Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,186
- 56
Mheshimiwa Kikwete, hiyo nchi inayoitwa Tanzania imekuchagua wewe kwa sasa kuwa raisi wao na una kila mamlaka na nguvu ya kuamua na kuiongoza. Naomba nikukumbushe kuwa hauitaji kuomba ruhusa ya yoyote yule kufanya kazi yako. Haya mambo ya kushuhudia na kujua yote waliyofanya marafiki zake kina Karamagi, Msabaha, Rostam Azizi, Mgonja, na mzee wa kasungura na ndege ya kupaa al-fisadi bin Lowasa bado ulikuwa hujaamua tu cha kufanya na nani atachukua nafasi zao? Yaani mpaka Lowasa ajiuzulu huku akitoa kashfa kubwa sana ndio uanze kupanga pa kutokea?
Pendekeza PM, nchi iende mbele kwa sababu hapa halali mtu leo mpaka kieleweke. Tukimaliza richmond tunakuja buzwagi, kiwira na zile pesa za benki zilizotumika kwenye uchaguzi mwaka 2005. Mhe Kikwete, majina watendaji wako wanayorusha hapa kwa siri yote kwangu ni sawa tu maana kuna kazi kubwa iko mbele ya kungoa miti yote ya ufisadi hapa bongo. Haijalishi kama unamleta Pinda au mama Kilango, bado haina tofauti kama unamleta Membe au chaguo lako la muda huu la mama Makinda.
Taifa linakusubiri...tik tak tik tak tik tak tik tak.....