Kikwete nchi imekushinda achia ngazi

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Wana JF na Watanzania wenzangu nadiriki kusema kuwa Rais aliyeko madarakani ameshindwa kuiongoza JMT na kwa hivyo anapaswa ajiuzulu au aondolewe kwa Nguvu ya Bunge yaani IMPEACHMENT.

Nimeamua kusema hivi kwasababu, mosi ni kwamba tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana 2010 umalizike Kikwete ameonyesha kuwa mkimya sana na mtu asiye na furaha kama vile hakushinda Urais. Hii inaonyesha kuwa ushindi wake ulikuwa ni wa mashaka sana.

Lakini la pili ambalo mimi naliona ni mhimu sana ni kuwa Kikwete kwa sasa ameamua KUKAA KIMYA AU KUNYAMAZA KABISA KANA KWAMBA HAYUPO NCHINI. Kuna matukio makuu na muhimu sana ambayo Kikwete kama Rais,Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu alitakiwa kutoa mwelekeo na msimamo wa Serikali yake ya CCM. Nitayataja matukio haya:

  1. Hukumu ya ICC dhidi ya TANESCO kuhusu kuwalipa DOWANS mabilioni ya shilingi.Kwanza zilikuwa 185b/- na sasa zimepungua mpaka 97b/- Katika swala tete kama hili ambalo linagusa uchumi wa Nchi yetu Rais alitakiwa alitolee ufafanuzi tena wa kina usiotiliwa shaka. Lakini kinyume chake Kiwete amenyamaza kimya kama vile hayuko amewaachia Waziri wake na Mwanasheria wa Serikali.
  2. Tangazo la EWURA/TANESCO kuhusu ongezeko la gharama za umeme kwa 18% huku Kiwete akiwa kimya kama vile hayupo. Amewaachia EWURA,Ngeleja na Tanesco walumbane na wananchi huku maandamano ya nchi nzima kupinga ongezeko la umeme yakiwa mbioni.
  3. Yeye akiwa Mwenyekiti wa CCM wa Taifa na Rais wa chama kilichoko madarakani alitakiwa awe ametoa mwelekeo na hatimaye kumaliza mgogoro wa Uchaguzi wa Meya Jiji la Arusha. Lakini kinyume chake amewaachia Katibu wake kihiyo Mkamba akipayuka kama mlevi akisaidiana na kichaa Mary Chitanda katika kuongeza Petrol kwenye moto unaowaka na hatimaye tukashuhudia mauaji ya watu zaidi ya 3.
  4. Tukio la tarehe 5 Januari,2011 lilikuwa ni tukio lilogusa kila Mtanzania mpenda amani,upendo na mshikamano wa Taifa letu. Kwamba watu zaidi ya 3 waliuwawa kwa risasi za moto kwa uzembe wa Polisi waliokuwa wamechochewa na Viongozi wa CCM. Baada ya maandamano hatimaye kufuatiwa na vifo,nilitegemea Kiwete angelipata maumivu, huzuni na hatimaye kuguswa na simanzi kwa damu ya Watanzania iliyomwagika pasipo na hatia. Na kwamba yeye kama Mkuuwa nchi angelikuwa tayari ameshatoa tamko rasmi kuhusiana na kadhia hii na hatimaye kupelekea kumalizika kwa mgogoro wa Arusha pasi kujali itikadi za kichama wala kidini.
Kwa matukio haya makuu 4 yanayogusa maisha ya Wa-tz moja kwa moja ilhali mkuu wa kaya amenyamaza mimi inanipa wasiwasi sana. Hii inathibitisha kuwa Kiwete nchi imemshinda, ameshindwa kutoa maamuzi kama Rais. Anaonekana ni Rais asiye na maamuzi na haya 4 ameshindwa aanzie wapi.

Hivi Rais unashindwaje kwa mfano kuzuia malipo hewa ya Shs.97b/- kwenda Kampuni hewa ya DOWANS ambayo wewe mwenyewe iliigharimu serikali yako mpaka ukavunja Baraza la Mawaziri???

