Kikwete ndio rahisi pekee anayeweza kuongoza tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ndio rahisi pekee anayeweza kuongoza tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salas, Jul 21, 2011.

 1. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watanzania tumegubikwa na tamaduni ya kukurupuka na kuendeshwa na matukio siku zote, rais ambaye ni mtulivu ambaye anajua kupanga ni kuchagua huwa asilani hana papara rais amekuwa akitumia muda mwingi kusafiri huku na huko kutafuta ni jinsi gani ataweza kusaidia changamoto zinazowakabili watu wake. Tusiwe tunafikiri kwa kutumia ubongo na sio ufahamu kama vile tunavyo wakshifu wengine kuwa wanatumia matumbo kufikiri tukiwa tuna maanisha wanafikiri kwa njaa.

  Rais Kikwete ameonekana akiwa bega kwa bega na watu wake katika mambo mbalimbali yanayokabili hali ya maisha ya kila siku, alikuwepo mkapa shutuma nyingi zilielekezwa juu yake ni mbabe, sio msikivu, dictator nakadhalika lakini leo hii wale watu hao kwa fikra zilezile wanadiriki kumkashifu muheshimiwa rais kwa tuhuma nzito na kubwa kabisa lakini tunajua agenda zao, wanatumiwa na uma wa wezi na wenye uchu wa madaraka.

  Tanzania ni kisiwa cha Amani na Utulivu, kama unabisha leo hii njoo burundi uone nini kinachoendelea, Asilani tutalinda amani na utulivu wa nchi hii kwa nguvu hata kwa tone la mwisho la damu kama itatupasa kufanya hivyo.

  Tumekuwa wepesi wa kulaumu na kuendeshwa na matukio haya swala la UMEME, je unafikiri kama raisi akitatua tatizo la umeme matatizo mengine yatakuwa yameeisha kwa mfano, vifo vya kinamama na watoto, elimu, maji, masoko ya biashara kwa wakulima wetu, ajira kwa watu wetu tunakurupuka kwa mihemuko ya kisiasa.

  Fikra sahihi huja pale mwanadamu, anapotumia na kufikiri nnje ya boksi kwa kuangalia na mbinu nyingine mbadala ambazo zinaweza zikasaidia kutatua matatizo.

  Raisi hafurahi kuona kuwa nchi inakuwa gizani, huitaji kuwa na degree ya chuo kikuu kudadaviua hili, la hasha hali ya uchumi wetu ndio inayosababisha yote haya yanayojitokeza kwa sasa. Rais amekuwa akitumia muda mwingi kutumia Muda wake kuwaza kuhusu mtoto yule anayekufa kwa kansa tandahimba, mzee yule anayekosa chakula leo masieda mbulu, na mama yule aliyeko mwandiga kigoma, ambae anajifungua akiwa anamsubiri nesi ambaye yuko kwenye foleni nmb kupokea mshahara wake.

  Rais nasema ndio anayefaa kuongoza nchi hii kwasababu anatumia uelewa wa wananchi wake kuzungumzia hali ya maisha, kwa mfano ni wangapi mlioku humu kwenye jamii forum mnao amini kukua kwa uchumi ni hata kuwa na gari, kwani uongo mwaka themanini ni wangapi wetu waliokuwa wanamiliki magari, leo hii ooh magari sio kukuwa kwa uchumi rais hafikirii angetatua tatizo la foleni, Je rais kama angeshauriana na Magufuli na kusema parking mjini kwa siku ni shilling elfu ishirini si mngeandamana uchi nyie mnaokuwa wepesi kulalamika??? Faini iliposomwa laki tatu badala ya hamsini mlipanua midomo mpaka kimeo kikaonekana.

