Kikwete: Nilianza kilimo miaka mingi sana, changamoto kubwa ya kilimo cha mananasi ni hii

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
JK.jpg
By Sanjito Msafiri

Pwani. Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.

Akizungumza leo Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.

"Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu," amesema.

Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.

"Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,"amesema.

Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.

Chanzo: Mwananchi

n.jpg
n1.jpg
 
Natamani kukupongeza Prof JK lakini BRN uliyotuachia tunayashuhudia huko huko Pwani hasa Mkuranga - Kibiti - Ikwiriri
 
Kuna mama naona kavaa yellow tshirt daaah Cowbell vibaya sanaaaaa
 
Mkulima wa Tanzania ameanza kulima tangu nchi inapata uhuru, ila sijui kwa nini mkulima hajawahi kutajirika mpaka leo...
Ninachoamini, ukitaka kutajirika usiingie kwenye kilimo. 80% ya watanzania waliotoka kappa kwenye kilimo, sio wajinga...
 
Niseme tuu nampongeza Mh Jk. Lakini kwa level aliyo kuwa amefika sio wa kulima kwa kutegemea mvua. Pili, washauri wake huenda hawampi ushauri sahihi kwenye kilimo. Ni aibu kupalilia ekari 200kwa mkono. Haita mlipa. Anahitaji kupata wataalamu sahihi wa kilimo.
Kuhusu umwagiliaji hata mimi niko tayari kumshauri Mh Kikwete.
 
Mzee J.K alipata kuwa ktk nafasi kubwa ktk nchi hii, na kama yy alivyosema alianza kulima miaka mingi sana, cjui alipigania vp bei za mazao, wkt wa utawala wake ili wakulima wanufaike ikiwemo na yy, badala ya kusema changamoto soko au yy aliuza mazao yake nje ya nchi kwa kuwa uwezo alikuwa nao/anao!
 
Hayo anayosema alikuwa na nafasi nzuri kuyakamilisha/ kuyafanya alipokuwa rais, kwa sasa sijui, hao wakulima wenzake wasubiri, pengine yatatokea.
 
My take, huyu jamaa ni mfano wa kuigwa
naona kama anatoa malalamiko, kama nionavyo ndivyo basi ni aibu kubwa kwa mlalamikaji kwani hata asipolima alipsswa aoneshe nini alifanya na nini wengine wafanye ili kilimo kiwe na maana
 
By Sanjito Msafiri

Pwani. Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.

Akizungumza leo Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.

"Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu," amesema.

Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.

"Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,"amesema.

Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.

Chanzo: Mwananchi

Hayo ni maneno ya Raisi wa nchi aliyeongoza kwa miaka 10 tena nchi ambayo Raisi ana karibia absolute power, sasa swali kwa nini hakutumia Uraisi wake kubadilisha/kuboresha hiyo hali ili Wakulima wanufaike? Kama hata yeye pia analalamika, sasa sisi wengine tufanye nini?
 
atunda pale Bagamoyo. Tatizo lake anaona kasalitiwa kwenye Sera ya ke ya kilimo kwanza na BIG RESULTS NOW(BRN). Bora tungeenda na Matokeo makubwa sasa kama tulikuwa hatuna dhamira ya dhati ya Viwanda
nimegoogle hizo sera mbili nimeambulia patupu, labda zilikuwa pantoni za kuvuashia magendo kwenda green party, i stand to be corrected
 
Hayo ni maneno ya Raisi wa nchi aliyeongoza kwa miaka 10 tena nchi ambayo Raisi ana karibia absolute power, sasa swali kwa nini hakutumia Uraisi wake kubadilisha/kuboresha hiyo hali ili Wakulima wanufaike? Kama hata yeye pia analalamika, sasa sisi wengine tufanye nini?

Hapo ndio huwa namshangaa Magu anasema watu wakalime wakati rais mstaafu mwenyewe analalamika kuhusu kilimo. Kibaya zaidi wanaoutunga sera hawalimi bali wanakaa ofisini tu. Leo JK analialia wakati hata harufu yake haijaisha ikulu na kuwa ndio mtoa dira mkuu wa kilimo. Ukiangalia signature yangu hapo chini ndio utajua nini naongea kuhusu kilimo.
 
Back
Top Bottom