Kikwete ni hatari zaidi kwa ccm kuliko dr slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ni hatari zaidi kwa ccm kuliko dr slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyauba, Mar 2, 2011.

 1. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni wakati muafaka sasa kwa wanachama,wapenzi na viongozi wa CCM kutambuaa hatari ya kuwa na Mkiti/mwanachama wa aina ya Kikwete ndani ya chama chao.

  Hali ya kisiasa nchini inaonyeshaa dhahirii,Kikwete alivyowezaa kukidhoofishaa CCM kupitiaa hulka yake ya kupendaa kufanya kazi kupitia mitandao.

  Kwa sasa CCM imekuwaa dhaifu kuliko wakati wowote wa historia yake na hivyoo kuwa katika hatari ya kuvunjikaa kutokana na makundi yanayoasimianaa ndani ya chama kwa kasi ya ajabu.

  Wana CCM amkeni!!!!!!!
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Tuko macho,usifikiri hao wanaoandamana na kutaka atoke madarakani wote ni CHADEMA,maisha magumu yanatufanya tuwe wamoja na kuweka ushabiki wa chama pembeni....tunaunga mkono wale wanaotuonyesha njia ya kupata haki zetu na si siasa za CCM za kulindana na kunufaisha wachache wengi tukiteseka.....kwa hali ya sasa,hakuna hata anayesinzia ndugu yangu!!!!CCM haijadhoofika tu iko mahutihuti.
   
 3. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mitandao inasaidia unadhani bila mtandao angeupata u-prezdaa?
   
 4. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Umemsahau makamaba na Tambwe!
   
 5. CPU

  CPU JF Gold Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ningependa kuona watu wa aina ya Samuel Six wanapewa kuongoza nchi hii.
   
 6. CPU

  CPU JF Gold Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hao wasingekuwa hatari bila Mkwere
   
 7. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kikwete+CCM=Maisha duni kwa watanzania
   
 8. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umewasahau akina Chiligati na Kinana.
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,858
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  Umemsahau Mlinzi mkuu wa Rais = Shekh Yahya.
   
 10. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tena hatari kwelikweli!!!!
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Msimsahau Riz1.
   
 12. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  CPU watu wa calibre ya Six ni threat ndani y ccm haitatokea wakapewa uongozi katika ngazi ya juu zaidi ya hapo alipo kama una kumbuka mwaka 1966 six na wanachuo wenzake waligoma kwa kupinga mfumo wa kinyonyaji kwani watu wachache walikua wanafaidi rasilimali za nchi ingawa Mwl Nyerere aliwafukuza chuoni lakini kwa kuanzia alijipunguzia yeye na mawaziri mishahara yao na kukiri kuwa kweli walikua ni moja ya mfumo wa kinyonyaji sasa kama SIX aliweza kumchalenji Mwl hawa waliopo si ndio atawasambaratisha kabisa ndio maana wanataka kumfanya awe underdog muda wote
   
 13. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  SIX yeye tuu kawa mnafiki kwa kujifanya anasomaa mchezo kwa tahadharii..kiukwelii anao kauwezo cha kuwatingishaa sana..ila lazima awe mwangalifuu kwani naye wanamjuaa vemaa tuu. pia bado kwa dhati moyonii hajaguswaa kuwakomboaa watanzaniaa kiutawala nje ya CCM.

  Kundi lao (akina SIX) linakua na natumai mpka 2015 watakuwa na idadi ya kutosha kutoa kauli ya pamoja ndani ya chamaa..na huendaa mkwere akawa anawachekeaa kiania awatumie kuvukaaa..
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kushauri CCM wachukue uzoefu wa ANC dhidi ya Thabo Mbeki na wafanye mabadiliko ya uongozi ili kurudisha dhana ya CCM chama cha Wakulima na Wafanyakazi.
   
 15. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  safi Kiongozi,kwahiyo ugomvi wako ni dhidi ya baadhi ya wanachama wa ccm na sio wote wa ccm,maana kama mh Samuel 6 akiiongoza nchi c ccm bado itakuwa inaongoza? au watu wa aina ya kina Samuel 6 ni akina nani?
   
