Kikwete, sasa umemwelewa Sumaye?

hahahaha hata hii uliondika sijui kama imeeleweka badili mbinu tusiamini eti wakirudia kusoma ndo wataelewa.
 
Natumaini kampeni tutafungia Jangwani, siku hiyo Sumaye ndiye atakae ongea mwanzo mwisho na kisha kwa dk chache sana EL atamalizia ya RICHMOND na kuipeleka rasmi CCM kuzimu kwa baba yake Lucifer.

Daaah,tukifungia Jangwani itakuwa raha sana maana ule ufunguzi tu ulikuwa burudani tupu.
 
Nawe ni mmojawapo? Mbona unakimbilia kutoa comment kabla hujasoma na kuelewa dhima ya mleta hoja? Siku ukiuelewa ujumbe huu, naamini hutokaa ushabikie usilolielewa na utakuwa umekombolewa kifikra nakushauri rudia kusoma tena na tena ili unufaike na dhima ya mleta hoja.
Kiukweli kiburi cha watawala walio wengi huwaangamiza wale wanaoongozwa. Laiti hawa viongozi wastaafu wangetumika kama think tankers nchi ingekuwa na siasa na uchumi bora kuliko nchi nyingi za Afrika. lakini kitendo cha kuwadharau kitaiangusha ccm ambayo ipo kifamilia zaidi.
Jiulize, familia za watawala zinataka kulinda himaya ipi au siri gani ccm? Na kama hakuna wanachokilinda, ile maana ya ccm kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi bado inafanyakazi? Kwanini hainekani kama ipo? Ukipata jibu utakuwa umemwelewa mtoa hoja.


Nashukuru umesaidia kuelewesha somo!!

Dalili za tawala nyingi kuanguka ni pale watawala wanapopigwa upofu wasielewe na kuona hali halisi mpaka pale wataposhindwa!!

Siamini JK aliposema wanaunganisha picha ni kwamba hakujua au alipigwa upofu?
 
Daaah,tukifungia Jangwani itakuwa raha sana maana ule ufunguzi tu ulikuwa burudani tupu.
Mkuu, pale ndipo tukapofanyia mazishi ya CCM, watanzania waliipenda CCM lakini Mungu kaipenda zaidi.
R.I.P CCM!
 
Wanachokifanya CCM ni siasa! Ikiwa huijui michezo ya siasa basi kuwa mpole ni busara kutoendelea kuhoji kwanini CCM wanamtajataja Sumaye?


Wewe ni wale wanaohitaji nguvu kubwa na muda wa ziada kuwafundisha waelewe...

Kwa sasa naendelea na walioelewa.... Panapo muda wa ziada NTAKUREJEA
 
Sumaye anaeleweka kwa wenye akili za kufikiria nje ya boksi! Hawezi kumwelewa,kwa nini,kwa sababu,kasoma uchumi chuo kikuu,bado haielewi kwa nini Tz ni maskini,Kawa rais kwa miaka 10 bado hajui kwa nini Tz ni maskini. Hawezi kumwelewa Sumaye
 
Sumaye anaeleweka kwa wenye akili za kufikiria nje ya boksi! Hawezi kumwelewa,kwa nini,kwa sababu,kasoma uchumi chuo kikuu,bado haielewi kwa nini Tz ni maskini,Kawa rais kwa miaka 10 bado hajui kwa nini Tz ni maskini. Hawezi kumwelewa Sumaye


Nakumbuka falme nyingi zilizoanguka zilishindwa kuelewa alama za nyakati...
 
Fastjet haelewagi
CCM ni shida. Hawana kitu vichwani. Mh.Rais hajui kwa nini watu wake maskini wakati kuna kila kitu. Ngumu sana kumuelewa graduate wa Harvard university.
Na mgombea wao naye kituko. Jamaa anapenda kuangalizia vya wenzake. Eti M4C kaifanya yake. Ph.D haitendei haki. Wanataaluma wa UDSM jaribuni kukaa tena,nina wasiwasi na JPM.
 
Nakumbuka timu yao ilipotangazwa mbwembwe zilikua nyingi...

Wakashindwa soma upepo na alama za nyakati...

Nasikia wengi wamechoka... wamekata tamaa kabla adui hajabadili mbinu za pambano...

CHANDIMU anaicheza na Maria sasa...

Na mbaya zaidi hicho Chandimu anakichezea pale Butiama kwa Chief Burito kabisa. Hivi ile Team ya Campaign tuliyotangaziwa kwa mbwe mbwe kabisa mbona siisikii kila siku namsikia Bulembo?
 
