Kikwete na semina elekezi kwa Mawaziri - Dodoma 2011

- Ukifanya kitu bila kukieleza ni sawa na kwamba hukukifanya
Childish!

Zamani tukiwa watoto nakumbuka ukienda mtoni kuteka maji, basi wakati wa kurudi unakataa kupokelewa na mtu mwingine yeyote zaidi ya mama aU baba!... ha ha haaaa!
Sasa sentenso ya pale juu kwenye quote ni kitu kama hicho!

Unatumia gharama kutengeneza kitu, then unatumia gharama ingine kutangaza kuwa umefanya!
Nakumbuka serikali ya hawa MAGAMBA iliamua kutuma mawaziri wake wazunguke nchi nzima kueleza mafanikio ya serikali(my hairs!!!!) na fedha nyingi sana ililiwa kwa mtindo huo wa safari za upuuzi na upofu!

Mtu ukifanya jambo zuri huna haja ya kupitisha nyago kuwaambia watu kuwa umefanya kadha na kadha, watu wataona wenyewe bana!

Kweli MAGAMBA mmechoka, na haata MKIGAWA FEDHA KWA RAIA hakuna jinsi mnaweza kujitoa shombo la UFISADI!
 
semina teketezi tu, kodi zetu zinateketezwa. Wasimlazimishe Sita kukubaliana na maamuzi ya kifisadi ya baraza la mawaziri. Sita watwange mumo kwa mumo, si kakuteua mwenyewe wakati anajua ww si wa aina yao?
 
Mbona haya maelezo yapo kijazba jazba......sijaona mafanikio yoyote anayotaka tuelezwe hapa. Kwa hio hata kama waziri alichosema hakina mantiki wala Tija kwa taifa basi mawaziri wengine tuitikie tu?? No I doubt him
 
Hapa ningemuona angalau kidogo kuna akili imesaria kichwani mwake kama angevunja baraza la mawaziri, hizi semina elekezi ni mbinu mpya ya kuiba pesa za watanzania, wakati wahuzuliaji wenyewe wa semina hakuna anaesikiliza kitu zaidi ya kusubiri posho, mimi nilifikiri atakuwa ameshajifunza na semina aliofanya kipindi chake cha kwanza kule Ngurudoto Arusha kwamba ilikuwa ni waste of money.

Pls JK asidhani kwamba Watanzania bado ni misukule. Tunahitaji atimize ahadi zake 68 alizoahidi kwenye uchaguzi mkuu, mimi silishwi porojo za kichovu hizo na sidanganyiki ng'ooo!
 
Mbona haya maelezo yapo kijazba jazba......sijaona mafanikio yoyote anayotaka tuelezwe hapa. Kwa hio hata kama waziri alichosema hakina mantiki wala Tija kwa taifa basi mawaziri wengine tuitikie tu?? No I doubt him



Hivi mtu kama Ngeleja ataeza mafanikio yepi wakati ndio kwanza Tanesco wametutangazia giza! Na Wasira naye kafinikiwa nini? au Gaudensia Kabaka kaongeza ajira ngapi? Hawa Ghasia je ameweza kutoa maruhani wote kwenye payroll system ya serikali? Nadhani bunge lijalo litakuwa mdundiko -sega! tusubiri.
 
semina teketezi tu, kodi zetu zinateketezwa. Wasimlazimishe Sita kukubaliana na maamuzi ya kifisadi ya baraza la mawaziri. Sita watwange mumo kwa mumo, si kakuteua mwenyewe wakati anajua ww si wa aina yao?

Hapo kwenye red hapo.....nimempapenda jhadi machozi yakanitoka....hivi tujiulize...mwaka uleee walienda Ngurdoto-Arusha kwa semina elekezi/teketezi, wakateketeza billion tatu( Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari) je zilikua na manufaa gani kwa taifa hili? zaidi ya kututia umaskini zaidi? Hivi hakuna mahali tukaenda kuwasemea hawa jamaa??
 
Hivi mtu kama Ngeleja ataleza mafanikio yepi wakati ndio kwanza Tanesco wametutangazia giza! Na Wasira naye kafinikiwa nini? Vituko!
Analazimisha ujinga na kinachofuata baada ya hapo ni Uongo, Yes < si Boss kasema tutangaze mafanikio? Ndio tutasimama majukwaani na kusema kuwa tulinunua Bajaj kama Ambulance!! What the Hell is this?

Wenzetu na majirani zetu wanawaza kununua Helcopters kama Ambulances sisi tunanunua Bajaj, yaani baada ya kwenda mbele tunarudi nyuma.....natamanui kulia kwa hasira. Halafu kuna watu wanawatetea.....
 
