Kikwete ngoma nzito! Sitta, Nape wasubiri huruma yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ngoma nzito! Sitta, Nape wasubiri huruma yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 6, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Na Waandishi wetu

  BUNDI mharibifu anazidi kuinyemelea CCM hali inayotishia mgawanyiko mkubwa miongoni mwa makada na wanachama wa chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.

  Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana, CCM imejikuta kwenye malumbano mazito miongoni mwa makada wake, yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na mitazamo tofauti katika uendeshaji wa chama na utekelezaji wa misimamo inayotolewa na chama likiwemo suala la kujivua gamba.

  Katika hali inayozidisha tishio la mpasuko huo, wenyeviti wa mikoa wa chama hicho sasa wamemtega Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka amfukuze uanachama Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta.

  Kwenye kikao cha kutathimini uhai wa chama katika mikoa yao kilichofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam, wenyeviti hao walishauri, Sitta avuliwe uanachama wa CCM kwa madai kuwa amemtukana, Mwenyekiti wa Taifa, Rais Kikwete.

  Mbali na Sitta, baadhi ya wenyeviti hao walitaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, adhibitiwe kwa madai kuwa amekuwa akitoa matamshi ya upotoshaji yanayokwenda kinyume na maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

  Walidai kuwa Sitta alimtukana Rais Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kupitia Kipindi cha dakika 45, kinachorushwa na Kituo cha ITV, kutokana na hatua yake ya kulalamikia utaratibu uliopendekezwa na chama hicho kusimamisha mwanamke kugombea kiti cha Uspika wa Bunge, kwa madai kuwa uamuzi huo ulitokana na shinikizo la mafisadi lililolenga kumwengua kwenye nafasi hiyo.

  Ingawa baadhi ya wenyeviti walipinga ushauri huo, kauli hii ni mtihani mpya na mzito kwa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) Novemba 23, mwaka huu mjini Dodoma.

  Sitta aliwahi kunusurika kuvuliwa uanachama baada ya baadhi ya wajumbe wa NEC kumtuhumu kuwa anaendesha bunge kwa ajili ya kuwasaidia wapinzani na kukivuruga chama hicho.

  Hata hivyo, Mwenyekiti Rais Kikwete na baadhi ya wajumbe wengine walimnusuru na kuendelea na wadhifa wake wa Spika hadi alipomaliza kipindi chake cha miaka mitano ya kuliongoza Bunge la Tisa mwaka jana.

  Kama wenyeviti hawa ambao pia ni wajumbe wa NEC watashikilia msimamo wao wa kutaka Sitta ang'olewe, huenda kikao kijacho kitakuwa moto, hivyo busara za Mwenyekiti (Rais Kikwete) zitahitajika kupoza hali hiyo inayotishia mpasuko mkubwa.

  Hata hivyo, wadadisi wa mambo ya kisiasa ndani ya CCM wanaamini kuwa kikao hicho cha wenyeviti ni sehemu ya maandalizi ya msingi kupima joto halisi la kisiasa ndani ya chama kuanzia ngazi ya mikoa kabla ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) kitakachofuatiwa na NEC.

  Kuna taarifa kwamba, wengi wa wenyeviti wanaoshinikiza kung'olewa Sitta, wanaungwa mkono na kundi la watuhumiwa ufisadi ambao wamekuwa kama paka na panya na kundi linalojipambanua kuwa wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama hicho, linaloungwa mkono na mwanasiasa huyo.

  Hivi sasa kuna kila dalili kuwa CCM inapita katika wakati mgumu, kutokana na makundi hayo mawili yanayovutana chini huku kila moja likijaribu kuonyesha kuwa lina nguvu dhidi ya lingine.

  Kundi la watuhumiwa wa ufisadi sasa linadaiwa kutumia nguvu ya fedha na vikao vya chama kuhakikisha linawageuzia kibao cha kujivua gamba wanaowapinga ili watoshwe na chama hicho.

Kauli ya Msekwa
  Makamu Mwenyekiti wa CCM- Tanzania Bara, Pius Msekwa, akizungumza baada ya mapumziko ya mchana ya kikao hicho, alikiri malumbano hayo kutawala kikao hicho na kusema; "Tunachofanya hapa ni kupokea taarifa ya hali halisi ya kisiasa ndani ya chama kwa mikoa yote ya bara na visiwani. Hiki siyo kikao cha maamuzi".

