Kikwete ni mdini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ni mdini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzito Kabwela, Oct 28, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kamati yake ya Kampeni inaongozwa na hawa wafuatao:
  1. Abdulrahman Kinana- Muislam
  2. Yusuph Makamba-Muislam
  3. Salma Kikwete- Muislam
  4. Miraji Kikwete- Muislam
  5. Ridhiwan Kikwete- Muislam
  6. Rashid Shamte- Muislam
  7. Mohamed Garib Bilal- Muislam
  Kampeni zake zinachagizwa kwa mbwembwe na madaha zikihusisha Radio Iman, Raio Quran, Sauti ya Adhana.
  Awali magazeti ya Annuur na Alhuda yalikuwa yakimtukana Slaa kwa matusi ya Ubaguzi uliopitiliza,serikali haijakemea wala haikuona kama hiyo ni tishio la umwagaji damu badala yake wakatishia magazeti makini ya Mwananchi na Mwanahalisi.
  Leo imedhihirika kuwa matusi yote yaliyoelekezwa kwa Slaa(PhD) toka kwenye magazeti hayo yanayomilikiwa na Taasisi za kiislam yalilenga kumnufaisha JK(BA Economics) na ndio maana hayajakemewa na serikali.
  Gazeti la Alhuda leo limekuja na kichwa cha habari JK ASUBIRI KUAPISHWA kichwa kingine SLAA AZIKATAA KURA ZA WANAWAKE WA KIISLAM.
  Gazeti la Taifa Tanzania ambalo linahaririwa na Prionce Bagenda chini ya mwamvuli wa Mafisadi limekuja na habari ya kupika ambayo inawafarakanisha waislam na wakristo. Habari hiyo ipo kwenye frontpage ya kijarida hicho.
  Mtazamo wangu, JK ni mdini, na kama ni hivyo nchi hii chini ya utawala wake kama akifankiwa kuiba kura na kutangazwa mshindi atawezaje kuyaunganisha makundi haya hasimu kwa imani za dini?
  Rafiki yangu mmoja mkristo ameachana na mwanamke wake wa siku nyingi kwa sababu za siasa zilizoegemea kwenye udini. Mwanamke pamoja na kutambua kuwa JK hajui na hawezi kutawala amesisitiza kuwa atamchagua JK kwakuwa tu ni dini moja na ya kwake. Zogo likazidi na hivi sasa tupo kwenye kusuluhisha.
  Tuna kazi kubwa baada ya Uchaguzi!
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  naomba tuwachukulie kama watanzania kwanza..! kama watafanya mambo bila kubagua dini then mie sioni tatizo..!

  mm ni mkristu ...ila sipendi kuhesabu watu kulingana na dini ama makabila yao..!

  lingekuwa suala la kadhi au OIC ....hapo huwa nakuwa mbogo..!
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kikwete ni mdini sana. hata ukipitia wizara zote angalia idadi ya waislam kuanzia makatibu wakuu mpaka wakurugenzi wasaidizi. tuwe wakweli jamani. huyu jamaa ni mdini wa chinichini anakwenda kwa vitendo tu. lakini tabia yake hiyo itamtokea puani tarehe 31 oktoba 2010.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  mbaya zaidi serikali haijawahi hata japo kukemea vijarida hivyo vya kiislamu vinavyoleta udini ktk nchi yetu...........serikali haiwezi kukemea wala kuchukua hatua kwa sababu vijarida hivyo vina tetea uislamu na uislamu ndiyo dini ya viongozi wa juu wa serikali ambao ni akina kikwete na vinyamkela vingine
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Baba askofu moses kulola amemsifia hadharani na kusema kuwa ni kiongozi safi
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  taifa letu linateketea kwa kukosa watu safi
   
 7. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mungu wangu, una habari huyu bwana kakoroga nchi kisa Udini!!! Nyerere angerudi kweli si angetucharaza viboko sie tunao lea hali hii?
   
 8. asam.thegunner

  asam.thegunner Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama statistics basi tunaweza kusema JK kawapendelea wakiristo mfano zaidi ya 65% ya mawaziri ni wakiristo, wakuu wa mikoa wengi ni wakiristo, wakuu wa wilaya, majajina karibia kila sekta wengi ni wakiristo. JK hana hata chembe ya udini ila nyie ndio mtaka kuleta mambo hayo ya udini. Tuachane na proganda siziso na tija kwa taifa letu hakuna atakayeumia pindi mambo yakiharibika ila ni mimi na wewe au ndugu zetu. Mungu ibariki Tanzania.
   
