Kikwete: Ni bora Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge

kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,716
999
Kwa wale waliobahatika kusoma gazeti la Mwanahalisi la leo kwenye kichwa cha habari nanukuu" Askofu huyu katumwa na nani?" mwaandishi kaandika kuwa kikwete alinukuliwa kwenye mikutano yake ya kampeni huko Singida kuwa

"Ni bora Dr Slaa kuwa raisi kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge" hii hofu ya Muungwa kwa Tundu Lissu inatokana na nini?

======

Askofu huyu katumwa na nani?

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 10 November 2010

ASKOFU wa Kanisa Katoliki anategemewa azungumze mambo ya maadili na imani. Anatarajiwa afundishe mafundisho ya kanisa, yasiyoegemea upande wowote wa kisiasa kwa kuwa yeye ana waumini wa vyama mbalimbali katika kanisa lake analoliongoza.

Katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani uliomalizika hivi karibuni hali imekuwa tofauti.

Uchaguzi umepita, walioshinda wanafurahia mitaani, walioanguka wanasikitika; yote hayo ni maamuzi ya wananchi na yanapaswa kuheshimiwa.

Katikati ya shangwe, wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki walitumiwa ujumbe kupitia mbunge wao, Tundu Lisu. Ujumbe huo ulitoka kwa mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya, unaomtaka mbunge huyo mteule aache kufurahia ushindi kwa nguvu, na kupeperusha bendera huku akipita na vipaza sauti.

Sababu? Eti kwa kufanya hivyo anawaumiza wale walioshindwa. Huku ni kupotosha maana ya mashindano.

Hakuna shida. Tatizo ni kwamba waliotuma ujumbe huo ni viongozi wa serikali, yaani mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya – Singida.

Mbaya zaidi aliyetumwa kuwasilisha ujumbe huo ni kiongozi wa Kanisa Katoliki mkoani humo, yaani askofu. Tunashindwa kuelewa.

Ilikuwaje mkuu wa mkoa, na mkuu wa wilaya wamtume askofu huyo kumwambia mbunge wetu maneno hayo? Hakukuwepo na watu wengine wa kutumwa katika ofisi ya viongozi hao wa serikali ila atumwe kiongozi huyo wa kiroho?

Na kwanini kiongozi huyo wa dini alijishusha sana kiasi cha kutumwa kazi kama hii isiyo na tija kwa kanisa? Na alikubali kuifanya kwa maslahi ya nani? Kwa ajili ya nini?

Askofu ananukuliwa akimwambia Lissu kwamba K"wa kuwa umepata ulichokuwa unatafuta usiwahamasishe wananchi waache kuchangishwa." Loo!

Mojawapo ya sera zilizomwongezea umaarufu Lissu katika kampeni zake ni kuzuia michango yote haramu, ukiwemo wa sekondari. Hoja ya Lissu ni kwamba mchango huo ni haramu kwa kuwa haukupitishwa kisheria na bunge.

Lisu amekuwa akihoji kuwa pesa nyingi zinazotengwa na serikali hazifiki kwa wananchi kujenga shule, hivyo anataka serikali iwajibike kujenga shule hizo kwa pesa za kodi badala ya kuwatoza wananchi michango ambayo imekuwa ikiwanufaisha wachache.

Lissu amekuwa mkali pia kwa vizuizi vinavyowekwa barabarani kukusanya ushuru wa mazao, kwani upo kinyume. Sheria ya serikali za mitaa liyofuta ushuru wa mazao ilitolewa kupitia tangazo la serikali Na 231, la tarehe 3/5/2002, wakati huo Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi akiwa waziri mwenye dhamana.

Sasa Bunge hadi sasa halijatunga sheria nyingine tofauti na hiyo, hivyo kuonekana kuwa serikali imewaibia Watanzania michango na au ushuru haramu kwa miaka minane.

Hayo ndio madai ya mbunge huyu machachari. Lakini askofu huyu ameenda kumshauri aache kuzungumzia ajenda hizi. Inakuwaje askofu anapokuwa anapenda wananchi wake kutozwa ushuru isivyo halali? Askofu anatumia gari yake inayolipiwa mafuta kwa sadaka za wakristo toka Singida mjini hadi Dung’unyi kwa Tundu Lissu kueleza mawazo mepesi haya.

Njia nzima Roho Mtakatifu hakumshukia askofu huyo amshauri tofauti? Wananchi wa Singida wamekuwa wakisikitishwa na baadhi ya dhuluma zinazoonekana kufanywa na viongozi hao waliomtuma.