  "Ni vikao vinavyofanyika mara kwa mara, lakini safari hii mimi ndiyo naongoza nikichukua nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais. Yeye yuko nje, sasa tumeona ni vema niwepo hapa kusimamia na kusikiliza taarifa za wenyeviti wa mikoa yote," aliongeza Msekwa.

  Kujivua Gamba
  Akizungumzia kujivua gamba, Msekwa alisema baadhi wanahoji kwa nini jambo hilo haliendi kwa kasi ili kulikamilisha na hatua hiyo iweze kufika pia ngazi ya chini.

  Makamu huyo alisema, ni kweli uamuzi huo wa kukisafisha chama ni wa NEC, lakini akatoa angalizo kwamba, "Tunachofanya sasa katika kutekeleza hili ni kitu kinachoitwa ‘Political Management.' Hatuwezi kufanya jambo hili kwa shinikizo".

  Alisema CCM ni chama cha siasa ambacho kinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zote za kiuongozi hivyo, hata utekelezaji wa maamuzi yake unapaswa kusukumwa kwa kanuni na misingi ya uongozi wa chama cha kisiasa na si vinginevyo.

  Mkutano wa NEC
  Mbali na suala la kujivua gamba inayotarajiwa kutawala mkutano NEC, mpasuko ndani ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) nao unatajwa kuteka kikao hicho.

  Kwa mujibu wa ratiba ya kikao hicho ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona jijini Dar es Salaam wiki hii na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa NEC, kikao hicho kitakaa baada ya kukamilika maandalizi yake ya msingi.

  Msimamo wa Ndejembi
  Katika hali inayoonesha kuzidi kufukuta moto ndani ya CCM, kada mkongwe wa CCM , Pancres Ndejembi, ameibuka na kusema kuwa rais ajaye anaweza kutokana na chama chochote ili mradi asiwe fisadi.

  Ndejembi alisema kwa sasa Watanzania wana macho na masikio, hivyo hawawezi kuchagua mtu ambaye ni fisadi katika nafasi ya urais na kukemea watu wanaoendeleza malumbano wakati muda muafaka haujafika.

  Ndejembi alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake Mtaa wa Kilimani, Dodoma ambapo alisema mtu atakayechaguliwa kuwa rais ni lazima awe mtu safi asiye na doa ndani ya chama na Serikali kwa ujumla.

  "Mabishano ndani ya chama hayafai, kwa kuwa ipo Katiba ya CCM ambayo inaelekeza jinsi watu wanavyoweza kutoa hoja. Kubishana katika vikao kuhusu urais ni ujinga unaotakiwa kukomeshwa mara moja,'' alisema na kuongeza;

  "Kama mabishano yao yanalenga urais basi watakuwa wamekosea kwa kuwa huu si wakati wa kujadili mambo hayo kwani Tanzania ina rais na anaitwa Jakaya Mrisho Kikwete sasa kwa nini waendeleze malumbano hayo katika kipindi hiki?''

  Alisema kuwa wanaobishana wamesahau kuwa Tanzania inaongozwa na mfumo wa siasa wa vyama vingi ambapo kila chama kitasimamisha mgombea wake na kuwa chama kitakachosimamisha mgombea safi ndicho kitakachoibuka na ushindi.

  Kada huyo aliwataka Watanzania kutulia kwa kuwa wakati utafika ambapo watatakiwa kuangalia nani anafaa kuwa rais wao lakini kipindi hiki ifahamike kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kutangaza habari za urais kwa kuwa bado kuna kipindi kirefu mbele yao.

  Kuhusu mvutano ndani ya CCM, alikemea na kusema kuwa tabia iliyojengeka kwa sasa ni mbaya kwa sababu watu wanalumbana bila ya kufuata utaratibu wa chama.

  Alisema watu wanaolumbana kwa sasa ndani ya chama wana ugomvi wao binafsi na wanaivuruga CCM.

  "Hebu watafute kitabu cha Mwalimu kiitwacho ‘Tujisahihishe' ambacho kiliandikwa kwa lengo maalumu la migogoro midogomidogo kama hiyo.''

  Ndejembi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma 1982-2007 na katika kipindi hicho alikuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mikoa wa chama hicho.

