Kikwete na Rais Magufuli hawana shida, sisi tu

Rulleger

Member
Aug 29, 2015
84
60
Eti JK hafurahishwi na JPM kwa sababu ya jinsi anavyotumbua majipu. Hizi hisia uwa zinakuwa batili kila watu hawa wakikutana. Wanaonyesha kuheshimiana na wanafurahiana.

JPM atamkoseaje heshima JK wakati kamfanya waziri wake kwa miaka 10? Pia bado anafuata mipango ya uchumi na dira ya taifa aliyoweka JK. Tusisahau kuwa hata kama inasemekana kuwa JPM hakuwa chaguo la kwanza la JK kwenye urais bado alikuwa mmoja wa watu ambao JK aliamini wanaweza kazi hiyo ndo maana akaingia tano bora za CCM, n.k.

Kwa upande mwingine JK hawezi kulalamika kwa sababu ya kutumbuliwa majipu. Mwenyewe alisema alikuwa mpole sasa anakuja rais mkali. Pia kila utawala una enzi zake na style take. Baada ya Magufuli itakuwa hivyo pia. Rais mpya na mambo mapya - labda anayependa kuongea na vyombo vya habari zaidi au anayependa Bunge lionyeshwe live, n.k

Kwa hiyo wazo kuwa hawa watu wana kinyongo ni hisia zetu tu. Hawana shida. Hongera JPM na JK.

Ref: Rais Dr. Magufuli ashiriki kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM
 
Wakati mwingine chumvi inayokifanya chakula kiwe kitamu, huweza kuharibu ladha ya chakula. Viongozi wa nchi wanayo madhambi yao, lakini kwa sababu hawawezi kumjibu kila anayewashambulia kwenye vyombo vya habari, hulazimika kukaa kimya na kupuuzia.
 
Kikwete-Maguccm_640_392.jpg
 
Singidadodoma,Moyo ni mkubwa sana,na Lady Jaydee aliimba kwamba hata siku moja usiusemee moyo wa Mwingine?SIyo kila Cheko ni la furaha...................Pole sana
 
Singidadodoma,Moyo ni mkubwa sana,na Lady Jaydee aliimba kwamba hata siku moja usiusemee moyo wa Mwingine?SIyo kila Cheko ni la furaha...................Pole sana
Kwa iyo wewe kwa akili zako za kupika maandazi unaona hawa watu wanabeef ? Your hypocrisy astounds me
 
Kwa iyo wewe kwa akili zako za kupika maandazi unaona hawa watu wanabeef ? Your hypocrisy astounds me

Bora ninaakili ya kupika maandazi maana najitegemea,na wewe je,akili zako zilizoshikwa na mtu mwingine?Unayesubiria kulipwa pale tu unapotoa hoja za kutukana wenye mawazo tofauti au kusifia hata visivyosifika.Kuna mahali nimesema hawa watu wanabeef?Usiwe unapenda kukimbilia kutukana kama hujamuelewa mtu.
 
Uwa nashangaa watu wanaosema JPM aliwekwa na Mkapa aaah wap kwa nguvu gan aliyokua nayo asikudanganye mtu urais unatoka kwa hawa wafuatao
1. Mkuu wa nchi kama rais anayeondoka madarakan hakutaki ni ngum sana kupewa urais refer lowasa na Jk
2. Jeshi hawa watu kama hawakutaki sahau kupewa nchi
3. Usalama pia hawa wana nafas kubwa katk kumweka madarakan mkuu wa nchi
Kwa maana iyo bas kikwete ndo kamwe magufuli kwan ata hao niliowataja safu zao zilisukwa na jk kwa iyo wasingeweza kumwangusha
 
Bora ninaakili ya kupika maandazi maana najitegemea,na wewe je,akili zako zilizoshikwa na mtu mwingine?Unayesubiria kulipwa pale tu unapotoa hoja za kutukana wenye mawazo tofauti au kusifia hata visivyosifika.Kuna mahali nimesema hawa watu wanabeef?Usiwe unapenda kukimbilia kutukana kama hujamuelewa mtu.
the way ulivooandika haitaki ata uwe na degree kujua ulichokusudia ..mfano sio kila cheko ni la furaha" apa ulikusudia nini kwa kiswahili sanifu?
 
the way ulivooandika haitaki ata uwe na degree kujua ulichokusudia ..mfano sio kila cheko ni la furaha" apa ulikusudia nini kwa kiswahili sanifu?

Ajuaye maana hapaswi kuambiwa maana.Nimejibu aliyetoa hoja kwamba asiusemee moyo wa mtu na ajue kwa hilo siyo kila cheko ni la furaha.Sijamaanisha chochote zaidi ya kumsahihisha tu aliyetoa hoja period.

Na ninamaana hiyo hiyo kwamba siyo kila ninapocheka nimefurahi............Kuna kicheko kingine inabidi tu nicheke maana sina namna hadhara isinifikirie vibaya....Bado sijamsema mtu nimeusemea moyo wangu.
 
Kwa vile umequote wimbo wa Jedy ukute uko full mistari ..jioni njema.
 
Shida iliyopo hapa ni:
ni watu wachache walio mpigia magufuli(c.c.m) kura wakiamini kuwa ktk uraisi wake wote,uccm atauweka kando!
Mwengine wanaenda mbele hata kudiriki kuamini kuwa Magufuli anabifu,chuki,au hasira na chama chake,nadhani ule uongo wa pigia kura Magufuli ila Sio C.C.M wengi uliwaingiza mkingi!
Hawaamini Magufuli wao anaweza tena leo akawa spotted akiwa amevaa madera ya kijani!
Tena kuna wengine imefikiwa kumhodhi Magufuli kuwa ni wao na sio mali ya C.C.M!
Pasipo kujua,watu hawa wanashindwa kujielewa kuwa walipigwa changa la macho kwa kuuziwa mbuzi kwenye gunia!
Ukimchagua Magufuli Umeichagua C.C.M,Mapema Watakapoacha Kuota Kuwa Magufuli ana bifu na Mwenyekiti wake the better!
Siwapendi C.C.M Kiitikadi,ila nawakubali kwa ujuzi wao wa siasa!
Walipiga Chenga ya Mwili wabongo,wamekuja shtuka wamemshangilia mchezaji wao wampendao na timu yake!
Tena mnavyo zidi kuwasema JK na Magufuli ndiyo mnavyo zidi kukiweka chama cha C.C.M katika chati!
HIVI NYIE MNAO JARIBU KUMTENGA MAGUFULI NA JK,HUWA MNAWASILIZA MAONGEZI YAO WANAPO KUWA FARAGHA YA WATU WAWILI?
 
Back
Top Bottom