  Rais kikwete ndio anayeweza kuongoza nchi hii, kuna baadhi ya wananchi wanao ona umeme ni anasa NDIO pia sisi tunaongozwa na huyo huyo mnao muona hafai kwetu tatizo sio umeme, HATUNA MAJI je kila mtu akianza kumuambia rais arudi safarini alipoenda KUHEMEA kwa ajili ya watu wake je mambo mengine yatatatulika??? Kwani ni asilimia ngapi ya wananchi wenye access ya umeme???? Hapa watu wanatumia kila nafasi kupayuka hasa kwa miitikio ya kisiasa, Angekuwa Dr Slaa rais angefunga vinu vya nuclear vizalishe umeme au angeangalia juu mwenyezi Mungu alete mvua????

  Kikwete wewe ndio unaofaaa sisi asilimia 80% tuishio vijijini wewe ndio rais wetu, tunakutambua na kukuunga mkono na yote ufanyayo ni kwa ajili yetu, rais haendi ulaya kufanya shopping ya chakula ndani, wala nguo za kuvaa anenda kwa lengo moja tu la kutafuta jinsi ya kutimiza AHADI ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Rais kikwete ndio anayefaa kuongoza Tanzania, Mungu mpe afya na hekima ya kuendelea kutatua matatizo ya watu wako, ningekuwa na namba ningekutumia sms ya kukupongeza.

  MAISHA BORA HAYAJI KWA KULALA, MAJUNGU NA MAANDAMANO AMKA FANYA KAZI TANZANIA ITAJENGWA NA MWANANCHI MMOJA MMOJA:
   
 2. k

  kiloni JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unatakiwa uwe na roho ya paka kuleta uchafu kama huu hapa! ngoja nikatapike nasikia kichefuchefu!!!!!!!!!!!
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo matatizo ya umeme kama alivyosema BBC ni ukame ndio ameendea maji South Africa au kwenye mikataba aliyo-sign na Zuma itasaidia kujaza maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme? Hivi ameenda kuhemia au kuomba? Usiongelee Dr. Slaa aongelea huyo failure bwana. Mafanikio ya Dr. Slaa kama Raid huwezi kuyafahamu mpaka awe Rais!!
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Quote from Salas....

  Asante. Sasa nimekuelewa....
   
 5. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa maana hiyo kwani hujui kuwa sisi tunatumia HEP ( Hydro electric power) sasa unategemea nini kama MVUA haijanyesha.......yeye ndio atakae jaza mabwawa tena naomba nieleweke kuwa RAIS HAJAENDA SOUTH KWA SABABU YA UMEME ana shughuli zake nyingine za kimaendeleo tu. Unajua ukiwa victim of negativity kulielewa hili ni kazi, unajua ukiwa umevaa miwani ya blue kila kitu ni blue wewe ni muumini wa DR Slaa unaamini hivyo endelea kuamini hivyo eti tumpe nnchi kwa majaribio
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa! Kumbe sio RAISI ni RAHISI safi sanaaaa!
   
 7. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Thio kikwete thema daktari ndio utheme kikw....
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maisha bora yanakuja kwa kulala ni sera ya ccm, majungu ni sera ya ccm na maandamano yamefanikisha kuelimisha watu na kuifanya serikali iamke. Wanaofanya kazi ni wengi lakini hawapati ujira wa haki. Tanzania itajengwa na mwananchi mmoja mmoja na kuliwa na viongozi wateule wa ccm na wafadhili wao kwenye mkakati wa UFISADI.
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako umejitia upofu mwenyewe, sasa sijui tukusaidiaje ili uone ? kama unasikia kichefuchefu na unataka kutapika hizo ni dalili za mimba hizo, sijui sisi tukusaidiaje na umeyataka mwenyewe
   
 10. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kiloni asamehewe bure na tumuombee hilo pepo lililompanda limtoke. Nafikiri anatambua vitu vichache sana kwa vile akili siyo yake
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kuna aina nyingi za upofu na vipofu wengi hawaelewi kama ni vipofu.. ahahahaha GB kanawe uso baharini mara tatu kutwa inasaidia...
   
Loading...