Kikwete, Nchimbi hata hili la kumuondoa Daily News Kaimu Mhariri asiye na Mkataba pia limewashinda, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, Nchimbi hata hili la kumuondoa Daily News Kaimu Mhariri asiye na Mkataba pia limewashinda,

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jasla, Apr 4, 2012.

 1. J

  Jasla New Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za uhakika zinathibitisha kuwa Kaimu Mhariri wa Kampuni ya
  magazeti ya serikali yaani Tanzania Standard Newspapers Ltd,
  inayochapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Spoti
  Leo amekuwa madarakani hivi sasa kwa takribani miaka miwili bila ya
  kuwa na mkataba unamwezesha kuwepo madarakani kwani mkataba wake wa
  cheo cha msingi ambacho ni Naibu Mhariri Mtendaji ulishakwisha toka
  mwaka 2009.

  Katika kile kinachotia mashaka ni kwamba baada ya kwisha kwa mkataba
  wake Mheshimiwa hakuchukua hatua zozote za kuomba mkataba mpya kwa
  kuwasilisha maombi yake kwenye Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni hiyo
  nguli ya magazeti. Kwa kuwa cheo chake cha msing kama kilivyotajwa
  hapo juu kinahusiana na mamlaka ya Bodi juu ya kumpatia mkataba mpya
  au laa, lakini cha kusikitisha ni kwamba hakuweza kuandika barua ya
  maombi ya mkataba mpya kwa cheo chake cha msingi alichoajiriwa kwenye
  kampuni hiyo ni cha mkataba wa miaka mitatu na kuongezwa muda kadri
  Bodi itakavyoamua.

  La kushangaza ni kwamba pamoja na kutokuwa na mkataba mheshimiwa huyo
  ameendelea kukalia kiti cha Kaimu Mhariri wa Kampuni hiyo kwa
  takribani miaka miwili sasa huku akijiidhinishia malipo ya mshahara
  mbayo hastahiki kwa kuwa hana mkataba na pia kuingiza kampuni hiyo
  kwenye mbalimbali bila ya kuwa na nguvu za kisheria zinazotokana na
  mkataba.

  Mheshimiwa haonekani kuwa na wasiwasi wowote juu ya hili, na hilo hasa
  ni jambo linalonipa taabu kuamini kama Tanzania yetu iliyojaaliwa
  rasilimali mbalimbali na watu wapole na wenye woga juu ya kupigania
  haki zao inaweza ikaendelea.

  Nilidhani Mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr.
  Jakaya M. Kikwete pamoja na waziri wake wa Habari Utamaduni na michezo
  Dr. Emmanuel Nchimbi wangeweza kulisawazisha suala hili kabla halijawa
  sugu na kuleta madhara zaidi kwa taasisi hiyo ya umma. Lakini mpaka
  sasa hakuna lolote la maana lilofanyika huku Mheshimiwa anayekalia
  kiti bila mkataba akionekana kuendelea na mambo yake bila shaka
  yeyote.

  Hapa kuna haja ya kujiuliza mara mbili mbili kama mambo haya madogo
  yametushinda kutolea maamuzi vipi kuhusu mambo mazito yanayoikabili
  nchi hii.

  Wazalendo mnaliona hili.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Jasia, ucha majungu, na kuleta zengwe la kupiga fitna ili jamaa ang'olewe!.

  Naamini unajua fika sababu zilizopelekea mpaka sasa hajathibitishwa!.

  Hivi kama umepewa mkataba wa muda, ule muda ukiisha ni jee ni jukumu la wewekuomba mkataba mpya au mwenye kazi yake kukumbusha mkataba wako umeisha asante kwa huduma yako, fungasha nenda zako!.

  Ukiona hujaambiwa nenda, ina maana huduma yako bado inahitajika!. Huyu mhusika unayetaka kumpiga zengwe, bado anahitajika ndio maana bado yupo!. Kwani mkataba wa ajira wa Tido ulipoisha nini kilifuatia!. Ukiwa huhitajiki unaonyeshwa njia ya kitokea!. Ukijiona hujafunguliwa mlango wa kutokea unaendelea kubaki mpaka muda wako wa kuonyeshwa njia ukifika, mlango wa kutokea utauoana uu wazi!.
  Mwache jamaa apige kazi!.

  Pasco.
   
 3. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwanza nikupe pole ndugu yangu kana hujui hao jamaa unaotaka wamuondoe kaimu mkurugenzi ni marafiki sana. La pili wakimuondoa hapo wanahisi hakuna wa kusimamia kuandika habari za si-ha-sa hasa huyo waziri wa habari.
   
 4. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nakupenda Pasco kwa ushujaa wako wa kuwatetea watendaji waovu bila woga wala haya! Big up sana kaka!!!!!!
   
 5. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Magaba Magamba wera wera sisi tunasonga
  Mbele wakishtuka tunamadiwani na wabunge
  Nchi zima!!!waendelee kukalia mauzembe
  Yao huku wakiteteana.
   
Loading...