  Ole Millya na vijana
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya amekionya chama hicho na kueleza kuwa kama kinataka kuendelea kushika dola, kihakikishe kinakuwa karibu zaidi na kundi kubwa la vijana na kuwapa matumaini.

  Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi Jumapili jana, Millya alisema chama chochote cha siasa hakiwezi kukamata dola kama hakiungwi mkono na vijana ambao ndio wengi.

  "UVCCM Arusha tunampongeza sana mlezi wetu Stephen Wassira akishirikiana na katibu wetu UVCCM, Martin Shigella kwa kufanikisha muafaka Arusha, tunaamini sasa tutasonga mbele kusaidia chama," alisema Millya.

  Hata hivyo, alisema angalizo ambalo analitoa sasa kwa CCM ni kuwasikiliza vijana na kuwa nao karibu ili iendelee kukamata dola.

  Akizungumzia siasa za makundi ndani ya CCM, Millya alisema ni tatizo kubwa ndani ya chama hicho na kwamba linatokana na siasa za majitaka na ubinafsi.

  Sir Kahama
  Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir George Kahama (82) naye ameishauri CCM na kuitaka kutambua kuwa ili nchi itawalike lazima pawepo demokrasia ya kweli kinyume na hapo, umma utachoka na kuingia mitaani kuleta vurugu.

  Sir Kahama alitoa kauli hiyo hivi karibuni kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake Dar es Salaam, kuhusu mustakabali wa kisiasa maendeleo ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

  chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Fang

  Fang Content Manager Staff Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 489
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  That is evident and the problem more lies with the fact that the groups are in sub-groups of which may be in agreement/in communication with the other side's group and sub-group. Either way they are doomed. A Tangled web if any.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  CCM imeshapitwa na wakati bora uje uchaguzi ujao kipatikane chama kipya na viongozi wapya wanaopenda maendeleo ya nchi yetu Change We Can........
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  ee mungu mwenyezi inusuru CCM na hili pigo
   
 5. Fang

  Fang Content Manager Staff Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 489
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  That is exactly what i mean if you got me good.
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa ccm, tiba yoyote sasa haiwezi kuleta uponyaji bali unafuu tu. Chama hiki kinatakiwa kiwekwe pembeni ili kijipange upya wakati cdm wakionyesha namna ya kuongoza nchi.
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mimi konachoniudhi dhani ya CCM ni kushindwa kusimamia baadhi ya mambo ambayo wameutangazia umma na umma kujenga matumini fulani! Umeme, kujivua gamba, n.k
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Achana nayo!
   
 9. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  0diggsdigg

  [​IMG] Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete

  SITTA, NAPE WASUBIRI HURUMA YAKE
  Na Waandishi wetu
  BUNDI mharibifu anazidi kuinyemelea CCM hali inayotishia mgawanyiko mkubwa miongoni mwa makada na wanachama wa chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana, CCM imejikuta kwenye malumbano mazito miongoni mwa makada wake, yanayochangiwa kwa kiasi kikubwa na mitazamo tofauti katika uendeshaji wa chama na utekelezaji wa misimamo inayotolewa na chama likiwemo suala la kujivua gamba.

  Katika hali inayozidisha tishio la mpasuko huo, wenyeviti wa mikoa wa chama hicho sasa wamemtega Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka amfukuze uanachama Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta.

  Kwenye kikao cha kutathimini uhai wa chama katika mikoa yao kilichofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam, wenyeviti hao walishauri, Sitta avuliwe uanachama wa CCM kwa madai kuwa amemtukana, Mwenyekiti wa Taifa, Rais Kikwete.

  Mbali na Sitta, baadhi ya wenyeviti hao walitaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, adhibitiwe kwa madai kuwa amekuwa akitoa matamshi ya upotoshaji yanayokwenda kinyume na maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

  Walidai kuwa Sitta alimtukana Rais Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kupitia Kipindi cha dakika 45, kinachorushwa na Kituo cha ITV, kutokana na hatua yake ya kulalamikia utaratibu uliopendekezwa na chama hicho kusimamisha mwanamke kugombea kiti cha Uspika wa Bunge, kwa madai kuwa uamuzi huo ulitokana na shinikizo la mafisadi lililolenga kumwengua kwenye nafasi hiyo.