 9. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,595
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Kikwete Siyo mdini, hakuna ushahidi wowte wa kuonyesha kuwa ni mdini.
  Miraji Kikwete ni mwanae kwa hiyo by default atakuwa ni mwislamu
  Salma Kikwete ni mkewe kwa hiyo chance ya mtu kuoa dini ya kwake ni kubwa zaidi.
  Gharib bilal ni Mzanzibar ambayo zaidi ya asilimia 95 ni waislamu.

  Baraza la mawaziri la Kikwete Asilimia 56 (Mawaziri pamoja na manaibu waziri na yeye akiwemo) ni Wakiristo, Waislamu ni asilimia 44 tu,

  Wenye kuleta hoja ya udini wa Kikwete ndiyo wadini, watu wenye chuki binafsi, wasio na ulewa mpana, washabiki. ni watu walioishiwa hoja.

  Msidhani mtamsaidi dr slaa kuingia Ikulu kwa kutumia njia za kuwagawa watu kwa misingi ya kidini, hata akiingia ikulu kwa njia hizi atashindwa kuongoza wala kutawala.
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Kweli kikwete ni mdini kama walivo watanzania wote. Sec.19 subsec.1,2 n 3. Tanzania ndo haina dini. Sishangai mtu kuwa mdini isipokuwa hasimdhuru mwenzie kiimani. Ni dhambi kubwa tulioizaa watawala wa sasa kuwakumbusha kuwa kuna dini Tanzania, kwamba Dr.slaa ni mdini,haya yote yatatugarimu. Wakuu nawahakikishia kuwa mwaka 2015 kura zitapigwa kufuatana na dini,asimi usiamini hii dhambi ya udini haitafutika,watawala wameiua nchi kwa ili.
   
 11. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri hayo hayatuhusu isipokuwa matendo yake
   
 12. Mkoroshokigoli

  Mkoroshokigoli JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2016
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 14,419
  Likes Received: 2,519
  Trophy Points: 280
 13. Zamiluni Zamiluni

  Zamiluni Zamiluni JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2016
  Joined: Feb 11, 2014
  Messages: 11,267
  Likes Received: 7,257
  Trophy Points: 280
  Huu uzi !! huu uzi ni katika uzembe wa mwisho ktk nyuzi zote humu JF !! imeprove..hata wachangiaji miaka yote (6yrs) haijakamilisha pahe moja !! khaaaaaaaaaaaaaaaaaaah .. Jamanii tuw waTZ waTaifa kwanza !!
   
 14. R

  Ralph Tyler JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2016
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 788
  Likes Received: 658
  Trophy Points: 180
  Unabii huu haukutimia kwa kuwa ulikuwa wa uongo tangu mwanzo. JK hajawahi kuwa mdini kwa namna yoyote unayoweza kumuelezea. Na leo hii hata upinzani wanashuhudia kuwa JK ni miongoni mwa marais bora kabisa ambao nchi hii imepata kuwa nao. Na japo wanapinga kila JPM anachofanya au kusema, atakapostaafu watakuja hapa na kusema wanamkumbuka au wanam-miss! Siasa za upinzani katika nchi yetu zimekosa consistency of issues, wanang'ang'ania matukio na kauli tu, zikikishapita wakati wake wanakosa hoja.
   
 15. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2016
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 14,461
  Likes Received: 21,432
  Trophy Points: 280
  Adui Mkubwa wa Uongo ni Muda.
   
 16. Luhanyula

  Luhanyula JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2016
  Joined: Jan 26, 2016
  Messages: 1,316
  Likes Received: 1,688
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni mdini?.
   
 17. Yamakagashi

  Yamakagashi JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2016
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 4,426
  Likes Received: 7,563
  Trophy Points: 280
  Mbona hizi threads za Kikwete ni mdini hazifiki hata page tatu lakini thread inayosema Magufuli ni mdini inatoboa page 20 ?
   
 18. Luhanyula

  Luhanyula JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2016
  Joined: Jan 26, 2016
  Messages: 1,316
  Likes Received: 1,688
  Trophy Points: 280
  Nikweli mkuu lakini angalia nyuzi ni mwaka gani,nafikiri pia utajua miaka hiyo niwatu wa aina gani walikuwa member wa JF.
   
 19. BAFA

  BAFA JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2016
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,331
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Duuuuhhhh akilalamika khalifa hamisi anaambiwa mchochezi
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2016
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Duh hii kali kumbe udini uliletwa na Chikwete leo masheikh wanamlaumu Pogba.
   
Loading...