Kikwete na semina elekezi kwa Mawaziri - Dodoma 2011

.............. but huu upuuzi wa huyu jamaa sijui utakwisha lini watu tunataka vitendo si maneno anazidi kujidhalilisha sana!

Mkuu sometime inabidi tuangalie level ya upuuzi kuna upuuzi mwingine uliopo sio wa rais ,wala waziri kuu wala waziri. Katika middle maanagement ambapo kwamtazamo wangu kuna vijana wengi pia kuna tatizo ten sugu

Mfano juzi juzi nimeona meya wa ilala anayeitwa J. silaa akiongea pumba . Sasa ukiona mawazo ya Pinda na jery silaha hayana hata chembe ya utofauti japo kidogo jua kuna tatizo kubwa . Na mwenye tatizo anakuwa sio pinda bali hi huyo kijana.


Au unaweza kujitahidi kumuelewa Msekwa akilaumu Jf lakini wanapokuja watu wenngine ambao ndio wanaonekana kama future ya CCM nao wakiwa na mawazo kama ya msekwa juu ya jf hiyo ni cancer ya taifa.
 
Hii naona kama inamlenga Waziri 6...manake yy ndo anatofautiana wa mawaziri wenzake mara nyingi. So kwa mwendo huu kila kitakachosemwa basi majibu...''ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI''......!!

JK yuko sahihi colective responsibility inatakiwa Lakini na Six naye yuko sahihi. tatizo kati ya hao nani mwenye ujasiri kuliko mwenzake wa kufanya maamuzi magumu ????

Nahodha JK amtose Six Au six aone jahazi alilomo haliendi kule anapooona panafaa na kujitoa. Kujiuzulu au kumuomba kiongozi fulani ajiuzulu ni vocabulary wakati tunasema tuna demokrasis

Mwisho wa siku unakuta wote ni wanafiki kila mtu ana faidika na uwepo wa mwenzake pamoja kuwa kuna mamboya msingi hawakubaliani. Sisi watanzania wa kawaida ndo tunatoka kapa.
 
Kikwete wakati anaingia madarakani kila kitengo kilianzisha idara ya mawasiliano na habari. Wizara na idara zikateua wakurugenzi wa habari. Alilisisitiza sana jambo hili........

Sasa sijui waliopewa vitengo ndio wadhaifu au hawajui nini majukumu yao. au nchi ina wanasiasa wengi kuliko watendaji.

But tunaweza kumalaumu JK tu lakini kuna uzembe wa watendaji wengi. na wengi wao ndo sisi.


TB
Naomba nisahihishe kidogo.

Kikwete HAKUANZISHA kitengo/idara ya mawasiliano kwa kila wizara. Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha hivi vitengo na kama mtakumbuka Peter Kallaghe (kwa sasa Balozi wa TZ- UK) ndiye alikuwa Director of Communications State House. Na kiutendaji ni kwamba Director wa Com State House alikuwa ana-coordinate mawasaliano toka idara/wizara zote hivyo kuweza kuifanya Serikali kuwa na sauti moja. Nisema Peter Kallaghe alikuwa amepiga hatua nzuri sana katika kuanzisha huu mfumo wa mawasiliano ndani ya Serikali huku akipata msaada mkubwa (financial & human resources) toka UNDP na DFID-UK.

Sasa hivi Salva Reywemamu ndiye Mkurugenzi na nadhani mambo yamedorora kiasi kwani Salva anaonekana kufanya kazi ya "Press Officer' na sio Director. Director maana yake una-direct na ku-coordinate govenment communication system including press officer.

Vitengo vya mawasalino/habari katika mawizara ni kama watoto yatima kwa sasa. Na mbaya zaidi vinafanya kazi kama Press angency yaani wanasubiri waziri awaambie nini cha kusema, press release mambo yamekwisha. Hakuna research, public oponion kwenye mikakati ya hivi vitengo.
 
UPDATES:

-Ni marufuku mawaziri kutoelewana

-Mawaziri wakishakubaliana katika baraza la mawaziri ni uamuzi wa wote

-Ukiona ni vigumu kuafiki ni bora kutoka

-Ni lazima kutekeleza uwajibikaji wa pamoja

-Hata miswada ya sheria bungine ni ya mawaziri wote

-Ni kinyume cha maadili waziri kupinga muswada wa waziri mwenzake

- Ni lazima muwe team players

- Kuhudhuria vikao vya bunge kwa mawaziri ni lazima

- Ni marufuku wakati wa vikao kutembelea jimbo lako

- Katika kikao cha bunge hatutegemei waziri kuwa na safari zitakazokuondoa bungeni