Na mbaya zaidi hicho Chandimu anakichezea pale Butiama kwa Chief Burito kabisa. Hivi ile Team ya Campaign tuliyotangaziwa kwa mbwe mbwe kabisa mbona siisikii kila siku namsikia Bulembo?


Wengi wamepoteza mvuto!!!

Awali walidhani wataweza kirahisi... ikawa hovyo mpaka wakamwingiza Slaa nayo imechuja...

Chandimu wanachezeshwa wenyewe.
 
Ndugu wana JF,

Nimelazimika kumwandikia rafiki yangu kipenzi JK waraka huu wa swali kwamba sasa amemwelewa Sumaye? Ktk makundi ya wanafunzi tunazo aina tatu yaani gold...silver...stone.

Gold huweza kuelewa bila msaada wa mwalimu na kwa haraka sana... Silver huelewa mara moja akifundishwa na mwalimu na hahitaji nguvu ya ziada ... Stone yeye hata akifundisha ni ngumu kuelewa na huhitaji mbinu kali zaidi aelewe ikibidi kwa kurudia rudia somo lkn hawa hawafiki mbali kielimu.

Nimeanza na utangulizi huo nikiikumbuka kauli ya rafiki yangu JK pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM aliposema amemsikiliza Sumaye hajamwelewa!! anasema mpaka siku hiyo anapokwenda uwanjani alikuwa hajamwelewa!!!!

Lakini ktk sokomoko hilo tumeshuhudia CCM ikibadili mbinu na sera... Bajeti ya kampeni ikiongezeka maradufu na hata kuwakumbatia wale JK aliowaita wanamiliki viwanda vya uongo ili tu kupunguza mvumo wa kauli na sumu za Sumaye majukwaani ndo nauliza sasa JK amemwelewa Sumaye?

Ndani ya vikao vya siri ajenda imekuwa Sumaye... ndugu yangu BM hana raha tangu Sumaye aondoke CCM...

Vilio na kutupiana lawama vimetawala ndani ya CCM juu ya kile Sumaye anafanya huko UKAWA!!!

Mafaili machafu dhidi yake yametafutwa yamekosekana!! hata hoja ya shamba halali la mvomero iliyoletwa na Makamba haijauza sasa wanaulizana ITAKUWAJE SUMAYE ANAYETUJUA SISI BINAFSI AKIAMUA KUFUNGUKA??

Siku anajitoa CCM Sumaye alisema huko CCM mmemuona ni sisimizi tu kiasi cha kuandika barua kutojibiwa hivyo wataona umuhimu wake akiwa Upinzani na ni dhahiri sasa anawatetemesha ndipo nauliza JK sasa umemwelewa Sumaye?

Nimeuliza kote walikopita wana UKAWA nimeambiwa watu wamekua na shauku kubwa mno yakumsikiliza bwana zero kuliko yeyote na amekuwa akitoa hamasa sana ....

Sumaye amejenga ujasiri sana kwa wapinzani na wapenda mabadiliko... ameondoa hofu na woga... amejenga kujiamini sasa vinaanza vitisho kuwa nchi haiendi upinzani!!!!

Nauliza tena JK uliyesema kwa dharau humwelewi Sumaye sasa umemwelewa au abadili mbinu za ufundishaji? umuulize na mdogo wako Makongoro ule mchezo wa CHANDIMU vipi mbona amechoka mapema??

Ahsante kwa kunisoma natumai umenielewa!!!

Ndimi LUSUNGO.

Baba mwanaAsha mpaka leo analalamika kuwa anaonewa

Hata issue ya Sumaye anaona kama conspiracy fulani hivi

but taratibu ameanza kuona light ndio maana kawa mpole sana siku hizu
 
Na hawa waliopo centre ya Masaki ndio wana ongoza kwa kumlisha JK matango pori, mala wamwambie picha za mafuriko zimeunganishwa na uwongo mwingi tu usio na tija.


Nasikia kuna siku waligoma posho ilichelewa...

Halafu ndo akili zile kweli zipambane na EL na UKAWA?
 
Baba mwanaAsha mpaka leo analalamika kuwa anaonewa

Hata issue ya Sumaye anaona kama conspiracy fulani hivi

but taratibu ameanza kuona light ndio maana kawa mpole sana siku hizu


Zile kauli za moto wa mabua sizisikii tena zaidi ya "hali ya uchaguzi ni ngumu"
 
85 Reactions
Reply
Back
Top Bottom