Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,186
- 56
Kikwete anaimaliza CCM, je wapinzani mko tayari kuchukua nchi?
Kwa wale ambao mnafuatilia siasa za Marekani mtakumbuka mwishoni mwa miaka ya tisini jinsi Joji Kichaka alivyojihusisha sana na mambo ya conservative christians kwa kujifanya kuwa ni mwenzao na mtu aliyezaliwa upya (a born again christian).
Watu wengi bila kujua wakamuamini Kichaka na hata kufikia nafasi ya kusema kuwa Kichaka ameteuliwa na mungu kuwa rais wa marekani (maneno ya Pat Robertson). Demokrats kama kawaida yao wakalialia na kupiga makelele kuwa dini inaunganishwa na siasa bila kujua kuwa kitendo cha Kichaka kujiita mkristo safi kilikuwa ni zawadi kubwa sana ambayo wangeifaidi kwa miaka mingi ya baadaye.
Miaka saba baada ya Kichaka kuchaguliwa kuwa rais amewathibitishia wamarekani kuwa yeye sio mkristo wa kweli kama alivyodai mwaka 2000 bali yeye ni mwongo, mwonevu, katili, asiye na utu, mchoyo, mwizi, na maovu mengine yote. Hii sio tu kuwa imevunja nguvu ya ushawishi ya christian conservatives katika siasa za marekani, bali pia imewafanya wengi wao kuwapuuzia wale wote wanaojiita wamezaliwa upya na kutowachukua on face value (no wonder Giulian anafanya vizuri kwenye polls).
Miongoni mwa marafiki wakubwa wa Kichaka barani afrika ni ndugu yetu mtiifu Kikwete AKA Mkwere AKA Vasco Da Gama. Yeye naye kama rafiki yake Kichaka alivyofanya Marekani, aliupata urais kwa kuwa na propaganda machine kubwa, kuwateka watanzania kwa kuvaa ngozi ya kondoo huku pia akitumia mbinu za mbwa mwitu, kutumia waumini na viongozi wa dini na watabiri, kutumia kwa siri mapesa ya nchi, nakadhalika na kufanikiwa kushinda kwa "kishindo".
Miaka michache tu ya uraisi, the guy amethibitisha kuwa si yule handsome boy au mr nice kama vile viongozi wa dini walimsifia wakati wa kampeni. Miaka michache tu ya urais, Vasco Da Gama anatumia mabilioni ya nchi kusafiri nje ya nchi kwa safari ambazo hazieleweki, miaka michache tu Kikwete anaigawa CCM kwa kuwakumbatia mafisadi marafiki zake huku akiuza nchi kila leo.
Kikwete anaigawa CCM so fast kuliko hata alivyofanya Mwinyi na Mkapa. Wanaccm wengi wamegundua kuwa huyu ni Raisi aliyewarubuni ili awe rais kujitajilisha yeye na rafiki zake wachache wa ndani na nje (kina Sinclair). Ingawa Kikwete alichaguliwa kwa "kura nyingi" , miaka inavyokwenda inathibitisha Kikwete ndiye anaweza kuwa mtu ambaye watu wengi wamekuwa wanasubiria miaka yote hii ili aivunjevunje ccm kutokea ndani.
Kama Kichaka alivyovunjavunja nguvu ya Republicans hapa US kwa sasa, Kikwete naye anavunjavunja nguvu na mshikamano wa ccm huko Tanzania kwa kasi kubwa ya ajabu. Kikwete ni zawadi ya krismas ya mwaka 2007 kwa wapinzani Tanzania. Swali la kujiuliza sasa ni kuwa, je wapinzani wako tayari kupokea zawadi hii toka kwa Mkwere ooopps Vasco Da Gama oops Kikwete na kufungua hilo box?