Kikwete ni kichwa kwa hii speech nimeikubali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ni kichwa kwa hii speech nimeikubali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by i pad3, Apr 14, 2012.

 1. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] Prof Baregu akataa Biblia & Kurani

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] RAIS Jakaya Kikwete amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hautavunjwa na wala Watanzania wasitarajie kuwa Tume ya Katiba itawahoji kama uwepo ama usiwepo.

  Msimamo huo ulitolewa jana na Kikwete alipowaapisha wajumbe wa tume hiyo katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, itakayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba.

  Badala yake alisema kazi ya tume hiyo itakuwa ni kuratibu maoni ya Katiba mpya, na namna ya kupata maoni ya kuimarisha Muungano na kuuboresha kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili na sio kujadili kuwepo au kutokuwepo.

  Kikwete aliongeza kuwa kazi ya tume ni kutafuta Katiba inayojali maslahi ya Watanzania wote na si kikundi cha watu wachache lakini pia itakayoheshimu mipaka ya mihimili mingine ya dola na kulinda Muungano.

  Alisema tangu mwaka 1984, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haikuwa na haki nyingi za raia ambapo kutokana na hali ya sasa, taifa linahitaji kuwa na Katiba ambayo itakuwa na haki nyingi za msingi za Watanzania zinazoendana na matamko ya Umoja wa Mataifa.

  Akizungumzia suala la mgombea binafsi, Rais Kikwete, aliwataka Watanzania kuamua kwa kutoa maoni yao ya kuwepo au kutokuwepo kutokana na hoja hiyo kupigiwa kelele mara kwa mara huku serikali ikishutumiwa kuweka ngumu.

  Rais Kikwete alisema kutokana na umuhimu wa kazi ya tume hiyo, serikali itatoa ulinzi wa kutosha mara tume hiyo itakapoanza kazi rasmi ya kuratibu maoni ya wananchi ikiwemo kupambana na watakaofanya fujo kwa kuchukuliwa hatua na vyombo vya dola.

  Awageukia wajumbe wa tume

  RAIS Kikwete amewataka wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katika kuwa makini na waadilifu wakati wa mchakato wa kukusanya maoni kwa wananchi, huku wakizingatia zaidi maslahi ya taifa badala ya kuangalia makundi binafsi.

  Akiwaambia wajumbe wa tume hiyo itakayoanza rasmi kazi yake Mei Mosi, Kikwete aliwataka kuwa wavumilivu na kupokea mawazo ya kila mtu kwa uhuru bila upendeleo wa aina yoyote.

  "Nina matumani makubwa na wajumbe wa tume hii ambayo imeapa leo na Watanzania nao wana imani nayo ndiyo maana hata pale nilipoitangaza baada ya kukamilisha hatua ya uteuzi wa majina, wengi wamepongeza.

  Wapo wachache tu ndiyo ambao wanaweza kuonyesha kutoipenda kwa sababu zao ambazo hata ukiwauliza kwa nini hawatakuwa na majibu.
  "Imani huzaa imani, hivyo matarajio yetu kazi ambayo itafanywa na tume hii ni kwa ajili ya wananchi wote.

  Hatutarajii kuona baadhi ya wajumbe wanakusanya maoni kwa kutanguliza maslahi ya makundi ambayo wanatoka. Watafanya kazi kwa kujua wana jukumu la kuwawezesha Watanzania wote kupata Katiba ambayo wanayoihitaji," alisema Rais Kikwete.

  Alisema hata kama kuna mjumbe ambaye anatoka katika chama cha siasa ama taasisi fulani atambue sasa taasisi anayoitumikia ni moja na chama chake ni cha Watanzania wote. Hivyo hatarajii kuona wajumbe wa kamati hiyo kwenda kinyume na matarajio yaliyokusudiwa na wengi.

  Rais Kikwete alisema kuwa kukamilika kwa mchakato huo kutafanya Watanzania kupata Katiba ambayo itaendena na mazingira ya sasa na wakati uliopo na ikiwezekana kwa ajili ya kutumika kwa miaka mingi ijayo.

  Hata hivyo Rais Kikwete alisema kuwa ili kufanikisha mchakato huo kwa amani na utulivu ni vema wananchi wakawa wavumilivu, maoni ya wananchi wote yasikilizwe na kupewa nafasi ya kuchambuliwa kwa kulinganisha hoja.