  Ingawa baadhi ya wenyeviti walipinga ushauri huo, kauli hii ni mtihani mpya na mzito kwa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) Novemba 23, mwaka huu mjini Dodoma.Sitta aliwahi kunusurika kuvuliwa uanachama baada ya baadhi ya wajumbe wa NEC kumtuhumu kuwa anaendesha bunge kwa ajili ya kuwasaidia wapinzani na kukivuruga chama hicho.

  Hata hivyo, Mwenyekiti Rais Kikwete na baadhi ya wajumbe wengine walimnusuru na kuendelea na wadhifa wake wa Spika hadi alipomaliza kipindi chake cha miaka mitano ya kuliongoza Bunge la Tisa mwaka jana.

  Kama wenyeviti hawa ambao pia ni wajumbe wa NEC watashikilia msimamo wao wa kutaka Sitta ang'olewe, huenda kikao kijacho kitakuwa moto, hivyo busara za Mwenyekiti (Rais Kikwete) zitahitajika kupoza hali hiyo inayotishia mpasuko mkubwa.

  Hata hivyo, wadadisi wa mambo ya kisiasa ndani ya CCM wanaamini kuwa kikao hicho cha wenyeviti ni sehemu ya maandalizi ya msingi kupima joto halisi la kisiasa ndani ya chama kuanzia ngazi ya mikoa kabla ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) kitakachofuatiwa na NEC.
  Kuna taarifa kwamba, wengi wa wenyeviti wanaoshinikiza kung'olewa Sitta, wanaungwa mkono na kundi la watuhumiwa ufisadi ambao wamekuwa kama paka na panya na kundi linalojipambanua kuwa wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama hicho, linaloungwa mkono na mwanasiasa huyo.

  Hivi sasa kuna kila dalili kuwa CCM inapita katika wakati mgumu, kutokana na makundi hayo mawili yanayovutana chini huku kila moja likijaribu kuonyesha kuwa lina nguvu dhidi ya lingine.

  Kundi la watuhumiwa wa ufisadi sasa linadaiwa kutumia nguvu ya fedha na vikao vya chama kuhakikisha linawageuzia kibao cha kujivua gamba wanaowapinga ili watoshwe na chama hicho.

Kauli ya Msekwa
  Makamu Mwenyekiti wa CCM- Tanzania Bara, Pius Msekwa, akizungumza baada ya mapumziko ya mchana ya kikao hicho, alikiri malumbano hayo kutawala kikao hicho na kusema; "Tunachofanya hapa ni kupokea taarifa ya hali halisi ya kisiasa ndani ya chama kwa mikoa yote ya bara na visiwani. Hiki siyo kikao cha maamuzi".

  "Ni vikao vinavyofanyika mara kwa mara, lakini safari hii mimi ndiyo naongoza nikichukua nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais. Yeye yuko nje, sasa tumeona ni vema niwepo hapa kusimamia na kusikiliza taarifa za wenyeviti wa mikoa yote," aliongeza Msekwa.

  Kujivua Gamba
  Akizungumzia kujivua gamba, Msekwa alisema baadhi wanahoji kwa nini jambo hilo haliendi kwa kasi ili kulikamilisha na hatua hiyo iweze kufika pia ngazi ya chini.

  Makamu huyo alisema, ni kweli uamuzi huo wa kukisafisha chama ni wa NEC, lakini akatoa angalizo kwamba, "Tunachofanya sasa katika kutekeleza hili ni kitu kinachoitwa ‘Political Management.’ Hatuwezi kufanya jambo hili kwa shinikizo".

  Alisema CCM ni chama cha siasa ambacho kinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zote za kiuongozi hivyo, hata utekelezaji wa maamuzi yake unapaswa kusukumwa kwa kanuni na misingi ya uongozi wa chama cha kisiasa na si vinginevyo.

  Mkutano wa NEC
  Mbali na suala la kujivua gamba inayotarajiwa kutawala mkutano NEC, mpasuko ndani ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) nao unatajwa kuteka kikao hicho.

  Kwa mujibu wa ratiba ya kikao hicho ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona jijini Dar es Salaam wiki hii na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa NEC, kikao hicho kitakaa baada ya kukamilika maandalizi yake ya msingi.

  Msimamo wa Ndejembi
  Katika hali inayoonesha kuzidi kufukuta moto ndani ya CCM, kada mkongwe wa CCM , Pancres Ndejembi, ameibuka na kusema kuwa rais ajaye anaweza kutokana na chama chochote ili mradi asiwe fisadi.

