iitwe kelele!

Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete. Kosa hilo vizazi vijavyo vitasimulia kama hadithi, kuwa "hapo zamani za kale kulikuwa na mwana CCM mmoja ambaye aliwapo watu matumaini sana kabla ya uchaguzi. Watu wengi waliamini kuwa mwanaCCM huyo ndiye atakuwa mkombozi na kiongozi wa kuwaonesha njia ya kufikia nchi ile ya ahadi. Walipomchagua kwa asilimia 80 ya wapiga kura, Watanzania walijawa na matumaini... Miaka miwili baadaye watanzania walishika vichwa vyao kujuta, kwani waliyemdhania ndiye kumbe siye... !! "....

Kama Rais Kikwete hatabadili mwelekeo wa uongozi wake, na kama ataendelea kufanya kazi kana kwamba madai na hoja zinazojengwa ni "kelele" tu na hivyo kuendelea kufumba macho ufisadi unaoendelea nchini (na hapa simaanishi rushwa ya kutoa na kupokea tu, namaanisha matumizi mabaya ya madaraka, n.k) basi ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa Rais Kikwete hapati nafasi ya pili ya kutoitumikia Tanzania. Endapo atagundua upotofu wa uongozi wake na kusahihisha mapema ndani ya miezi sita ijayo yawezekana akajiokoa na kuukoa urais wake. Vinginevyo, Rais Kikwete atakuwa ni Rais wa kwanza kutawala kwa mhula mmoja!!

sikumbuki kama nimwahi kuchangia hii topic, ninachofanya narudia rudia wee, kuisoma.Acha leo niseme kuwa nimeisoma tena. na ninaona kuna mambo mengi mno. Kama ningekuwa na fund, halafu nikawa mtu wa sociology basi hapa ningepata title ya reserch more that 10 titles.LAKINI ZOTE CONCLUSION YAKE INGEKUWA KIKWETE SIO SAFI SO AS CCM.
 
sikumbuki kama nimwahi kuchangia hii topic, ninachofanya narudia rudia wee, kuisoma.Acha leo niseme kuwa nimeisoma tena. na ninaona kuna mambo mengi mno. Kama ningekuwa na fund, halafu nikawa mtu wa sociology basi hapa ningepata title ya reserch more that 10 titles.LAKINI ZOTE CONCLUSION YAKE INGEKUWA KIKWETE SIO SAFI SO AS CCM.


hivi hata sielewi kama naota au nasinzia! Waberoya u were the last person to post in that thread.. sasa mbona una tuaccuse kuwa hatumgusi Kikwete?
 
Kama Kikwete angekuwa safi, basi Ikulu isingekuwa inapoteza muda wake na resources kutangaza mambo kama haya hapa chini:

Ikulu yaeleza aliyoyafanya Kikwete kuhusu Richmond

Na Leon Bahati

SIKU chache baada ya baadhi ya wanasiasa kumhusisha Rais Jakaya Kikwete na kashfa ya utoaji wa zabuni kwa kampuni tata ya Richmond Development LLC, Ikulu imetoa msimamo wa kumtetea huku ikitaja mambo manne ambayo alihusika nayo.

Msimamo huo wa Ikulu ulitolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana, akisisitiza Rais Kikwete hakuhusika kwa namna yoyote ile ya kufanikisha zabuni hiyo kutolewa kwa kampuni hiyo tata.

"Katika siku za karibuni kumekuwepo na maneno na vijembe ati kuwa, kuna mkono wa Rais Jakaya Kikwete katika kutoa tenda (zabuni) ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopata Kampuni ya Richmond," alisema Luhanjo akisisitiza:

"Tunapenda kusema tena kwa msisitizo kuwa maneno hayo si ya kweli na hayana msingi wowote. Rais hajahusika na uamuzi wa tenda hiyo kupewa Richmond kama vile ambavyo hakuhusika na kupewa tenda kwa Kampuni za Aggreko na Alstom."

Luhanjo alitaja mambo manne ambayo Rais Kikwete alihusika katika suala zima la ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme ikiwemo ya Richmond: Kwanza, katika kuamua Tanesco itumie mitambo ya kukodi kuzalisha umeme na serikali igharamie ukodishaji huo.