Wananchi wamedhulumiwa mashamba katika mradi wa umeme unaotarajiwa kuanza, wananchi wameendelea kunung’unikia kuuzwa kwa majengo ya Chama cha Ushirika mkoani (SIRECU), wananchi wameendelea kushuhudia mikataba tata ya kifisadi katika jengo la utamaduni lililopo mjini Singida.

Wananchi wamekuwa wakitozwa ushuru usio halali mjini Singida, hutozwa fedha kwa ajili ya usafi wakati mji wa Singida ni mchafu. Hayo yote yanahitaji mtetezi.

Askofu anapoamua kumwonya mtetezi wa haki ili kutumikia mafisadi hawa, analenga nini? Anafaidika vipi na uongozi unaolalamikiwa na wananchi? Yeye kama askofu aliumia vipi na kwa nini aliumia na ushindi wa Lissu, hadi aone walioshindwa wanahuzunika?

Je, anakubalina na rushwa iliyotumika kuwanunulia wananchi vitenge, kanga, magodoro fulana na kofia alizokuwa anatoa yule aliyeshindwa? Anamhurumia aliyeshindwa kwa kuwa alitoa fedha nyingi kupita kiasi kuhonga wananchi? Anatufundisha nini sisi waumini wake kwa siku zijazo?

Je, kuwahurumia watoa rushwa walioshindwa huku akiwawaonya walioshinda kihalali waache kushangilia ushindi wao ni msimamo wa kanisa au wake binafsi?

Maaskofu wangapi walifanya kitu kama hicho kwenye majimbo yao? Askofu huyu atatumiwa na mkuu wa mkoa kwa mambo mangapi? Na atatumiwa vile kwa muda gani? Na alipotumwa hakugundua kuwa mkuu wa mkoa anao watu wengi wa kutuma kwa mambo mepesi kama hayo ili amshauri vinginevyo kuliko kujitolea kwenda?

Ziara yake kwenda kuonana na Lissu ililipiwa kiasi gani toka kwa mkuu wa mkoa? Kwa nini hakupewa gari na ofisi ya mkuu wa mkoa akaamua kutumia gari yake inayolipiwa na waamini wa kanisa hilo? Ni kitendo cha aibu, ambacho kama bado kipo kwenye akili za waumini, basi ni cha kuvumilia.

Lakini mkuu wa mkoa wa Singida na askofu huyu wamedhalilisha kanisa kwa kutumia gari ya askofu kufanyia siasa ambazo hazina lengo la kumkomboa maskini wa Kitanzania.

Si vema askofu kuwabeba viongozi wa aina hii, ni aibu katika jamii. Tunamwomba Mungu awajalie busara wasirudie mchezo mchafu kama huu. Na kwa aibu hii ingefaa askofu na mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya waombe radhi wakristo kwa Singida kwa kutumia gari la wakristo kwa shughuli zenye manufaa ya kifisadi, yasiyo na tija hata kidogo kwa maendeleo ya Kanisa.

Hofu ya viongozi wa serikali kwa ushindi wa Lissu imekuwa kubwa tangu wakati wa kampeni, ndio maana akiwa Singida, Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema; "Heri Dk. Slaa awe rais, kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge."

Pamoja na hayo yote tunawaomba viongozi wa serikali na viongozi wa dini msipingane na sauti za wananchi. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

Chanzo: Mwanahalisi
 
yeye mwenyewe anamjua tundu lisu ni mtu wa kazi


sasa tundu lisu kawa mbunge na kama ilikuwa hofu ya huyu jk basi aachie ngazi na kumpisha slaa, na sababu iwe hii ya kuwa ana mhofu lisu


atakoma mwaka huu


mkikutana nae huyu kikwete mwambieni ule upuuzi wake wa kukatisha dozi aache mara moja.
 
Mkuu mimi nakuhakikishia Tundi Lissu machine nyingine

Imefight for 15yrs na serikali sasa imepata nafsi wewe subiri
 
Kwa wale waliobahatika kusoma gazeti la Mwanahalisi la leo kwenye kichwa cha habari nanukuu" Askofu huyu katumwa na nani?" mwaandishi kaandika kuwa kikwete alinukuliwa kwenye mikutano yake ya kampeni huko Singida kuwa " Ni bora Dr Slaa kuwa raisi kuliko Tundu lisu kuwa mbunge" hii hofu ya Muungwa kwa Tundu Lisu inatokana na nini?
Ndio maana wanahaha na ishu ya spika...wanajaribisha huyu, wanaona hafai, yule hafai!
Wameingizwa Kingi this time!
 
