Kikwete ni mbinafsi?

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Rais kikwete inaonyesha hakubaliani kabisa na baadhi ya sheria za utumishi zinazotumika hapa kwetu Tanzania kwa mfano;

1. Sheria ya utumishi inayotaka mtumishi wa umma apewe mwaka mmoja kwa ajili ya kumtazamia yaani probation period.

1. Katika sekta binafsi wakati mwingine wanatoa Probation period ya miezi sita.

Kwa mujibu wa kikwete hiki ni kipindi kifupi sana kwa mtu kujifunza kazi na kuthibitishwa, ndo maana kwa mamlaka aliyonayo kama mtu aliye juu ya sheria akatangaza wakati wa kampeni na akajipa yeye kipindi cha miaka mitano kama ni kipindi kifupi kilichomtosha kujifunza kazi Ikulu kama Rais na baada ya kumaliza hicho kipindi cha miaka mitano akawaomba watanzania mda mwingine wa ziada ili aweze kufanya kazi alizo jifunza ndani ya miaka mitano na bila hiana robo ya Watanzania waliojiandikisha kupiga kura wakakubaliana na hilo wakampatia fursa nyingine.


Kwa maneno ya kikwete alitaka amaanishe kwamba tusimuhukumu kwa miaka mitano aliyokuwepo madarakani maana nikipindi kifupi alichokitumia kujifunza kazi hivyo mtu kuhukumia kwa utendaji kazi anatakiwa apimwe kwa kipindi zaidi ya miaka mitano.


Sasa nawauliza wana Jamvi wenzangu;

1.Je hizi sheria za utumishi zibadilishwe? maana hata mkuu wa nchi ameliona hilo kwamba at least mtu akipata probation period ya miaka zaidi ya mitano itamtosha kujifunza kazi.

2. Na kama kweli hizi sheria za utumishi hazimtendei haki mtumishi, Je Rais kikwete ni mbinafsi? Kwasababu ameliona hilo lakini ameona lina apply katika urais tu, maana hajawahi kuikemea hii sheria kwamba inawabana wafanyakazi hivyo ana onyesha hataki watumishi wote tupewe mda mrefu zaidi wa kujifunza kazi.:target:
 
Back
Top Bottom