Kikwete Rais bora Tanzania kuzidi waliomtangulia

Kila mtu ana ubora wake na mara nyingi kuna neno moja linaloweza ku sum up ubora wa huyo mlengwa.

Kwa J.K naweza kusema ni rais bora kuliko waliomtangulia kwa "UDHAIFU". Hapo nampa 199%.
 
Sory bro nlishaanza kuku tukana kwa kukurupuka kisoma heading ya thread...ila nilivyozama nikagundua wewe great thnker ulichosoma nakikubari kabisa
 
wanajamvi nawasalimu:

Nimewaza mda mrefu nikaona niweke slide hii maana nimeona ipo sawa kuifikiria sisi kama great thinkers:

Kikwete ni Raisi bora kuliko wote waliomtangulia hapa tanzania kwa sababu zifuatazo ( upo free kuongeza )

1. Amepanua democrasia kwa kiasi kikubwa hadi sasa hadi kijijini wanaujua ubaya na udhaifu wa serikari yetu.
2. kila chombo cha habari chaweza kuandika tuhuma hata kama ya jinai inayoihusu serikari pasipo kuchukuliwa hatua
3. amewafanya watu kuipenda sana CDM kuliko CCM hata waliomo CCM wanapenda kuwa katika chama Makini CDM lakin ndo hivo matumbo yao bado yana njaa.
4. asilimia 80 ya Raia wa Tanzania wanachukizwa na utawala wake ila wengine hawana jinsi wanaogopa kutema Vibarua

Kwa kuwa Kikwete alikuta System ikiwa vile lakin wananchi hawaelewi hivo akaona hawez nyamaza wakati wananchi wanaumia kwa mda wote, niyafanye haya yote, nioneshe kuwa mie ni dhaifu sana ili watu waanze kugundua na kujua nini kilichokuwa kinafanyika Ikulu ya Tanzania miaka ya nyuma.
Kwa Point hizo nahis Kikwete ni Raisi Bora Kuwazidi akina Mkapa, Mwinyi na Nyerere.

Kikwete ndio rais aliyelizamisha taifa hili pahali pabaya zaidi, na tutamkumbuka kwa ubaya zaidi mifano ipo mingi sana,

1. Mchakato wa Katiba ambao ndio roho ya nchi yetu hata kwa wasiokuwa na vyama alivyoweza kushawishiwa na akashawishika bila kujiamini na hatua uliofikia.

2. Mauwaji mangapi yametokezea kizembe akiwa yeye ni rais na bado yanaendelea.
3. Ubaguzi alivyoweza kuwagawa watanzania kwa dini zao na makabila kwa mfano lukuvi alienda makanisani kusema Zanzibar wasipewe mamlaka yao mana ni waislam wataanzisha dola ya kiislam Zanzibar akiwa pia kauli zilizotolewa na jaji Warema Bungeni juzi kuhusu kuwabagua wazanzibar wazi wazi mchan kweupe na yeye anaona anasikia anaambiwa bila ya kuchukua hatua wala kukemea hatua hizo za mawaziri wake ambao yeye ndio amewapa mamlaka.
4. Rais kikwete toka amekuwa rais wa JMT maendeleo ya nchi Tz imekuwa ni ndoto, maisha magumu, hamna ajira, wizi, rushwa, ufisadi umeongezeka maradufu,nk

Jk hawezi kuwa kiongozi bora na hatakuwa kiongozi bora, Kisheria ni wa kupelekwa the heag akimaliza mda wake
 
1. kwa kuuza wale twiga na wale wanyama wengine, kweli raisi bora, maana sidhani kama kuna aliyewahi fanya hayo

2. Mwenye deni kubwa la taifa kuliko maraisi waliotangulia

3. Mwenye safai nyingi kuliko waliomtangulia
 
Ni kweli naunga Mkono hoja maana jamA kakopa 7 Tril ndani ya Mwaka mmoja, wanasema ni za kufidia Bajeti, lakini ukweli ni kuwa hela iliyopatikana huko mawizarani haifiki hata 50%. Je amepeleka wapi hizi hela?
 
Angempongeza Mwinyi kwa kufungua milango miaka ya 1991, 92 au 93 kama sijakosea ningemwelewa,

Naona wakuu mmeshindwa kumwelewa huyu mleta Mada, hapo ndo u-great thinker unavyotupiga chenga! Jamaa kasema kabisa Kikwete ni bora kuliko wengine kwa udhaifu wake! Someni katikati ya mistari labda mtamwelewa!

