Nnamfuatilia Raisi Jakaya Kikwete,anasema "Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa sn"Hivi uchumi wa nchi kukua kuwa na majengo marefu au hali nzuri(kujimudu kimaisha)kwa wananchi?
Hii naona kama inamlenga Waziri 6...manake yy ndo anatofautiana wa mawaziri wenzake mara nyingi. So kwa mwendo huu kila kitakachosemwa basi majibu...''ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI''......!!
msiwatwange mawe....barabara ya kilwa mmeijenga kwenye kiwango kizuri tu zungukeni kwenye vyombo vya habari muanze kujitangaza, kwa sababu wananchi hatuna macho
neakaje magwaha ya weakwe.
eti anadai anategeneza misingi ya leo kwaajili ya 2025 huu ni uongo wa hali ya juuuu, nchi ishakushinda semina haifai hata kuangalia inaboa wala haifai nashangaa sana jk na serikali yake kuendelea kuwa madarakani mpaka sasa
Hapa ningemuona angalau kidogo kuna akili imesaria kichwani mwake kama angevunja baraza la mawaziri, hizi semina elekezi ni mbinu mpya ya kuiba pesa za watanzania, wakati wahuzuliaji wenyewe wa semina hakuna anaesikiliza kitu zaidi ya kusubiri posho, mimi nilifikiri atakuwa ameshajifunza na semina aliofanya kipindi chake cha kwanza kule Ngurudoto Arusha kwamba ilikuwa ni waste of money.
Mimi sielewi anawaelekeza nini??
Mkuuu uko sahiihi na aksante kwa mashahihisho lakini kurugenzi nyingi za habari kwenye mawizara na idara zimeanza ipindi cha JK. kabla hapo vitengo vya habri vilikuwa vina watu na iidara za kawaida tu. Chap chap watu wakisikia statement kama hizi za raisibalada ya kufanya kazi wao wanajua ulaji.Naomba nisahihishe kidogo.
Kikwete HAKUANZISHA kitengo/idara ya mawasiliano kwa kila wizara. Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha hivi vitengo na kama mtakumbuka Peter Kallaghe (kwa sasa Balozi wa TZ- UK) ndiye alikuwa Director of Communications State House. Na kiutendaji ni kwamba Director wa Com State House alikuwa ana-coordinate mawasaliano toka idara/wizara zote hivyo kuweza kuifanya Serikali kuwa na sauti moja. Nisema Peter Kallaghe alikuwa amepiga hatua nzuri sana katika kuanzisha huu mfumo wa mawasiliano ndani ya Serikali huku akipata msaada mkubwa (financial & human resources) toka UNDP na DFID-UK.
Sasa hivi Salva Reywemamu ndiye Mkurugenzi na nadhani mambo yamedorora kiasi kwani Salva anaonekana kufanya kazi ya "Press Officer' na sio Director. Director maana yake una-direct na ku-coordinate govenment communication system including press officer.
Vitengo vya mawasalino/habari katika mawizara ni kama watoto yatima kwa sasa. Na mbaya zaidi vinafanya kazi kama Press angency yaani wanasubiri waziri awaambie nini cha kusema, press release mambo yamekwisha. Hakuna research, public oponion kwenye mikakati ya hivi vitengo.
... hii inanikumbusha kisa cha mlevi na mkewe walipotinga nyumbani wakiwa chakari na pale jamaa aliamrisha apewe chumba namba 17. Nyumbani kwake mwenyewe. Walevi bana! kwi kwi kwi.