Kikwete na Shahada Mbili za Udaktari kwa mwaka mmoja... Wasomi wetu Vipi juu ya Hili

geophysics

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
904
166
GO9G9231.JPG


Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi,Muhimbili Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akimtunukia Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Afya ya Jamii(Doctor of Public Health,Honoris Causa) wakati wa mahafali ya nne ya Chuo hicho iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto akiangalia ni Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Kisali Pallangyo....... Mwananyamala, Amana na Temeke watu wanakufa kwa kukosa dawa.... Malaria inaua watu mara tatu zaidi katika uongozi wa awamu ya nne ya uongozi...kipindu pindu kila mwaka..... Vyoo vya shimo karibu kila mahali, mifereji ya maji machafu inafurika hadi City center.... Muhimbili maiti zinaozea vitandani kama sio mortually.... Kweli hii shahada ya udaktari aliyepewa anastahili kwa wakati huu??
 
Na UDOM nao wamempa shahada ya udaktari eti ni kweli???
Muhimbili pia eti ni degree ya heshima ya udaktari wa afya.....
 
sasa kama mwenyewe kataka kwa nini asipewe? ukiwa na nguvu utapewa kila kitu hata kama siyo stahili yako. huenda mheshimiwa ndoto zake ilikuwa kupata PhD, sasa ndoto zake zimetimia tena na kupitiliza. Tatizo hapa ni kuwa na wasomi uchwara ambao wanadharirisha hizo PhD kwa kumtunuku mtu hata asiyefaa. Shame on them!!!
 
Body language ya pallangyo inaacha hoi, inaonesha kama vile anasali wakati mkulu anakwaa digrii. Ni kama vile anatubu kwa mungu kwa kuruhusu kitu hicho kieendelee. Wanasaikologia waichunguze picha hiyo na kutueleza finding zao
 
Hii ndo Tanzania masalia, yaani mambo yanayoendelea utadhani kuna uwendawazimu fulani unawasukuma watu kuyatenda. Historia siku moja itahitaji kujua ni wapi sisi Wabongo tulipojikwaa; na hasa hasa hawa wasomi wetu, sijui ni nini kilichoboreka sana ndani ya huduma ya afya ktk kipindi hiki, kustahiki hiyo degree, uwenda wagonjwa wanaolala mzungu wa nne pale Mhimbili au wanaolazwa chini kwenye sakafu, anyway hii ndo Afrika
 
Vyuo vingi hutumia nafasi hiyo ya kutoa shahada kwa viongozi, kwa kujikweza ili vionekane vyuo vya maana. Na Kiongozi wa nchi akishakua phd hapo, chuo hicho hutegemea kuwa PHD zingine za hapo zitakuwa zinakubalika katika jumuiya za wanataaluma. Ni mbinu inayotumiwa na vyuo visivyojiamini kuwa ni vyuo vikubwa ndio vinatumia ujanja huu. Hata hivyo vyuo vizuri pia huweza kutoa PHD za heshima kwa kufuata vigezo fulani. Hapa nina maana kuwa MUHAS inawezekana ni chuo kizuri tu ambacho kimeamua kumpa mheshimiwa PHD kwa kuzingatia vigezo fulani.
 
mambo ya tz kila kitu ni siasa tu, kuna umhimu gani ya kuwapa maraisi waliositaafu kuwa tena wakuu wa vyuo kama sio siasa zaidi? kwani hakuna wasomi nchini wakuweza kuongoza hivyo vyuo? everything is politics hata katika mambo ya mhimu zaidi lol
 
Sioni tatizo hawa watu washajua kuwa JK ni mtu wa kupenda sifa na ukimpa iyo PHD ya heshima lazima akulipe fadhila.
Mtaziona zikimiminika izo PHD za heshima
 
MUHimbili wanatibiwa walalahoi.
I guess Mwinyi check up Ulaya!wengine wanakwenda India na Sauzi .

Tanzania a big joke!
 
Hivi hawezi kuzikataa hizo shahada za heshima? Ooh nimesahau....yeye mwenyewe anazipenda...jaribuni tu kuangalia lugha yake ya mwili pindi azipokeapo. Inaongea kila kitu.
 
naskia makamu mkuu wa chuo alitaka kupandisha mzuka kwa kupayuka ili kukataa kumpa jk hiyo phd.......
 
Back
Top Bottom