Elections 2010 Kikwete ni mkweli na anawaheshimu Watanzania

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Naamini kuwa Kikwete, iwapo atatangazwa kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo atakuwa mkweli na kuonyesha heshima kubwa kwa Watanzania wote, waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura kwa kutekeleza ahadi alizozitoa katika kampeni zake. Naamini kwamba ni kutokana na ahadi hizo alizotoa, ndizo ambazo zilimfanya apate kura hizo za kumpa ushindi.

Natumaini kuwa ahadi hizo alizitoa mbele ya Watanzania watu wazima, na wengine wengi wakiwa na umri mkubwa kuliko yeye. Ni adabu na heshima kusema ukweli katika jamii yetu. Atakuwa amewafanyia heshima kubwa Watanzania kwa kutimiza ahadi hizo alizotoa na kwa wakati alioahidi. Wananchi wengi tutakuwa tunafuatilia ahadi hizo kwa umakini sana katika kipindi kijacho. Ahadi hizo ni:

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
35. Kulinda haki za walemavu- Makete
36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
42. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Kama akitawazwa ataanza na visirani vyake tuu na kuanza visasi
 
Sasa itakuwaje maana karibu yote haya yalikuwa yategemee Obama, na sasa Obama yupo njiani kuondoka madarakani.....?
 
Sasa itakuwaje maana karibu yote haya yalikuwa yategemee Obama, na sasa Obama yupo njiani kuondoka madarakani.....?

Ataomba misaada uarabuni, lakini kwa sharti la kujiunga na OIC na kuanzishwa mahakma ya kadhi na sharia.

Hapo ndipo mtakapojuta kuzaliwa Tanzania
 
Niambie moja ya ahadi hizo yenye uhusiano na kujenga uchumi na kuondokana na utegemezi wa magharibi! Zote hizo ni shughuli za kila siku za Halmsahauri za Wilaya
 
Atatafuta excuse kumbe nyie hamjui, hapa alisingizia mtikisiko wa uchumi
 
Aksante Mkuu Dingiswayo kwa kuileta hii!
Mara baada ya kuiona nimecopy na kuisevu mahala pa salama kabisa...nitakuwa na'update kama wengine watakumbuka mpya!
Akianza kushindwa utekelezaji ataomba Tanzania ipate CRISIS ili iwe sababu...shindwa!
 
Anajua kwamba hatutamuuliza sababu anamaliza ngwe yake ya mwisho - Hata robo ya hizi ahadi nina imani 100% hatazitimza. tutegemee maisha magumu zaidi, nawahurumia sana watanzania wangu walio vijijini waliomchagua bila kujua kwamba jamaa ni msanii.
 
Mkuu Dindswayo:

Tunaweza kuiweka hii ikawa Reference come 2015?

MODS please do the necessary!:doh:
 
Back
Top Bottom