- Tuna udhaifu mkubwa katika kusema mafanikio yaliyopatikana

- Ukifanya kitu bila kukieleza ni sawa na kwamba hukukifanya

- Uongo ukisemwa mara nyingi hugeuka kuwa kweli

- Wananchi wanalaumu serikali kutokana na kuelezwa uongo dhidi yake

- Tuwe wepesi kusahihisha uongo dhidi ya serikali, raslimali zipo, vyombo vya habari vipo, hatuvipi habari

- Kila wizara kuna wasemaji, hawasemi, wasemasji wengine wanazuiwa kusema

- Maafisa habari wapewe fusa watuimie taaluma yao, wao wanajua; msilaumu kwamba vyombo haviwataki

- Lazima serikali iwasiliane na watu wake kupitia vyombo vya habari

- Kama ulikubali kuwa waziri ni lazima uitumikie, tafuta muda muafaka wa kuhudumia jimbo

- Mawaziri wengine wanaongozana na kundi la waandishi wa habari majimboni

- Uadilifu ni muhimu sana waziri, naibu, katibu mkuu wanatakiwa kuwa mfano mwema. Mawaziri, naibu wasinyooshewe vidole. Siyo kufika saa 5 na kuondoka saa 7 mchana; uzembe, wizi, kuchonga line za kupata, kutumia ofisi kujunufaisha, ulevi, uzinzi wala ubabe

- Haiwezekani unakunywa kwenye baa unakunywa mpaka unapataka msaada wa kubebwa

- Ukiwa waziri ni kuwa kuna baadhi utavikosa. Unakatisha wananchi tamaa, acha ubabe, unadhulumu watu

- Sasa JK anaelezea utelezaji wa ilani kwa miaka mitano nyuma. Mipango ya baadaye nk katika kuwatumikia wananchi. Kilimo, afya, miundombinu kuboreshwa katika kutekeleza vision ya 2025

- Kwamba itafika wakati umeme utakuwa haukatiki

- Bado kuna makosa mengi, kuna upotevu wa fedha za umma

- Kuna maendeleo fulani lakini hayatoshi

- Tutapata kusikiliza kutoka kwa watendaji wa vyombo vya dola kuhusu jitihada zinazofanywa na idara zao

- Hali ya kupunguza msongamano wa wafungwa, usalama, udhibiti wa madawqa ya kulevya, takukuru

- Kila wizara iandike kueleza mafanikio katika wizara yake, tufanye tahmini ili kuhifadhi kumbukumbu kwa vizazi vya baadaye

wana udhaifu.

waongo.

walevi.

sas tuna mwaziri au wahuni tu. au ndo tuseme wameteuliwa kimjinimjini?
 
Hivi wakati Kikwete anatembelea Wizara lengo hasa lilikuwa ni nini, sioni tofauti kati ya Rais kutembelea Wizara na Rais kuwapa Semina elekezi mawaziri, halafu hii habari ya kusema eti umeme utakuwa haukatiki wakati tumeishatangaziwa mgao kuanzia wiki ijayo nashangaa sana anaposema kitu ambacho hana uhakika nacho.

Anaposema"NI MARUFUKU MAWAZIRI KUTOELEWANA" hapo hata sijui labda kama mimi ndio sijamuelewa vizuri huyu Kikwete
 
Hivi wakati Kikwete anatembelea Wizara lengo hasa lilikuwa ni nini, sioni tofauti kati ya Rais kutembelea Wizara na Rais kuwapa Semina elekezi mawaziri, halafu hii habari ya kusema eti umeme utakuwa haukatiki wakati tumeishatangaziwa mgao kuanzia wiki ijayo nashangaa sana anaposema kitu ambacho hana uhakika nacho.

Anaposema"NI MARUFUKU MAWAZIRI KUTOELEWANA" hapo hata sijui labda kama mimi ndio sijamuelewa vizuri huyu Kikwete

Kwani pumba zinaeleweka?
 
Sijui ni mimi tu au kuna mtu mwingine anapata shida na hii style ya kufanya/kutoa maamuzi hadharani. Haya mambo anayoongelea Mh Rais nadhani ni ya ndani zaidi na sioni logic ya yeye kutumia vyombo vya habari katika kuwekana sasa.

Binafsi ningetaka kusikia serikali inaongelea mikakati ya kuongeza ajira kwa vijana, kupunguza inflation, security etc etc ni sio maelekezo kwamba mawaziri wasitembelee majimbo yao wakati wa vikao vya bunge! Yaani wanasafiri all the way to Dodoma kuongelea vitu ambavyo kwangu ni job-description? Kwa mfano, point kwamba Ni kinyume cha maadili waziri kupinga muswada wa waziri mwenzake - hii si suala la kuongelea kwenye cabinet meeting tu? No wonder this country is broke maana kwa matumizi ya hovyo kama haya hela itatoka wapi.
 