Kuhusu mageuzi ni Nyerere ndiye aliyeyapigia debe, vinginevyo Mwinyi asingeweza! Enzi za Mzee Ruksa bado Nyerere alikuwa anaongoza indirectly na ndiye aliykuwa anampa maelekezo nini cha kufanya!
 
Nampongeza kwa kujitengea bilioni 50 za kuvinjari ughaibuni,raha jipe mwenyewe bwana!vijana endeleeni kugombania viajira vya uhamiaji yaani kwa uwiano wa vijana 10 kwa nafasi 0.7 za ajira.
 
Nimejaribu kutafari sana nikagundua kuwa Kikwete ndiyo rais bora. Amepanua wigo wa democrasia na pia amejenga miundo mbinu Umeme, barabara, majumba marefu na makubwa.Shule nyingi na vyoo vikuu.

Hata kwenye chama chake hatompendelea mMTU katika uteuzi. Anayetegemea nguvu na ushawishi Wa Mkt. asahau. Mkt. ni mpenda haki na hili mtukuja kulingundua badaaye.

Akistaafu uongozi mtatamani aje angombee urais tena.
 
Hata uchumi umekua sasa dolla 1930 na alichukua nchi ikiwa1300 sukari ilikuwa 600 sasa 2000 kweli tutamkumbuka.
 
Ametusaidia kwa kweli mana angekuwa na roho mbaya magereza yote yangejaa mafisadi walioshika chati katika kipindi chake na pia tungepoteza ndugu zetu wanaoua albino mana angesign wanyongwe
 
Nimejaribu kutafari sana nikagundua kuwa Kikwete ndiyo rais bora. Amepanua wigo wa democrasia na pia amejenga miundo mbinu Umeme, barabara, majumba marefu na makubwa.Shule nyingi na vyoo vikuu.

Hata kwenye chama chake hatompendelea mMTU katika uteuzi. Anayetegemea nguvu na ushawishi Wa Mkt. asahau. Mkt. ni mpenda haki na hili mtukuja kulingundua badaaye.

Akistaafu uongozi mtatamani aje angombee urais tena.
menina
 
amesafiri duniani kuliko raisi yeyote duniani. kwa hili tu namuona si raisi bora tz wala afrika tu, ni raisi bora duniani
 
Sasa unaogopa nini kusema kuwa Kikwete ni dhaifu na mlegevu kuliko marais waliomtangulia...Yaani hata Mwinyi anamzidi huyu jamaa yako!!
 
Binafsi nampa credit kwenye Mambo kadhaa
1.Kupambana na Rushwa na Ufisadi
2.Kuboresha elimu ambapo kwa sasa viwango vya ufaulu vimeboreshwa kwa elim ya msingi na sekondari
3.Kupambana na ujangili,ndani ya utawala wake idadi ya tembo imeongezeka
4.Kuwa na timu ya mawaziri wachapa kazi ambao si mizigo,mfano Kawambwa,Maghembe,Nyalandu,Mkuya
5.Anapambana na madawa ya Kulevya kwa juhudi zote,mpaka sasa ameifanyia kazi orodha ya wauza unga
6.Amebana matumizi ya serikali kwa kiwango kikubwa hasaa ambapo kwa sasa idadi ya mashangingi imepungua serikalini
7.Ujambazi umeondoka kabisa,kwa sasa waweza tembea na mil 50 kwenye rambo na watu wakaziona na wasikupore.
8.Ongezeni
 
Miaka kumi ya JK imetumika kuifanyia Tanzania Audit iliyokuwa long overdue tangia siasa za ujamaa zi-fail, tangia mwalimu alipoondaka na value alizoziacha zipo wapi, mfumo gani mbele wa maendeleo unatufaa, kwa taratibu zipi, bado tunataka kuweka nguvu nyingi sehemu moja kwenye usimamiaji wa wafanyakazi wa umma kama mwalimu alivyokuwa anafanya; yeye alikuwa na sababu zake sisi bado tunasababu za kuendelea nazo leo kwa jinsi mambo yalivyo.

In short JK kaifumua Tanzania mpaka uvunguni kwa kujua au kutokujua lakini kwa sasa hakuna longo longo tena matatizo yetu ni dhahiri choice yetu ya raisi ajaye ndio zitaamua tuna taka kwenda mbili vipi kuendelea na siasa hizi hizi au tunataka mtu anaesafisha kwanza system na kuipanga upya JK kaacha hizo mechanism how do we utilise hizo system tena habari zingine.

Nampa B+ kwa sababu mengi aliyoyataka watanzania wayaone wameyaona hila kashindwa kuchukua hatua stahiki sana sana kwa watendaji wa serikari.
 
Back
Top Bottom