Suala hilo lilikuwa lazima liamuliwe na yeye kwa sababu lilikuwa linahitaji serikali kugharamia ukodishaji. Kama si hivyo lisingefikishwa kwake kwani ni jambo ambalo lingekuwa juu ya Tanesco kuamua kukodisha na kulipia. Gharama hizo hazikuwa zimepangwa katika bajeti ya serikali, hivyo ilikuwa ni lazima kupata idhini ya rais ya kutafuta hizo pesa na kuzitumia kwa ajili hiyo.

Pili, Rais alihusika katika kuzungumza na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kuwaomba wakubali sehemu ya pesa waliyopanga kuipa Tanzania kama msaada kutokana na mpango wa msamaha wa madeni itumike kugharamia ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond (ambayo baadaye ikawa Dowans) na matumizi mengine ya dharura za umeme. Matumizi hayo mengine yalijumuisha pia ununuzi wa mitambo ya aina ya Watsilla ya kuzalisha megawati 100 za umeme pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Mitambo hiyo imeshanunuliwa, kufungwa na tayari inazalisha umeme.

Tatu, Rais alihusika katika vikao vya Baraza la Mawaziri vilivyojadili matatizo ya upungufu mkubwa wa umeme nchini na kuamua hatua mbalimbali zichukuliwe kukabiliana na tatizo hilo. Moja ya hatua zilizoamuliwa kuchukuliwa, ni hii ya kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme. Katika vikao hivyo vya Baraza la Mawaziri alitoa maelekezo ya mambo ya kuzingatiwa katika zoezi zima la kupata makampuni au watu watakaotoa huduma hiyo. Hususan, rais alisisitiza kuwa pamoja na udharura uliokuwepo Kanuni na Sheria ya Ununuzi wa Umma zizingatiwe.

Nne, Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya USD 10 milioni na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane. Rais alikataa maombi yaliyopelekwa kwake na Wizara ya Nishati na Madini ya kumwomba aagize Wizara ya Fedha, iilipe kampuni hiyo fedha hizo.

Rais aliagiza Wizara ya Fedha ibaki na msimamo wake na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tanesco wafanye mambo mawili. Kwanza, wafanye utafiti zaidi kujua undani wa Kampuni ya Richmond.

Isije kuwa ni kampuni bandia wakapewa fedha wakatokomea nazo na mitambo isipatikane na hakuna namna ya kuipata kampuni wala wahusika wake. Pili aliagiza wawatake viongozi wa Kampuni ya Richmond kwanza walete mitambo, ikishafika, ndipo walipwe. Maagizo hayo ya rais yalizingatiwa na Kampuni ya Richmond ikapewa sharti hilo. Lakini, ikashindwa kulitekeleza na kuishia kuingia mkataba na Kampuni ya Dowans iliyokuja kuleta hiyo mitambo badala yake.

Hivyo ndivyo alivyohusika rais katika suala zima la ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kwa makampuni ya Aggreko, Alstom na Richmond. Kama kweli kungekuwa na mkono wake wa upendeleo kwa Kampuni ya Richmond kupata tenda, iweje tena yeye ndiye akatae kampuni hiyo isilipwe fedha za kianzio mpaka kuifanya ishindwe kazi?

Wiki hii Ikulu ilikanusha Rais Kikwete kuhusika na kashfa ya Richmond ikiwa inajibu tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kwamba, rais anahusika na kashfa hiyo.
 
Kama Kikwete angekuwa safi, basi Ikulu isingekuwa inapoteza muda wake na resources kutangaza mambo kama haya hapa chini:

na alihusika vipi kuhusu kuileta Dowans? Hawa watu kwa kweli kwa maneno yao wenyewe wamethibitisha kuwa alihusika. The other day nilikuwa ninampa somo Dilunga kuwa unapojenga hoja hakikisha you don't commit makosa ya kimantiki na la kwanza kati yao ni kujipinga humo kwa humo (internal contradiction). Sasa hawa wanasema Rais hakuhusika halafu wanatoa ushahidi wa Rais kuhusika!
 
na alihusika vipi kuhusu kuileta Dowans? Hawa watu kwa kweli kwa maneno yao wenyewe wamethibitisha kuwa alihusika. The other day nilikuwa ninampa somo Dilunga kuwa unapojenga hoja hakikisha you don't commit makosa ya kimantiki na la kwanza kati yao ni kujipinga humo kwa humo (internal contradiction). Sasa hawa wanasema Rais hakuhusika halafu wanatoa ushahidi wa Rais kuhusika!