 16. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kufa kwa CCM ni heri yetu sisi cause imekuwa kama jok linalokula watu.
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  RA, EL, NK ndo wenye remote ya ikulu. Ni kama movie za ki-vampire, akikung'ata unakuwa mmoja wao. JK ni Vampire already.
  Wanasambaa kama magugu. Kutegema SIX et al watakuwa na influence CCM 2015 4get it.
  The only way ni kuzika CCM. System corrpted.
  To restart Tanzania.
   
 18. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yes,
  kwa hesabu za kawaida za pinda

  MKapa + Mangura + EPA + All ccm members = 80% in 2005
  Kikwete + Makamba + R1 + Salma + TISS +Kinana + Dowans = 61% in 2010
  kazi ipo 2015.
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete akiagana na Msaidizi wa Makamu wa Rais Bw . Agostin Ngonyani pamoja na viongozi wengine wa serikali kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Jana alipokuwa akielekea nchini ufaransa na Ivory Coast. Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal.

  [​IMG]

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kutoa mada juu ya umuhimu wa shughuli za uziduaji na uwazi katika mapato ya madini katika mkutano wa Kimataifa wa Tasnia ya Uziduaji, (Global Extractive Industries Transparency Initiative -EITI), ambayo ina malengo ya kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia. ​

  Mkutano huo wa siku mbili unaanza kesho, Jumatano, Machi 2, 2011 jijini Paris, Ufaransa, na Rais Kikwete anaondoka nchini leo asubuhi kwenda kuhudhuria mkutano huo.​

  Tanzania iliomba na kupewa uanachama wa muda wa EITI tangu mwaka 2009. Tanzania itaweza kupata uanachama kamili baada ya kuwa imekamilisha na kutimiza vigezo vya kuwa mwanachama kamili na kuweka misingi ya utoaji taarifa hizo muhimu kwa umma juu ya malipo ya kodi kutoka makampuni mbalimbali yaliyopo nchini.​

  Lengo kuu la kujiunga na EITI ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia kwa kutangaza hadharani malipo yanayotokana na rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi wake.Utaratibu huu utaweka uwazi na kuondoa usiri ambao unaweza kuwa mwanya wa kuficha mapato halisi ya makampuni husika.​

  Baada ya kumaliza mkutano huo wa Paris, Ufaransa, Rais Kikwete atasafiri kwenda moja kwa moja Nouakchott, Mauritania kwa ajili ya kikao cha marais wa Afrika wanaotafuta suluhisho la tatizo la kisiasa katika Ivory Coast.​

  Katika Mauritania, Rais Kikwete atajiunga na marais wa Mauritania, Afrika Kusini, Burkina Faso, Chad, Nigeria na Equatorial Guinea pamoja na wawakilishi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Balozi Jean Ping na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN).​

  Katika kikao hicho, viongozi hao watafikia uamuzi wa AU kuhusu mzozo huo na kupendekeza namna gani ya kuutatua mzozo huo uliolipuka kufuatia raundi ya pili ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa Ivory Coast Novemba 28, mwaka jana, 2010.​

  Matokeo yake, nchi hiyo imegawanyika katika sehemu mbili, moja ikimuunga mkono aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Alassane Quattara na nyingine ikimuunga mkono Rais aliyekuwa anatetea kiti chake katika uchaguzi huo, Mheshimiwa Laurent Gbagbo.​

  Kila mmoja kati ya wanasiasa hao amejitangaza kuwa Rais na kila mmoja ameunda na kutangaza Serikali katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Wiki iliyopita, viongozi hao wa Afrika walikutana mjini Nouakchott na baadaye wakaenda Abidjan, Ivory Coast ambako walikutana na viongozi hao wawili nchini humo katika jaribio la kutafuta suluhisho la mzozo huo.​
  Imetolewa na:


  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,


  Ikulu,  DAR ES SALAAM
   
 20. L

  Leornado JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Lini TZ tutaipata bahati ya raisi wa tz kufariki ili uchaguzi urudiwe na mambo yaanze moja?

  This JK is a curse, he deserves hell. We are tired, u r the worst ever.
   
Loading...