Kikwete, Shein kazeni kamba kudhibiti utengano Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, Shein kazeni kamba kudhibiti utengano Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 12, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  WIKI 3 Zilizopita ilitawaliwa na vurugu zilizoibuka Zanzibar Mei 27, mwaka huu baada ya watu wanaodaiwa kuwa washirika wa Jumuia ya Mihadhara ya Kiislamu (Jamiki) kuchoma makanisa kisiwani Unguja kwa kisingizio cha kutaka Muungano uvunjwe.


  Vurugu hizo ambazo baadhi ya washiriki wa kikundi hicho walizitumia kutangaza kuwa watu wa Bara waondoke visiwani, ziliilazimisha Serikali kutumia nguvu kubwa kuwadhibiti na kisha viongozi wa juu wa serikali ya zote kutoa matamko ya kulaani vitendo hivyo.


  Rais wa SMZ, Dk Mohamed Shein aliweka bayana kuwa Serikali yake hatavumilia kuona baadhi wa watu wanatishia kuvunja muungano na kwamba watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.
  Si hivyo tu Dk Sheibn alipiga marufuku vikundi vya dini zote kuhubiri siasa kwenye mikusanyiko yao na kuvitaka vitangaze mambo ya dini zao.


  Pia alivitaka kutotumia mihadhara na mahubiri kukashifu dini nyingine na kusisitiza kuwa sasa vyombo vya dola vinafuatilia mwenendo wa mihadhara na mikusanyiko ya dini zote na kuongeza kuwa Serikali yake itawachukulia hatua wote watakaoibainika kuhatarisha amani na umoja wa kitaifa.


  Rais Jakaya Kikwete alipigilia msumari katika hotuba yake kwa taifa ya kila mwisho wa mwezi, aliyotoa Juni 2, mwaka huu kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1) akisema kuwa Muungano hauvunjwi kwa kuchoma makanisa na kuwalaani walifanya vitendo hivyo.


  Kikwete aliahidi kuwa Serikali yake haitakuwa tayari kuona Muungano unavunjwa wala kuona watu wanafanya vurugu kwa kutumia udini kuvuruga amani ya Tanzania iliyodumu kwa miaka mingi. Na alisisitiza kuwa hatakuwa tayari kuona hilo linatendeka katika enzi ya utawala wake.


  Katika mwendelezo wa kupinga vurugu hizo zilizojikitia katika hoja ya kuvunja Muungano, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa aliokemea machafuko hayo na kusisitiza kuwa amani ya nchi na umoja wa kitaifa lazima ulindwe kwa gharama yoyote.


  Wakati viongozi wa kitaifa wakiweka bayana msimamo wa Serikali zote mbili na kabla siku hazijaenda mbali, makundi pinzani ya kubaguana kimaeneo yameinuka baina ya Wapemba wa Waunguja ili kuthibitisha maneno aliyosema Mwalimu Julius Nyerere zaidi ya miaka 17 iliyopita kwamba; ‘dhambi ya ubaguzi kamwe haiwezi kuachwa, sawa na kula nyama ya watu. Muungano ukivunjika Waunguja na Wapemba watabaguana na kuendelea...’


  Hilo limedhihirika mwishoni mwa wiki iliyopita, kwani baada ya vurugu za kundi la Jamiki kutaka kuvunja muungano na kuwataka Watanzania Bara warudi kwao, kundi lingine linalojitambulisha kuwa la Watu wa Unguja lilisambaza kuwapinga wenzao wakidai kuwa washiriki wake wanatoka Pemba, wanataka kuharibu amani ya Unguja.


  Kibaya zaidi waliwaomba Rais Kikwete na Dk Shein wawaruhusu wanaotaka kuvunja muungano wapewe kisiwa chao cha Pemba kwa kuwa hapo nyuma walidai wapewe kiswa chao, ila viongozi wa serikali ndiyo waliong’ang’ania kuwa hawezi kuvunja umoja.


  Baadhi vipeperushi hivyo vilienda mbali kutangaza wazi ubaguzi kwa kusema watu wa Pemba asili yao ni Wamakonde kutoka Msumbiji ndiyo maana wanautukana Muungano na kwamba, Waunguja asili yao ni Wasegeju kutoka Tanzania Bara.


  Maneno hayo yanadhihirisha wazi kuwa tunakoelekea kubaya zaidi na ni dalili ya kutokea mgawanyiko mkubwa wa kitaifa, jambo ambalo ni hatari kwa wananchi masikini wasiokuwa na masilahi yoyote wakiwamo wanawake na watoto.


  Si hivyo tu, hoja hizo zinachochea utengano ambao unajenga uadui na hatimaye vurugu zinazoweza kusababisha vita vya kikabila au wenyewe kwa wenyewe ambayo ni hatari na si rahisi kuvizima.
  Kwa sababu hiyo tunawaomba viongozi wote wa kitaifa wakiongozwa na Rais Kikwete na Dk. Shein kuhakikisha kuwa Muungano unalindwa kwa nguvu na gharama zote kama walivyoahidi ili kuliokoa taifa kuingia katika machafuko.


  Ni kweli kwamba, wanaoendesha kampeni hizo hawana nia njema bali wanataka kutekeleza masilahi yao binafsi kwa kuwatumia Wapemba na Waunguja.


  Sisi tunaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali kulinda Muungano kwa manufaa ya Watanzania wote ( wa Bara na Zanzibar) na umoja wa kitaifa.
  Kikwete, Shein kazeni kamba kudhibiti utengano Zanzibar
   
Loading...