Lazima wamsafishe kwa kila hali maana wanajua 2010 ndiyo inasogea taratibu. Akiulizwa ni lipi alilofanya katika kutetea maslahi ya nchi na Watanzania tangu aingie madarakani 2005 sidhani kama atakuwa na lolote la kuzungumza, lakini Watanzania tukiulizwa ni madhambi yepi ambayo alishindwa kuyashughulikia tangu aingie madarakani na hivyo kushindwa kutetea maslahi ya nchi yetu basi tunaweza kujaza kurasa chungu nzima. Hii njemba Shibuda inawapeleka puta sana wanamtandao sasa inabidi waanze kumsafisha mtu wao.
 
Last edited:
Kikwete anasingiziwa tu. Huyu jamaa yuko safi kabisa na hana doa hata moja na ndiye anafaa kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
 
Kikwete anasingiziwa tu. Huyu jamaa yuko safi kabisa na hana doa hata moja na ndiye anafaa kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo.

Richmond (houston)-----Daraja(barozi usa)-----kikwete--deligation--Lowasa-deligation---Karamagi/msabaha/tendering panel
 
Tatizo letu weusi nafikiri ni ile ubwana tuliyorithishwa na wakoloni.watu waliyopata unyapara walikura daraja la pili. wazungu walikuwa daraja la kwanza. walipoondoka wazungu watawala wakawa ndo daraja la kwanza.hii hali haijatoweka miongoni mwa watu weusi, bado inatutafuna.watumishi wanadhani wao ni bora kuliko wengine kwaiyo wanahitaji vingi kuliko wengine.Watumishi hawajibiki kwa umma kama ilivyokuwa enzi za ukoloni. Kikwete na watu wake wanajifanya mabwana na si watumishi.Mkuu wa jeshi mwanasheria mkuu, usalama, makatibu wa kuu, mawaziri,wakurugenzi, wabunge, wote ni mabwana.Kwaiyo mwananchi yupoyupo tu kupiga kura basi. Mikataba ya mali ya umma ni siri. Dhana ya mali ya umma iko wapi?Ni mali ya mabwana.Wananchi hatuna chetu. Kama mali ni yetu mikataba isingekuwa siri. Kwaiyo wakina kikwete na mawaziri kwa sababu ni mabwana mikataba kwanza lazima iwafaidi wao basi na si umma. Tuanze upya.Kila mwananchi anakijanawake lazima naye awe na maisha mazuri siyo kijana wako kuwa mtumishi wa kijana wa mwanamke mwingine.Vita vya iddi amini watanzania wote walishiriki kwa kutoa maisha yao na mali yao na siyo mrisho kikwete,RA, lowasa,mramba, peke yao.haitawezekana kamwe. NIMEWAKILISHA
 
Maneno haya ni ya Lunyungu aliwahi kuandika hapa na akapinga vikali JK kuwa Rais ilikuwa hatari kwa Nchi.


Lunyungu alitoa maneno haya aki refer kampeni za Temeke mwaka ule JK aliwa waziri wa Maji nk .Alienda Temeke ku kampeni dhidi ya Mrema ili Sisco awe Mbunge .JK akiwa Temeke mwisho saa kumi mchana alisema uongo akiwa jukwaani kwamba Word bank wamesha toa pesa za maji Temeke so wanatemeke mchagueni Sisco maji yamwagike maana pesa sasa ziko .
Kikwete aliamua kusema uongo kisa kura na akasahau kwamba alikuwa bado ni waziri aliyekula kiapo .

JK aliwa London ambako muda wote aliongozana an wahindi wa UK wanamchukulia Limosine toka London hadi London Gatwick wanafanay biashara ndani ya gari , kabla hajatoka alikutana na Lunyungu akamuuliza mkama maji tena yamesha kuja maana pesa zilisha tolewa .

JK akajibu ilikuwa siasa na ilikuwa kufanya vile watoto wake waweze kwenda ****** .

