Ni ajabu, aibu, na kukosa uelewa kwa mtu anayesadikika kuwa na digrii ya uchumi (UDSM) (ambayo si amini kama aliwahi kupata) Kukubali kupewa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akijua ameshindwa katika uchaguzi. Leo hii Tume yake ya Uchaguzi imemtangaza kuwa raisi lakini akiwa HANA WATU WA KUWAONGOZA. Katika mjii huu wa Arusha kumepoa na watu wanaendelea na kazi zao kama vile kuna msiba uliotokea. Sijui kesho Tanzania itaamkaje na msiba huu laiti kama tungeanza kulia. Ushindi huu wa CCM ikulu ndio mwanzo wa misiba mingi kwa miaka mitano ijayo-Bora Arusha wameanza kujizoesha. LAKINI KAMA HATUTAKI MISIBA NA TAABU TUFANYE JAMBO WATANZANIA HATA KAMA NI GUMU