Kiraia ndiyo mbunge wa CCM aliyekuwa anagombea na Mh.Tundu lissu au wewe
mpambe wake ?
 
Kumuogopa Lisu inaweza kuwa inatokana na matatizo aliyoyapata Lisu wakati akitetea Wana Mara na ugomvi wao na wenye migodi ya dhahabu. Lisu inasemekana alikamatwa na kuteswa sana na serikali ya CCM.

Nina imani kuna mtu atakuja kuilezea hii kwa urefu maana hata mie huwa naisoma nusunusu.

Mama Lisu ni dada yake Tundu Lisu na si Mkewe. Muwe wa kweli.
 
Kama Chenge amesema anagombea nafasi ya uspika ili kuhakikisha hoja binafsi hazipati nafasi bungeni na kusabaisha majeraha kwa watu fulani, je upinzani chini ya Lissu, Halima, Mbowe na Zitto utaweza ku shine kama ilivyokuwa kwenye bunge lililopita?
 
Yeah, nimeona jina la Christina Lissu (Singida) kwenye orodha ya Viti Maalum Chadema. Hivi huyu ni mkewe Tundu Lissu?
 
haya lisu,tunamatumaini na wewe piga kazi mkuuuuu usirudi nyuma tumekuongezea nguvu upo na mr antivirus(sugu) anauhuru wa kusema na atasema, UKITAKA KUMJUWA SUGU NINANI SIKILIZA ANTIVIRUS)yupo kabweeeeeeeee,jamani ni uwakilishi mwema tunaouhitaji wenye tija na wenye kuleta mabadiliko ktk taifa letu

2015 zamu yangu nitagombea morogoro kwa tiketi ya chademaaaaaaaa
MAPINDUZIIIIIIIII DAIMAAAAAAA
 
Nashauri CHADEMA wamteue Tundu Lisu awe Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Wana:yield: JF Mnaionaje hii Imekaa vema!!!:yield::yield:
 
Kama Chenge amesema anagombea nafasi ya uspika ili kuhakikisha hoja binafsi hazipati nafasi bungeni na kusabaisha majeraha kwa watu fulani, je upinzani chini ya Lissu, Halima, Mbowe na Zitto utaweza ku shine kama ilivyokuwa kwenye bunge lililopita?
Huyu ni wa visasi
 
tatizo la wapinzani na Raia maskini ni kibaraka wa mafisadi (Zitto kabwe) Huyu akiwa kiongozi wa upinzani basi tumekwesha the guy amebadilika sana these days, amekuwa nothing but simply puppet
 
Nashauri CHADEMA wamteue Tundu Lisu awe Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Wana:yield: JF Mnaionaje hii Imekaa vema!!!:yield::yield:

Nadhani wanahofia ishu ya Uzoefu kwenye maswala ya bunge, zitto ne Mbowe wote walishakaa bungeni kwa miaka 5 ila kila mmoja wao ana matatizo yake mfano
Mbowe: wanasema ni mtu mwenye hasira sana kwa hiyo kuwaunganisha watu especially kambi ya upinzani itakuwa ngumu
Zitto: wanasema ana element za CCM ndani yake hii ni baada ya Mkuu wa Kaya kumteua kwenye ishu ya Madini pia ishu ya Dorwan imemchafua kwa kiasi fulani
 
Mbona CCM hawakemei kauli ile ya chenge? huko CCM naona wote ni "kambale" (kila mtu ana masharubu)
 
haya lisu,tunamatumaini na wewe piga kazi mkuuuuu usirudi nyuma tumekuongezea nguvu upo na mr antivirus(sugu) anauhuru wa kusema na atasema, UKITAKA KUMJUWA SUGU NINANI SIKILIZA ANTIVIRUS)yupo kabweeeeeeeee,jamani ni uwakilishi mwema tunaouhitaji wenye tija na wenye kuleta mabadiliko ktk taifa letu

2015 zamu yangu nitagombea morogoro kwa tiketi ya chademaaaaaaaa
MAPINDUZIIIIIIIII DAIMAAAAAAA

Hapo kwenye red umeharibu
 
Sina imani na kabwe tangu alipokubaliki kuongoza kamati ya bunge kwenye masuala ya nishati na madini huyu jamaa kashuka na siku ile aliposhupalia kuwa serikali inunue mitambo ya dowans nilimwona sijakubaliana naye.Napendekeza kambi ya upinzani iongozwe na Lisu au Mnyika hapo vipi??????????:yield::yield::yield:
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom