Kikwete ni zawadi ya krismasi kwa wapinzani

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Kikwete anaimaliza CCM, je wapinzani mko tayari kuchukua nchi?

Kwa wale ambao mnafuatilia siasa za Marekani mtakumbuka mwishoni mwa miaka ya tisini jinsi Joji Kichaka alivyojihusisha sana na mambo ya conservative christians kwa kujifanya kuwa ni mwenzao na mtu aliyezaliwa upya (a born again christian).

Watu wengi bila kujua wakamuamini Kichaka na hata kufikia nafasi ya kusema kuwa Kichaka ameteuliwa na mungu kuwa rais wa marekani (maneno ya Pat Robertson). Demokrats kama kawaida yao wakalialia na kupiga makelele kuwa dini inaunganishwa na siasa bila kujua kuwa kitendo cha Kichaka kujiita mkristo safi kilikuwa ni zawadi kubwa sana ambayo wangeifaidi kwa miaka mingi ya baadaye.

Miaka saba baada ya Kichaka kuchaguliwa kuwa rais amewathibitishia wamarekani kuwa yeye sio mkristo wa kweli kama alivyodai mwaka 2000 bali yeye ni mwongo, mwonevu, katili, asiye na utu, mchoyo, mwizi, na maovu mengine yote. Hii sio tu kuwa imevunja nguvu ya ushawishi ya christian conservatives katika siasa za marekani, bali pia imewafanya wengi wao kuwapuuzia wale wote wanaojiita wamezaliwa upya na kutowachukua on face value (no wonder Giulian anafanya vizuri kwenye polls).

Miongoni mwa marafiki wakubwa wa Kichaka barani afrika ni ndugu yetu mtiifu Kikwete AKA Mkwere AKA Vasco Da Gama. Yeye naye kama rafiki yake Kichaka alivyofanya Marekani, aliupata urais kwa kuwa na propaganda machine kubwa, kuwateka watanzania kwa kuvaa ngozi ya kondoo huku pia akitumia mbinu za mbwa mwitu, kutumia waumini na viongozi wa dini na watabiri, kutumia kwa siri mapesa ya nchi, nakadhalika na kufanikiwa kushinda kwa "kishindo".

Miaka michache tu ya uraisi, the guy amethibitisha kuwa si yule handsome boy au mr nice kama vile viongozi wa dini walimsifia wakati wa kampeni. Miaka michache tu ya urais, Vasco Da Gama anatumia mabilioni ya nchi kusafiri nje ya nchi kwa safari ambazo hazieleweki, miaka michache tu Kikwete anaigawa CCM kwa kuwakumbatia mafisadi marafiki zake huku akiuza nchi kila leo.

Kikwete anaigawa CCM so fast kuliko hata alivyofanya Mwinyi na Mkapa. Wanaccm wengi wamegundua kuwa huyu ni Raisi aliyewarubuni ili awe rais kujitajilisha yeye na rafiki zake wachache wa ndani na nje (kina Sinclair). Ingawa Kikwete alichaguliwa kwa "kura nyingi" , miaka inavyokwenda inathibitisha Kikwete ndiye anaweza kuwa mtu ambaye watu wengi wamekuwa wanasubiria miaka yote hii ili aivunjevunje ccm kutokea ndani.

Kama Kichaka alivyovunjavunja nguvu ya Republicans hapa US kwa sasa, Kikwete naye anavunjavunja nguvu na mshikamano wa ccm huko Tanzania kwa kasi kubwa ya ajabu. Kikwete ni zawadi ya krismas ya mwaka 2007 kwa wapinzani Tanzania. Swali la kujiuliza sasa ni kuwa, je wapinzani wako tayari kupokea zawadi hii toka kwa Mkwere ooopps Vasco Da Gama oops Kikwete na kufungua hilo box?
 
Na bado nashikilia msimamo wangu kuwa habari zinazovuja kuwa Kikwete hatagombea tena mwaka 2010 zina ukweli kwa asilimia kubwa sana.

Swali ni kuwa, je hata hiyo 2010 atafika? au akimaliza kuuza nchi atakimbilia ulaya au marekani kujificha?
 
Hamjasoma alama za Nyakati kaaamua anataka aweke Historia awe Rais wa kwanza kutawala Miaka 5, kasha kata tamaa alichamua kufanya sasa ni kuchukua kila kinachowezekana then anakabidhi chama chao na nchi yenu yeye kama Balali anishia huko Ukwereni
 
nakiri ukweli kuwa kikwete hayuko tayari kugombea tena 2010 kama tutamkomalia ila anajaribu kuangalia upepo unavyokwenda upinzani waanze kukomaa na ile list ya mafisadi ili wananchi tupate majibu yao CCM itapasuka sasa hivi kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2009 hivi kweli yule aliyetukana wanawake kuwa wana wivu yeye kuwa mwenyekiti wa vodacom leo anaweza kunyanyuka na kujidai anaweza CCM? uongoooooo
 
Hapo naona mnajiridhisha tu juu ya hili la JK kutokugombea tena 2010.