  Ndejembi alisema kwa sasa Watanzania wana macho na masikio, hivyo hawawezi kuchagua mtu ambaye ni fisadi katika nafasi ya urais na kukemea watu wanaoendeleza malumbano wakati muda muafaka haujafika.
  Ndejembi alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake Mtaa wa Kilimani, Dodoma ambapo alisema mtu atakayechaguliwa kuwa rais ni lazima awe mtu safi asiye na doa ndani ya chama na Serikali kwa ujumla.
  “Mabishano ndani ya chama hayafai, kwa kuwa ipo Katiba ya CCM ambayo inaelekeza jinsi watu wanavyoweza kutoa hoja. Kubishana katika vikao kuhusu urais ni ujinga unaotakiwa kukomeshwa mara moja,’’ alisema na kuongeza;
  “Kama mabishano yao yanalenga urais basi watakuwa wamekosea kwa kuwa huu si wakati wa kujadili mambo hayo kwani Tanzania ina rais na anaitwa Jakaya Mrisho Kikwete sasa kwa nini waendeleze malumbano hayo katika kipindi hiki?’’
  Alisema kuwa wanaobishana wamesahau kuwa Tanzania inaongozwa na mfumo wa siasa wa vyama vingi ambapo kila chama kitasimamisha mgombea wake na kuwa chama kitakachosimamisha mgombea safi ndicho kitakachoibuka na ushindi.
  Kada huyo aliwataka Watanzania kutulia kwa kuwa wakati utafika ambapo watatakiwa kuangalia nani anafaa kuwa rais wao lakini kipindi hiki ifahamike kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kutangaza habari za urais kwa kuwa bado kuna kipindi kirefu mbele yao.
  Kuhusu mvutano ndani ya CCM, alikemea na kusema kuwa tabia iliyojengeka kwa sasa ni mbaya kwa sababu watu wanalumbana bila ya kufuata utaratibu wa chama.
  Alisema watu wanaolumbana kwa sasa ndani ya chama wana ugomvi wao binafsi na wanaivuruga CCM.
  “Hebu watafute kitabu cha Mwalimu kiitwacho ‘Tujisahihishe’ ambacho kiliandikwa kwa lengo maalumu la migogoro midogomidogo kama hiyo.’’
  Ndejembi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma 1982-2007 na katika kipindi hicho alikuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mikoa wa chama hicho.

  Ole Millya na vijana
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya amekionya chama hicho na kueleza kuwa kama kinataka kuendelea kushika dola, kihakikishe kinakuwa karibu zaidi na kundi kubwa la vijana na kuwapa matumaini.

  Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi Jumapili jana, Millya alisema chama chochote cha siasa hakiwezi kukamata dola kama hakiungwi mkono na vijana ambao ndio wengi.

  “UVCCM Arusha tunampongeza sana mlezi wetu Stephen Wassira akishirikiana na katibu wetu UVCCM, Martin Shigella kwa kufanikisha muafaka Arusha, tunaamini sasa tutasonga mbele kusaidia chama,” alisema Millya.

  Hata hivyo, alisema angalizo ambalo analitoa sasa kwa CCM ni kuwasikiliza vijana na kuwa nao karibu ili iendelee kukamata dola.

  Akizungumzia siasa za makundi ndani ya CCM, Millya alisema ni tatizo kubwa ndani ya chama hicho na kwamba linatokana na siasa za majitaka na ubinafsi.

  Sir Kahama
  Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir George Kahama (82) naye ameishauri CCM na kuitaka kutambua kuwa ili nchi itawalike lazima pawepo demokrasia ya kweli kinyume na hapo, umma utachoka na kuingia mitaani kuleta vurugu.

  Sir Kahama alitoa kauli hiyo hivi karibuni kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake Dar es Salaam, kuhusu mustakabali wa kisiasa maendeleo ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Kila mtu anatafuta pa kujifichia when things do not move
   
 11. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu hiki kitu kinanichanganya, wenyeviti wanasema Nape hanapotosha umma kuhusu dhana ya kujivua gamba?
  Sasa ni nani mkweli? mbona wanapingana wenyewe kwa wenyewe wakati wote waliudhulia kikao cha NEC kilichopita.!!
   
Loading...