Kikwete rudi sasa

Dawson

Member
Mar 6, 2009
43
3
Kikwete na huku nako umefuata nini nasikia umekutana na mcheza Filamu wa Marekani Steven Seagal hivi kweli watanzania wanaitaji hili umepita kwenye makampuni ya computer IBM na google hivi unajua ni 2% ya watanzania wanaumeme ni kweli tunayaitaji haya kwa sasa baba nakusihi rudi rudi nyumbani watanzania tumechoka
 
Attachments

  • 5.JPG
    5.JPG
    18.9 KB · Views: 84
Huyu hata akirudi hana jipya atakalofanya. Kwasasa akija

ni mambo ya mbio za 2010 basi! No maendeleo kwa watu,

nothing!

Mwache akae huko huko akirudi akute SLAA ni Rais!

Mimi nadhani anataka kuwa selebrety wa holiwood naona ameenda kuomba application ndio maana anaongea na stiven segal.Watanzania sasa ni wakati wa kujutia uchaguzi tuliofanya kwa mapenzi yetu kumchagua JK mpenda umaarufu angalia anavyo tia haibu kilakukicha yuko kwenye ndege kama mtalii.
 
Huyu hata akirudi hana jipya atakalofanya. Kwasasa akija

ni mambo ya mbio za 2010 basi! No maendeleo kwa watu,

nothing!

Mwache akae huko huko akirudi akute SLAA ni Rais!

mh hii kali so tumwache akae huko hili akirudi akute Slaa rais
 
Mkuu bado hajamaliza kutalii anataka aonane na Anold sasa yule gavana.
Bado ana tanua si ziala ya kikazi siku 9.
 
Watanzania tutajuuuta kumfahamu! Huyu jamaa akiambiwa ni msanii anakasirika lakini anadhihirisha ule msemo usemao no matter how deep you bury the truth, it will manage to come out one day! sasa huyu ndie Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete mwenyewe, a.k.a mtoto wa mjini.

Nafikiri sasa watanzania tumejifunza, na tuanze sasa kujifunza kutoamini kila king'aacho ni dhahabu! Kula bata mzee na Steve, tafuta na wakali wengine upige nao picha tukuone, si unataka kushindana kwa usanii na kina Kanumba!
 
nasikia kikwete ana site Marekani anafatilia ujenzi that why kila leo yuko huko ndugu yangu Shein yeye kazi aliyopewa ni kufunga na kufungua ndio maana utasikia leo kafungua daraja mara kafunga semina ya madiwani. mh wadanganyika kazi tunayo
 
Hii lakini jamani ni noma sana. Hivi huyu ndio rais wa nchi masikini kabisa duniani anatumia pesa zetu kwenda kukutana na steve seagal???. Hivi watanzania tumerogwa au maana mimi sielewi. Viongozi wa nchi tajiri hawafanyi haya anayofanya huyu jamaa. Pole yetu kubwa wabongo.
 
Nadhani Dr Shein anakazi kubwa sana binafsi nisingaliiweza, mshindikiza na kumpokea kila siku Mkwere pale JNIA! Naona Sasa anajiandaa kwenda mpokea akirudi na kuambiwa aaah ziara ilikuwa ya mafanikio sana ...nimeona google inavyofanya kazi, nimekutana na Steven Seagal, Obama, Michele, Hilary C na masuper star wa Holywood. Nimewaomba waje watusaidie kuanzisha Tanzawood yetu...akina Kanumba si wapo? Maisha bora kwa kila fisadi!
 
Kikwete na huku nako umefuata nini nasikia umekutana na mcheza Filamu wa Marekani Steven Seagal hivi kweli watanzania wanaitaji hili umepita kwenye makampuni ya computer IBM na google hivi unajua ni 2% ya watanzania wanaumeme ni kweli tunayaitaji haya kwa sasa baba nakusihi rudi rudi nyumbani watanzania tumechoka

Huyu hata akirudi hana jipya atakalofanya. Kwasasa akija

ni mambo ya mbio za 2010 basi! No maendeleo kwa watu,

nothing!

Mwache akae huko huko akirudi akute SLAA ni Rais!

Mnaota ndoto za mchana. Slaa raisi!!!!?Mwacheni atafute channel za kujienga Tanzania maana bado ana miaka 5 na lazima anapata hili lipo wazi kama u*** wa mbuzi. Hivi hamjiulizi kwanini awepo Shein pale alipo na Pinda. Da washikaji JK mnataka awaalete chakula nyumbani maana kusema kwamba hakuna maendeleo kwa watu nakuwa sielewi. hheee.. aaahhh. wananchi kweli tumechoka yaani JK atusaidie hata kulisha familia zetu wakati sisi kutwa tunashinda maskani (Ni mawazo tuu)
 
Kikwete na huku nako umefuata nini nasikia umekutana na mcheza Filamu wa Marekani Steven Seagal hivi kweli watanzania wanaitaji hili umepita kwenye makampuni ya computer IBM na google hivi unajua ni 2% ya watanzania wanaumeme ni kweli tunayaitaji haya kwa sasa baba nakusihi rudi rudi nyumbani watanzania tumechoka

Dawson, kwa takwimu za sasa ni kuwa angalau 10 % ya Watanzania wana umeme.

Infact wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005 naweza kusema kusema kulikuwa na matabaka makuu mawili. La kwanza ni la wale waliokuwa wanachagua chama (CCM) kwa hofu kuwa vyama vya upinzani vilikuwa havijakomaa kupewa nchi japo wengi walijua kuwa Kikwete was a "playboy" mtu aliyekuwa mpenzi sana wa kwenda kujirusha viwanja ikiwemo Bilicanas na kupenda sana "vimwana". Kwahiyo mtu usingetegemea atoke mtu wa maana humo kuongoza nchi. Kundi la pili ambalo wengi wao walikuwa ni vijana walimwona Kikwete kama mwenzao anayeweza kuwaletea maendeleo kutokana na kujichnganya nao hasa huko kwenye kumbi za starehe. Cha ajabu leo mwenzao kaiacha nchi mikononi mwa fisadi papa RA ingawa anaona kabisa mambo yanakwenda ndivyo sivyo. Dawa i mikononi mwetu watanzania wenzangu katika uchaguzi mkuu 2010.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom