Kikwete nje ya nchi na watu kumi na sita 16 ati wanaita ujumbe.....!!

Picha unazoziona zimepigwa na wapiga picha wake, haiwezekani asiende na wataalamu wa masuala yaliyompeleka, nafikiri unamuamini sana Zito kuwa ana mawZo mazuri sana, lakini alikubali kuongozana na mkuu wa nchi badala ya kubaki ili asilipwe posho, tena ameleta picha kapiga na spika mstaafu, nafikiri ungetumia asilimia mbili tu ya akili yako usingelalamika idadi ya watu 16, siku chache zilizopita walinzi 11 wa obama walirudishwa, naongelea 11,
 
Huyu Rais mtalii yuko safarini na watu kumi na sita 16,sasa la kujiuliza ni kwamba hawa watu wote wanaenda kufanya nini na wote hawa lazima walipwe so hapa si ndo kule kutafuna Taifa au tuseme wanatafuna chapaa za walipa kodi.Hivi huyu jamaa anaitakia nini nchi hii maake its too much kwa nini asiende na watu hata 3 ukiongeza mabodigadi,Dr na mke wake?
Poleni sana kwa wale wote walioshiriki kumpa kula badala ya kura wakati ulee wa uchaguzi na kuchakachua matokeo,poleni sana kwa maisha magumu na bidhaa feki hiki ndo kipindi chenu Watanganyika na bado miaka 3 safi kabisa mtakula nyasi

Tatizo lako ni ufinyu wa mawazo, ikiwa Slaa tu sio Rais na anasafiri na Josephine, Hausigeli na bebi boi na mlinzi na dereva. Wangapi hao? ukipata jibu jiulize Rais kwenda na watu 16 ni wengi? kama unawaona ni wengi nadhani hujui maana ya Rais.

Kwa kuongezea tu, safari hii ni mwaliko wa G8, ujuwe wana cover costs zote.
 
jk anadhani anawaongoza watz kweli?mi ninavyojua mpaka sasa hv ni muhudumu wa chai kwenye ndege,maana hizo trip too much!,Vasco dagama ilizunguka kwasababu ambazo hv leo zimemfanya awekwe kwenye historia ya kimataifa na pia alizunguka kwa faida sio hasara km huyo jk
 
Msafara wa Raisi unatakiwa na Doctor 1, walinzi 2, mpiga picha 1, Waandishi wa habari 2, mpiga pasi 1, Maofisa wa usalama wa taifa 2, mwandika hotuba 1, washauri wa Raisi 2, mpishi 1, watu wa protokali 2 na first lady.
Hivyo kuwa na watu 16 ni sawa kabisa na kwa kweli Mh Raisi ameweza kusikia kilio cha watanzania kwa kupunguza idadi ya watu katika misafara yake.

mperndwa,

nakubaliana na wewe mia kwa mia!!,

kwa anayejua "msafara wa rais" maana yake nini, atakuwa amekuelewa. mimi baba yangu alikuwa DC, msafara wake siku zote ulikuwa na idadi sawa na watu hao, so kama kweli rais kasafiri na watu hao tu, anahitaji kupongezwa sana kwa kulionea huruma taifa letu!!

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
 
Mwacheni jamani nchi yetu kubwa sana............kikwete anajitahidi kuhakikisha kila mkoa unakuwa na muwakilishi angalau mmoja kw\ hiyo ana nia njema kabisa tatizo letu watz wabishi sn.......nchi hii kubwa sana ...nyie mnataka aende ziarani na watu watano km afanyavyo w/mkuu wa uingereza wkt mnajua kbisa uingereza ni kanchi kadogo kabisa ukikompea na linchi letu?.....mambo ya nchi masikini sijui nini na nini mtajitu wenyewe...lakini rais anaangalia maslahi ya watz wote kwa kujitahidi kila mkoa unakuwa na mwakilishi......
Mwacheni rais wetu...hata hivyo bado miaka mitatu tu kwani kuna shida gani si ataondoka?....akiondoka atakuja yule wa kuondoka na shangazi na wajomba wake wote mtasemaje?....

nakubaliana na wewE mia kwa mia.

mie natoka familia ya kisiasa, katika misafari kama hiyo kuna kitu kinaitwa "regional balance" kitu hiki kipo pia katika uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri na hata wakuu wa mikoa na wilaya. ukikijua vizuri, utamujelewa rais wetu.

narudia TENA KAMA NILIVYOSEMA KABLA, KAMA KWELI RAIS KASAFIRI NA WATU 16 TU, BASI ANATAKIWA KUPONGEZWA SANA KWA UJASIRI WAKE NA UZALENDO WAKE KWA KULIONEA HURUMA TAIFA LEYU

MBARIKIWE SANA WAPENDWA,

GLORY TO GOD!
 
Kwa ushindi wa Chelsea atapita Uk kumpongeza Drogba kwa ushindi na kumwalika Tz aje kuona watakavyoshirkiana na Tenga kuinua soka la Tanzania. Si unajua Beckam yupo njiani? lol!
 
Jk kanyaga twende,Hata Mwl Nyerere msafara wake ulizid watu 16! Tunakuelewa,tunakuthamini,tunakuheshim na tunakupenda,Bila ya kuwadhibiti yale majambaz ya mabenk leo hii wasingekuwa wanakuponda!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom