Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Hatimaye Mwenyekiti wa CCM, DK Jakaya Kikwete amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kubadilisha maamuzi yake aliyotangaza Singida wakati wa maazimisho ya kuzaliwa kwa CCM kuwa ataachia nafasi hiyo ifikapo Juni 2016.
Kikwete ameyasema hayo Ijumaaa Mei 6 wakati alipozungumza na Watangazaji wa Clouds Media wakiwemo Masoud Kipanya na Baby Kabaye ambao walienda nyumbani kwake kufanya mazungumzo na mama Salma Kikwete.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Masoud Kipanya leo asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa hewani na Clouds FM, mara baada ya watangazaji hao kumaliza kuzunguza na Mama Salma, Kikwete aliungana nao wakati wa chakula. Kwamba, baada ya kusalimiana, Mheshimiwa Kikwete aliwauliza na nanukuu; "Mbona hamjamuuliza Mama Salma juu ya mimi kujiongezea muda wa kuongoza CCM tofauti na nilipotangaza hapo awali kuwa nitaachia nafasi hiyo ifikapo Juni 2016?" (wote wanacheka.......) mwisho wa kunukuu.
Baada ya Mheshimiwa Kikwete kuwatupia swali hilo na wote wakacheka kwa kufurahi, aliwadokeza kuwa hana mpango huo. Alisema kuwa hata kwenye nafasi ya Urais, wapo waliozua kuwa ana mpango wa kujiongezea muda wa kukaa madarakani. Kwamba, tofauti na awali ambapo kelele hizo zilipazwa na viongozi wa vyama vya upinzani, safari hii vyombo vya habari ndivyo vilivyochukua jukumu hilo. Mheshimiwa Kikwete anasema kuwa hajajua ni nini kimesababisha uwepo wa tuhuma hizo ambazo amesema kuwa hazina ukweli wowote.....Masoud, ikiwa sikuweza kung'ang'ania nafasi ya Urais, iweje sasa nifanye hivyo kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa CCM? aliuliza Kikwete.
Alisema kuwa CCM ina utaratibu mzuri wa kupokezana kijiti cha uenyekiti mara baada ya Rais mpya kupatikana kupitia CCM. Aliwakumbusha kuwa Mwalimu Nyerere alifanya hivyo kwa Mzee Mwinyi. Mzee Mwinyi akafanya hivyo kwa Mzee Mkapa. Mzee Mkapa akafanya hivyo kwake. Na sasa ni zamu yake kufanya hivyo kwa Rais Magufuli. Aliwakumbusha kauli yake ya awali kuwa ikiwa Magufuli atashinda Urais, atalala usingizi. Kwa vile Magufuli ndiye Rais, hana wasiwasi wowote juu yake na kwamba ifikapo Juni 2016, wale wote waliozua uongo juu yake wataaibika.
Mwisho wa uongo ni Aibu