Ukweli ni kwamba hataondoka hapo mpaka labda kwa kutolewa kwa kura za wananchi.

Tumwondoe kwa kutumia ubora wa upinzani lakini hili ka kufikiri atajiuzulu naona ni kama ile tamaa ya fisi kudhani mkono utadondoka.
 
Unachosema ni kweli kabisa Mtanzania. Inabidi nguvu zielekezwe kwenye kumtoa kwa kura au walio ccm waseme kuwa n-uff is n-uff!

Ila pia kuna habari zina-leak kuwa Vasco Da Gama ataachia ngazi mambo yakienda mrama na sio vibaya hizi nazo zikawekwa wazi ili watu wasijekukutwa hawajajiandaa na Mwamunyange akachukua nchi.
 
Jinsi nisivo na hamu na huu utawala wa kishikaji, natamani mwamunyange afanye kweli hata leo, ila tu kama yuko tayali kuwaondoa wezi wa raslimali zetu, na kuwashika mashati woooote walio chota warudishe mapema kilicho chetu!

Hata hivo, hivi kweli wana JF wote tulio na mapenzi na nchi yetu kweli, hatuwezi anzisha kampeini ya nguvu kwa kuwaelewesha ndugu zetu walioko kila kona ya tanzania, kwamba hii imetosha CCM walipo tufikisha yatosha, then hiyo 2010 tukaweka historia?? walau kukata mzizi wa mwenzetu, muache apumzike, ushikaji n.k?

Naamini inawezekana jama, hebu tuwe serious!
 
Hizo fikra nzenu ni ndoto kweli. Wajinga wakubwa nyie. Mmeondoka TZ siku nyingi mnajifanya mnaelewa. Aagh!!!!
 
Unachosema ni kweli kabisa Mtanzania. Inabidi nguvu zielekezwe kwenye kumtoa kwa kura au walio ccm waseme kuwa n-uff is n-uff!

Ila pia kuna habari zina-leak kuwa Vasco Da Gama ataachia ngazi mambo yakienda mrama na sio vibaya hizi nazo zikawekwa wazi ili watu wasijekukutwa hawajajiandaa na Mwamunyange akachukua nchi.

Sasa hapo ile habari ya kupokezana vijiti ndio itakuwa imetimia hasa.

You know what, Richmonduli anachukua njiti. Sijui tutasemaje tena! Usisahau, wakipendacho CCM, ndio hicho tukipatacho; usije ukajidanganya vinginevyo.
 
Interesting! Inakuwa kama makubaliano ya Tonny Blair na Gordon Brown ya kupokezana vijiti
 
our fellow member John Mnyika naye sasa yupo TVT mnaweza kumwangalia
 
Hizo fikra nzenu ni ndoto kweli. Wajinga wakubwa nyie. Mmeondoka TZ siku nyingi mnajifanya mnaelewa. Aagh!!!!

Polepole ndugu, kama huna hoja soma tu utulie, sio lazima uchangie. Enzi ya kujibu hoja kwa matusi tulishaipita siku nyingi. Kutukana ni kielelezo cha wazi cha unyonge na u-primitive wa mtu, nawe kwa maandisha yako haya umethibitisha jinsi ambavyo ustaraabu bado mnapishana. Pole sana.
 
Kikwete anaimaliza CCM, je wapinzani mko tayari kuchukua nchi?

Kwa wale ambao mnafuatilia siasa za Marekani mtakumbuka mwishoni mwa miaka ya tisini jinsi Joji Kichaka alivyojihusisha sana na mambo ya conservative christians kwa kujifanya kuwa ni mwenzao na mtu aliyezaliwa upya (a born again christian).

Watu wengi bila kujua wakamuamini Kichaka na hata kufikia nafasi ya kusema kuwa Kichaka ameteuliwa na mungu kuwa rais wa marekani (maneno ya Pat Robertson). Demokrats kama kawaida yao wakalialia na kupiga makelele kuwa dini inaunganishwa na siasa bila kujua kuwa kitendo cha Kichaka kujiita mkristo safi kilikuwa ni zawadi kubwa sana ambayo wangeifaidi kwa miaka mingi ya baadaye.

Miaka saba baada ya Kichaka kuchaguliwa kuwa rais amewathibitishia wamarekani kuwa yeye sio mkristo wa kweli kama alivyodai mwaka 2000 bali yeye ni mwongo, mwonevu, katili, asiye na utu, mchoyo, mwizi, na maovu mengine yote. Hii sio tu kuwa imevunja nguvu ya ushawishi ya christian conservatives katika siasa za marekani, bali pia imewafanya wengi wao kuwapuuzia wale wote wanaojiita wamezaliwa upya na kutowachukua on face value (no wonder Giulian anafanya vizuri kwenye polls).