Jamaa anaangaika si kawaida amezungukia wizari zote (je alikuwa anapoteza muda?) sasa mawaziri kesho makatibu kesho kutwa wakurugenzi mtondo afisa mradi mtongooo wafagiaji

Do we have president????
 
Sijui ni mimi tu au kuna mtu mwingine anapata shida na hii style ya kufanya/kutoa maamuzi hadharani. Haya mambo anayoongelea Mh Rais nadhani ni ya ndani zaidi na sioni logic ya yeye kutumia vyombo vya habari katika kuwekana sasa.

Binafsi ningetaka kusikia serikali inaongelea mikakati ya kuongeza ajira kwa vijana, kupunguza inflation, security etc etc ni sio maelekezo kwamba mawaziri wasitembelee majimbo yao wakati wa vikao vya bunge! Yaani wanasafiri all the way to Dodoma kuongelea vitu ambavyo kwangu ni job-description? Kwa mfano, point kwamba Ni kinyume cha maadili waziri kupinga muswada wa waziri mwenzake - hii si suala la kuongelea kwenye cabinet meeting tu? No wonder this country is broke maana kwa matumizi ya hovyo kama haya hela itatoka wapi.

Point, but jk hawezi kufikilia mambo hayo mwenyewe anataka sifa tu
 
Mambo yote anayoyaorodhesha leo ndio standard operation manual ya serikali.

Kuna matatizo mawili makubwa yanayomkabili Kikwete na serikali yake:

Kwanza, haya hayatekelezwi na pili, ambalo ndilo kubwa zaidi, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kutokana na kutotekelezwa haya zaidi ya maneno zaidi kama anavyofanya kupitia hiyo semina elekezi.

Kwa hali jinsi ilivyo hakutakiwa kuwe na semina elekezi tena. Huu ulikuwa ni wakati wa vichwa kuviringika, si kukumbushana wajibu kwa sababu kila mmoja serikalini anajua wajibu wake... kama kuna ambaye hajui, hakustahili kuwepo humo
 
Nadhani JK anajisumbua kwani pamoja na tamko lake lakini hakuna atakayeheshimu, subirini mtaona. Kuna matamko mengi yamekwishatolewa lakini mmmh! Sielewi nchi hii inaelekea wapi?
 
Ukiangalia yote aliyoongea hapo juu utaona kwamba Raisi Kikwete hajaacha ngebe za kuwadhalilisha na kuwaonyesha Mawaziri kwamba hawafai kwa jamii.

Ukweli yeye ndio mwenye tatizo mtu atauliza imekuwaje yeye kama Raisi avumilie baada ya kuambiwa waziri wako alilewa mpaka akabebwa si amfukuze kazi juzijuzi tuu hapa Ruana Waziri ili bidi ajiuzulu baada ya picha yake na vimwana ilivyowekwa wazi kwa umma.

Anakiri kwamba mawaziri wake hawawajibiki wanafanya kazi chini ya muda kisheria halafu yeye anaendelea kuwaweka,huyu bwana anatuchosha na propaganda zake hana pakushika tumelimika hatutadanganyika tena.

Angejiuliza kwa nini serikali yake haiaminiki na wananchi, kwa undani angeanza kujisafisha na kusafisha mawaziri wake wabovu, ungekuta wananchi ndio tungeona mabadiliko na kurejesha imani yetu kwake vinginevyo anaendeleza usaniii wake tuuu
 
Point, but jk hawezi kufikilia mambo hayo mwenyewe anataka sifa tu

King of Kings,huu ndio ugonjwa mkubwa unaoutafuna ccm na serikali yake. wanajiaminisha kwamba wanachokiongea basi ndicho hicho hicho wananchi wananchi wanataka kusikia! Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi. Chadema kazeni buti kuongelea mambo yanayowagusa wananchi.
It will be interesting to know budget ya 'vitafunwa' kwenye hii semina elekezi!
 
kama jk alivyochoka kuingoza nchi ninayoishi mimi vivyo hivyo nami nimechoka kukaa nchi inayo-ongozwa na jk..TUMECHOKANA...

sijisikii raha kuitwa mwananchi wa jk na namuomba asijisikie raha kuitwa rais wangu.... JK MIE KAMA MTANGANYIKA AISEE NIMEKUCHOKA MZEE... SIKUELEWI UNAONGEA NINI NA UNAFANYA NINI...HUFAI KUONGOZA BWANAAA SI UONDOKE TUU BWANA
 
Hili la kuongozana na kundi la waandishi majimboni hata yeye alikuwa akilifanya wakati akiwa waziri....wenzie wataacha kweli.
 
Back
Top Bottom