Hivi kama Rais unashindwaje kuwa wajibisha viongozi wako waandamizi kwa uzembe waliosababisha wa kupotea roho za watu? Kwa mfano Kiwete ameshindwa nini kuwatimua kazi Nahodha,Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Mwema akiwemo Makamba na Chitanda kwa kusabanisha mgogoro wa Umeya Arusha na hatimaye kupelekea Mauaji??

Hivi kama Rais unashindwaje kutoa amri kupeleka mwakilishi wa Serikali kwenye mazishi ya watu waliouwawa kwa uzembe wa Polisi??Unaona aibu gani wakti wewe hukusababisha? Unless kama Kiwete anataka kutuaminisha kuwa yeye ni sehemu ya mgogoro na mauaji hayo!

Tukio la jana kwenye mazishi ya watu waliouawawa na Polisi limeiabisha Serikali ya Kikwete kwa sana. Moja ni kwamba CCM na serikali yake wameonekana kwamba walifurahia vifo hivyo na Pili wameonyesha kuwa wanachuki kwa upinzani kwa vile walikufa ni wafuasi wa Chadema. Hii ni hatari sana kwa CCM hasa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa mwendo huu CCM mmejimaliza na kujikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.
 
Bro ngoja hali iendelee hivi watu wazidi kuichukia ccm ili 2015 chadema ichukue nchi kiulani
 
mkuu... naipata point yako... lakini wale wa ku unga unga si wata perish before 2015...tuwasaidieje... ? something need to be done before 1015 as an immediate rescue mechanism
 
kuna wakati huwa nakaa na kufukiri njia ya mkato ili atoke pale na apotee kabisa........hata ikibidi turudie uchaguzi........lazima ifanyike namna ili yuhu atoke pale.......hivi hivi hatoki.......ataendelea kusogeza miwani tu akiwa pale........
 
Wana JF na Watanzania wenzangu nadiriki kusema kuwa Rais aliyeko madarakani ameshindwa kuiongoza JMT na kwa hivyo anapaswa ajiuzulu au aondolewe kwa Nguvu ya Bunge yaani IMPEACHMENT.

Nimeamua kusema hivi kwasababu, mosi ni kwamba tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana 2010 umalizike Kikwete ameonyesha kuwa mkimya sana na mtu asiye na furaha kama vile hakushinda Urais. Hii inaonyesha kuwa ushindi wake ulikuwa ni wa mashaka sana.

Lakini la pili ambalo mimi naliona ni mhimu sana ni kuwa Kikwete kwa sasa ameamua KUKAA KIMYA AU KUNYAMAZA KABISA KANA KWAMBA HAYUPO NCHINI. Kuna matukio makuu na muhimu sana ambayo Kikwete kama Rais,Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu alitakiwa kutoa mwelekeo na msimamo wa Serikali yake ya CCM. Nitayataja matukio haya:

  1. Hukumu ya ICC dhidi ya TANESCO kuhusu kuwalipa DOWANS mabilioni ya shilingi.Kwanza zilikuwa 185b/- na sasa zimepungua mpaka 97b/- Katika swala tete kama hili ambalo linagusa uchumi wa Nchi yetu Rais alitakiwa alitolee ufafanuzi tena wa kina usiotiliwa shaka. Lakini kinyume chake Kiwete amenyamaza kimya kama vile hayuko amewaachia Waziri wake na Mwanasheria wa Serikali.
  2. Tangazo la EWURA/TANESCO kuhusu ongezeko la gharama za umeme kwa 18% huku Kiwete akiwa kimya kama vile hayupo. Amewaachia EWURA,Ngeleja na Tanesco walumbane na wananchi huku maandamano ya nchi nzima kupinga ongezeko la umeme yakiwa mbioni.
  3. Yeye akiwa Mwenyekiti wa CCM wa Taifa na Rais wa chama kilichoko madarakani alitakiwa awe ametoa mwelekeo na hatimaye kumaliza mgogoro wa Uchaguzi wa Meya Jiji la Arusha. Lakini kinyume chake amewaachia Katibu wake kihiyo Mkamba akipayuka kama mlevi akisaidiana na kichaa Mary Chitanda katika kuongeza Petrol kwenye moto unaowaka na hatimaye tukashuhudia mauaji ya watu zaidi ya 3.
  4. Tukio la tarehe 5 Januari,2011 lilikuwa ni tukio lilogusa kila Mtanzania mpenda amani,upendo na mshikamano wa Taifa letu. Kwamba watu zaidi ya 3 waliuwawa kwa risasi za moto kwa uzembe wa Polisi waliokuwa wamechochewa na Viongozi wa CCM. Baada ya maandamano hatimaye kufuatiwa na vifo,nilitegemea Kiwete angelipata maumivu, huzuni na hatimaye kuguswa na simanzi kwa damu ya Watanzania iliyomwagika pasipo na hatia. Na kwamba yeye kama Mkuuwa nchi angelikuwa tayari ameshatoa tamko rasmi kuhusiana na kadhia hii na hatimaye kupelekea kumalizika kwa mgogoro wa Arusha pasi kujali itikadi za kichama wala kidini.
Kwa matukio haya makuu 4 yanayogusa maisha ya Wa-tz moja kwa moja ilhali mkuu wa kaya amenyamaza mimi inanipa wasiwasi sana. Hii inathibitisha kuwa Kiwete nchi imemshinda, ameshindwa kutoa maamuzi kama Rais. Anaonekana ni Rais asiye na maamuzi na haya 4 ameshindwa aanzie wapi.

Hivi Rais unashindwaje kwa mfano kuzuia malipo hewa ya Shs.97b/- kwenda Kampuni hewa ya DOWANS ambayo wewe mwenyewe iliigharimu serikali yako mpaka ukavunja Baraza la Mawaziri???

Hivi kama Rais unashindwaje kuwa wajibisha viongozi wako waandamizi kwa uzembe waliosababisha wa kupotea roho za watu? Kwa mfano Kiwete ameshindwa nini kuwatimua kazi Nahodha,Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Mwema akiwemo Makamba na Chitanda kwa kusabanisha mgogoro wa Umeya Arusha na hatimaye kupelekea Mauaji??

Hivi kama Rais unashindwaje kutoa amri kupeleka mwakilishi wa Serikali kwenye mazishi ya watu waliouwawa kwa uzembe wa Polisi??Unaona aibu gani wakti wewe hukusababisha? Unless kama Kiwete anataka kutuaminisha kuwa yeye ni sehemu ya mgogoro na mauaji hayo!

Tukio la jana kwenye mazishi ya watu waliouawawa na Polisi limeiabisha Serikali ya Kikwete kwa sana. Moja ni kwamba CCM na serikali yake wameonekana kwamba walifurahia vifo hivyo na Pili wameonyesha kuwa wanachuki kwa upinzani kwa vile walikufa ni wafuasi wa Chadema. Hii ni hatari sana kwa CCM hasa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kwa mwendo huu CCM mmejimaliza na kujikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.
mkuu hiyo ya pili alishajibu kwenye mwaka mpya speech kuwa isiingizwe kisiasa, na gharama za maisha na uendeshaji zimepanda, cha ajabu hakueleza yeye atafanyeje kwa wafanyakazi wa serikali ili waendane na upandaji wa gharama. HAPO NDO NAONA MAKOSA YALIKUWEPO BCS GHARAMA SI KWA KWA TANESCO TUU NI PAKA MIFUKONI MWA WANANCHI WAKE.
 
''Nasema hivi utulipe Dowans...ama sivyo usitulaumu''

pmo.jpg
 
Mganga wake, Mohamed Mbega kutoka Bumbuli amemwambia aongoze nchi kwa staili hiyo!
 
Nmesoma coment, nashauri Magu aongeze mbinyo ili hawa watz wajifunze kitu.

Kumbe suala la Dowans lipo toka 2011 ila kwa sasa hawa nyumbu wanaona kina ruge wanaonewa
 
Back
Top Bottom