Lunyungu anasema baada ya kusikia JK ana nia na hatimaye kuchukua form kugombea Urais alitaka aende mahakamani kumpiga maana JK alisema uongo akiwa chini ya kiapo .Lakini kwa kuwa hakuna utawala bora na Majaji wa CCM wasingalikubali basi akanywea.Watanzania wakaingia katika ushabiki juu ya JK leo huyo watu wanalia .

Kwa jambo hili pekee JK si msafinna hakustahili Urais wa Tanzania .Wewe unasemaje ?
 
Pili, Rais alihusika katika kuzungumza na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kuwaomba wakubali sehemu ya pesa waliyopanga kuipa Tanzania kama msaada kutokana na mpango wa msamaha wa madeni itumike kugharamia ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Walikubali, na USD 225 milioni zilitumika kukodisha mitambo ya Kampuni za Aggreko, Alstom na Richmond (ambayo baadaye ikawa Dowans) na matumizi mengine ya dharura za umeme. Matumizi hayo mengine yalijumuisha pia ununuzi wa mitambo ya aina ya Watsilla ya kuzalisha megawati 100 za umeme pale Ubungo kwa kutumia gesi asilia. Mitambo hiyo imeshanunuliwa, kufungwa na tayari inazalisha umeme.

huyu mchumi wetu yani anakubali hiyo hela itumike kukodisha na sio kununua na kukodisha kwenyewe bei mbaya hivyo
lazima atakuwa na mshiko wake tuu
na kama aliiagiza timu yake iichunguze dowans kabla ya malipo na kuzuia $10m zisilipwe mwanzo, je timu yake ilimpelekea majibu gani ambayo yakamfanya aikubali dowans? au ulikuwa uwamuzi wake?? kama timu yake ilisema dowans ni safi then timu yake ni mbovu, je amewashughulikia??
 
Watanzania wenzangu!!!

Tukumbuke kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha... wale wanaoijua vizuri historia ya Siera Leone watakubaliana na mimi kwamba tusipokua makini, tutaangukia huko in less than 20 years, YES!!!

Sijui kwa nini tunashindwa kuyaona hayo na baadhi ya viongozi wetu nao wanaacha mambo mengine yaendelee!!!!

Tuombe mungu tupate viongozi wachache who can dare, na wote tuwe nyuma yao, hasa members wa JF

Ikibidi, tuvue haya ma-MTM, Kifimbo na majina kama hayo na kuvaa uhalisia wetu na kila mtu ajue tunasimama wapi

WE CAN STILL HELP OUR COUNTRY....

THANKS MMMKJ KWA KUENDELEZA MWENGE HALISI WA UHURU, NA SI ILE TOCHI INAYOTUMIA MAFUTA MENGI NA KUCHAFUA MAZINGIRA
 
Watanzania wenzangu!!!

Tukumbuke kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha... wale wanaoijua vizuri historia ya Siera Leone watakubaliana na mimi kwamba tusipokua makini, tutaangukia huko in less than 20 years, YES!!!

Sijui kwa nini tunashindwa kuyaona hayo na baadhi ya viongozi wetu nao wanaacha mambo mengine yaendelee!!!!

Tuombe mungu tupate viongozi wachache who can dare, na wote tuwe nyuma yao, hasa members wa JF

Ikibidi, tuvue haya ma-MTM, Kifimbo na majina kama hayo na kuvaa uhalisia wetu na kila mtu ajue tunasimama wapi

WE CAN STILL HELP OUR COUNTRY....

THANKS MMMKJ KWA KUENDELEZA MWENGE HALISI WA UHURU, NA SI ILE TOCHI INAYOTUMIA MAFUTA MENGI NA KUCHAFUA MAZINGIRA



Nakuunga mkono kwa mawazo yako haya .
 
Mimi nakubalia sana Mwanakiji.
Mweshimi yeye katika wale mabingwa wa usifadi anaongoza.Huyo iliyeleta mada ya Kikwete kafanya mema sijaona hata moja labda atwambie ana atupe evidence za atakayosema

sisi tunachojua ni bibwa wa kukusanya akisaidia na marafiki zake
 
Back
Top Bottom