  "Hakuna sababu ya watu kuzomeana kwa sababu ya maoni kutofanana na maoni ya mtu mwingine ambaye ana mitazamo yake. Hata kama kuna maoni ya watu ambao wanajifanya wana akili wakayaona ni ya kipuuzi ni bora yakasikilizwa na hao wenye akili nao wasikilizwe.

  Hakuna sababu ya watu wataalumu kutaka maoni yao ndiyo yapewe nafasi bali kila mmoja atoe maoni yake kwa maslahi ya wote," alisema Rais Kikwete.

  Alikiri kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo na hali ya kutoaminiana kati ya serikali na baadhi ya wadau, na hivyo, kuzinduliwa rasmi kwa tume ya kuratibu maoni ya kupata Katiba mpya ya nchi ni ishara tosha ya taifa kuingia katika historia iliyotukuka kwa kuanza safari mpya ya kuelekea kuzaliwa kwa Katiba mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania wenyewe.

  "Mwalimu Julius K. Nyerere, alisema mawazo hayapingwi kwa rungu bali hujibiwa kwa mawazo yaliyo bora zaidi. Ni vema mtambue kuhamaki si jibu ila jambo jema ni kutoa mawazo yako yaliyo bora zaidi. Kama Watanzania tutaifanya kazi hii kwa moyo tutafanikiwa kupata Katiba iliyo bora itakayolilea taifa letu katika miaka 50 ijayo," alisema Kikwete
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata afanyaje kuna HATERZ wa CDM hawampendi just for being a mslm. loosers
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwanini auzuie muungano kujadiliwa na wala si Kadhi na OIC?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bado kwangu mimi atabakia ni Utumbo na Msanii ! Angalia deni la taifa na uchumi uko mikononi mwa mafisadi wenzake
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  hivi huyu msanii hajatoa filamu tu?

  nilisikia anasoma script watoe moja na vicent kigos ray na akina aunt Ezekiel, the guy will be the main character
   
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ungejua JK mwenyewe ni CDM damu damu, usingesema hayo mkuu.
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Is this the best what u can say!!.......kuwa na jina la kiislamu ndiyo uislamu? ndio maana mliingizwa mkenge na Fatuma Kimario kumbe mwenzenu ni mfuga nguruwe maarufu pale Mbezi Beach. ur total upstairs empty.
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha ha ha.........................
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  kama nimemuelewa vizuri ni kwamba amewaasa kutokupendelea makundi fulani na badala yake wavae utanzania. Kwangu mimi hiyo inatosha.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tumeona wanavyochota fedha za NSSF na hawataki kuzirudisha!
   
 11. m

  mams JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Terms of Reference (TOR) wasijadli kuuvunja Muungano. Bali wajadili jinsi ya kuimarisha!
   
 12. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nyie ndiyo mnaohatarisha amani ya Tanzania, hivi watu waliomponda sana Lusinde na Mkapa kwa kuteleza ndimi zao nao wanawachukia hawa watu kwasababu ya Ukristo wao?? au Lowasa jamii inamchukia kwa ajiri ya Ukristo wake? nyie ndiyo mnaifanya dini ya Kiislam ionekane imejaa watu wenye uwezo finyu ambao siku zote wanataka wapate upendeleo maalum kwa Serikali kama walivyo wanawake na watoto.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanini azuie kujadiliwa Kadhi na OIC?
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa, kikwete ni kichwa cha nyoka!
   
 15. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Watu wanaropoka tu bila kuangalia wanaemtaja hapa ndio mkuu wa nchi na serikali.
  OTIS
   
 16. M

  Mnyaturu Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhuru wa mawazo ya mtu nafsi yako haiwezi kuyazungumzia.ama kweli ya moyoni yaliponzwa na ulimi.
   
 17. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 701
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Si hotuba mbaya ipo 50/50
   
 18. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Speech gani ya kikwete uliyoikubali mkuu? Au hujaielewa?
   
 19. SR senior

  SR senior JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 342
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  we umeelewa vp?
   
 20. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hotuba nzuri tatizo ccm hawana dhamira///////
   
Loading...