Ukiangalia yote aliyoongea hapo juu utaona kwamba Raisi Kikwete hajaacha ngebe za kuwadhalilisha na kuwaonyesha Mawaziri kwamba hawafai kwa jamii.

Ukweli yeye ndio mwenye tatizo mtu atauliza imekuwaje yeye kama Raisi avumilie baada ya kuambiwa waziri wako alilewa mpaka akabebwa si amfukuze kazi juzijuzi tuu hapa Ruana Waziri ili bidi ajiuzulu baada ya picha yake na vimwana ilivyowekwa wazi kwa umma.

Anakiri kwamba mawaziri wake hawawajibiki wanafanya kazi chini ya muda kisheria halafu yeye anaendelea kuwaweka,huyu bwana anatuchosha na propaganda zake hana pakushika tumelimika hatutadanganyika tena.

Angejiuliza kwa nini serikali yake haiaminiki na wananchi, kwa undani angeanza kujisafisha na kusafisha mawaziri wake wabovu, ungekuta wananchi ndio tungeona mabadiliko na kurejesha imani yetu kwake vinginevyo anaendeleza usaniii wake tuuu
Ni kweli mkuu, hajaeleza ufanisi au udhaifu wa ofisi anayoiongoza yeye mwenye - Ikulu
 
Hivi hakuna kitu kingine cha kuweza kutuletea maendeleao zaidi ya hizo porojo zao? Naomba sana kama ikiwezekana atueleze pia kuhusu mgawo wa umeme ulioanza tangu juzi huku akitangaza kuwa mgao mkali zaidi unakuja!!! Hivi hawa jamaa wakoje vile??
 
Mafanikio????

Kuhusu elimu ya kujenga vyumba vya madarasa na kuwapotezea muda watoto wetu, kuwafanya wawe makahaba na majambazi ya hapo baadae, wavuta bangi na washinda mitaani??? Labda khusu barabara?? Barabara gani zote zimejengwa chini ya kiwango ukiacha Sam Nujoma peke yake? Nenda kaangalie Shekilango, hiyo Kawawa je? Na nyingine nyingi.

Mmh hebu tuangalie Zahanati labda.... kila siku akina mama wanafia njiani, hakuna madawa hakuna chochote cha maana, Madokta wanakimbilia green pastures Botswana na kwinginkeo wanakojua kumlinda Proffessional.

Je kwenye Ualimu?? Huyu ndio amekuwa mtu wa kuonewa kwa kila jambo, pesa anakatwa, mzigo wa lawama juu,, mazingira ya kazi mabovu na kudhalilishwa juu yake, apigwe na wanafunzi yeye, atukanwe yeye, adhulumiwe yeye! Kha.

Hao Polisi ndio wanaishi kwenye mabanda ya Nguruwe na kuku, je kuku na mifugo mimingine tuipeleke wapi???

TZ let us be serious. Ngoja nilie kwanza halafu narudi
 
Kikwete is a Joker!
He is indeed a very big JOKER Rev.

Hivi jamani tofauti ya semina hiyo ya Dom na zile za Ngurudoto ni nini?

Financially nchi inapumulia mashine badala ya kupunguza matumizi unaongeza matumizi kwa kazi zisizo na tija kama hii? Ninatamani ningeiona program ya hiyo semina ndugu though I'm sure huu ni aina nyingine ya upuuzi wa awamu ya nne.

Je ni kweli kwamba hayo watayoongea hapo walishindwa kuyaongea katika moja ya vikao vya baraza la mawaziri? JK wewe na serikali yako mkifanya mambo mazuri wananchi tutayaona tu wala huhitaji kusimama mbele ya camera na kuyaimba kama wimbo, hilo waache waimbaji wa bongo flavour na taarabu..
 
Bravo JK kwa kuchukua hatua wakati muafaka!!!n:israel:

Ameongea hajachukua hatua. Kama kuongea ndo kuchukua hatua basi huyu jamaa amechukua hatua nyingi sana ikwemo ya kuahidi kujenga World Trade Centre hapa Dar wakati akiwa huko Cape Town hivi karibuni. Yaani aibu..
 
Kishindo cha upinzani wa kweli kinamtia wazimu mkuu wa nchi... Sasa anatapatapa mpaka atakimbia nchi... izo semina elekezi anatoa kila siku lakini hazina tija...

Chama Cha Magamba kinatia huruma sana... from hero to zero! Go go go Chadema
 
Back
Top Bottom