Miongoni mwa marafiki wakubwa wa Kichaka barani afrika ni ndugu yetu mtiifu Kikwete AKA Mkwere AKA Vasco Da Gama. Yeye naye kama rafiki yake Kichaka alivyofanya Marekani, aliupata urais kwa kuwa na propaganda machine kubwa, kuwateka watanzania kwa kuvaa ngozi ya kondoo huku pia akitumia mbinu za mbwa mwitu, kutumia waumini na viongozi wa dini na watabiri, kutumia kwa siri mapesa ya nchi, nakadhalika na kufanikiwa kushinda kwa "kishindo".

Miaka michache tu ya uraisi, the guy amethibitisha kuwa si yule handsome boy au mr nice kama vile viongozi wa dini walimsifia wakati wa kampeni. Miaka michache tu ya urais, Vasco Da Gama anatumia mabilioni ya nchi kusafiri nje ya nchi kwa safari ambazo hazieleweki, miaka michache tu Kikwete anaigawa CCM kwa kuwakumbatia mafisadi marafiki zake huku akiuza nchi kila leo.

Kikwete anaigawa CCM so fast kuliko hata alivyofanya Mwinyi na Mkapa. Wanaccm wengi wamegundua kuwa huyu ni Raisi aliyewarubuni ili awe rais kujitajilisha yeye na rafiki zake wachache wa ndani na nje (kina Sinclair). Ingawa Kikwete alichaguliwa kwa "kura nyingi" , miaka inavyokwenda inathibitisha Kikwete ndiye anaweza kuwa mtu ambaye watu wengi wamekuwa wanasubiria miaka yote hii ili aivunjevunje ccm kutokea ndani.

Kama Kichaka alivyovunjavunja nguvu ya Republicans hapa US kwa sasa, Kikwete naye anavunjavunja nguvu na mshikamano wa ccm huko Tanzania kwa kasi kubwa ya ajabu. Kikwete ni zawadi ya krismas ya mwaka 2007 kwa wapinzani Tanzania. Swali la kujiuliza sasa ni kuwa, je wapinzani wako tayari kupokea zawadi hii toka kwa Mkwere ooopps Vasco Da Gama oops Kikwete na kufungua hilo box?

mjomba umechemsha, wapinzani Bongo wako kama huyu Paka
fail-24.jpg

au huyu:

6okxaop.jpg
 
Naona tunashindwa kujibu hoja kwa kutumia hoja. Kutoka Tanzania siku nyingi si kigezo kwamba watu hawako intouch na mambo yanayoendelea nyumbani.
 
Polepole ndugu, kama huna hoja soma tu utulie, sio lazima uchangie. Enzi ya kujibu hoja kwa matusi tulishaipita siku nyingi. Kutukana ni kielelezo cha wazi cha unyonge na u-primitive wa mtu, nawe kwa maandisha yako haya umethibitisha jinsi ambavyo ustaraabu bado mnapishana. Pole sana.

Asante Kitila,

Kuna watu wanajua kumwaga matusi tu kila mara time hoja zikiwaishia. Watasubiria hadi ikitangazwa kuwa wananchi wote wa kanda ya ziwa wahame ili kuipisha Barrick (mkataba wa Buzwagi unairuhusu Barrick kuchukua ardhi yoyote ile ambayo italeta manufaa kwa biashara yake) ndio wajue ubovu wa serikali ya CCM na mikataba yake ya madini!
 
Kwa uchache wa maneno ya Suleiman ya kututukana kwa ujumla wetu naomba Afungiwe milele kuingia forum hii . Kumwachia means wengine wataiga lugha ya kijiwe wakati watu wanakata issue . Yeye kaka Tanzania muda wote mbona wizi na wezi wako naye na hatujamwita mjinga ?
 
Hii mada ni muhimu sana, na swali moja ambalo litatakiwa kujibiwa ni "nani ataikoa tanzania na CCM". Hadi hivi sasa CCM hawataacha kula kwa vile tunalia njaa; CCM wataacha kula pale ambapo tutawafunga mikono na kuwaondoa mezani! Vinginevyo kama mbwa mbele ya bwana wake tutakufa tunafoka foka na mzee atatutupia tunyama (mabilioni ya JK) na tuminofu minofu (ahadi za uchaguzi) na wakati sisi tumekaa na ngoma zetu za kienyeji kushangalia kugawiwa kasungura hako wao watakuwa wanachinja ng'ombe mwingine! Ni mpaka pale tutakaposema kuwa "hatutaki tumefupa, na tuminofu" na sisi tunataka nyama na mchuzi! Hapo ndipo watawala wetu watajua kuwa Tanzania imefikia kilele chake! Hapa tunahitaji mabadiliko ya kifikra na ndicho hicho kwanza ambacho lazima tushinde kabla hatujashinda kwenye sanduku la kura.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom