Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
Kwa matamshi na maamuzi haya ya viongozi wa juu wa Taifa...... kumbe bado nchi imekwama kwenye matope.... sasa sijui tufanyeje ili tuikwamue.....
KWA MUDA MREFU NIMEVUMILIA KUTOCHANGIA HII THREAD ILI ANGALAU NIONE KAMA WATAJITOKEZA MASHABIKI WA MAGUFULI WAKIWA NA VIELEE-LEZO AU WATAENDELEA KUMWAGA MANENO MATUPU KUWA MAGUFUOI ANASIMAMIA SHERIA BILA YA KUZITAJA KINAGAUBAGA SHERIA ANAZOSIMAMIA ILI KWA PAMOJA TUZIPIME KAMA ALIKUWA SAHIHI AU MAGUFULI ALICHEMKA.
NAANZA SASA:-
SABABU ZA MAGUFULI KUAKARIPIWA HIZI HAPA.
Sasa imebainika sababu za Mhe John Pombe Magufuli kukaripiwa na wakubwa wake serikalini ni kutokana na kuwa mbumbumbu wa sheria za barabara ambazo amekuwa akitamba kuwa aliapa kuzilinda.
Kama ambavyo Mhe John Magufuli aliliambia bunge lililoisha wakati akijibu swali kuhusu hifadhi ya barabara, alisema upana wa hifadhi hiyo nchi nizma ilikuwa ni Mita 22 kila upande kutoka katikati ya barabara, lakini upana huo uliongezwa kufikia Mita 30 kwa Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 zilipopitishwa kwa Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009 ibara ya 29 . Na akaongeza kuwa wananchi wanaoguswa na ongezeko hilo wana haki ya kulipwa fidia.
Ibara ya 27 (2) ya Kanuni za Sheria hiyo inamtaka Waziri wa Ujenzi atakaporidhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara atawasiliana na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa. Kutokea upana wa hifadhi ya barabara kuongezwa kwa MIta 8 kupitia Kanuni za 2009, hakuna Waziri yoyote wa Ujenzi wala Mhe John Magufuli mwenyewe aliyewasiliana na Wizara ya Ardhi ili itimize wajibu wake wa kuhifadhi eneo hilo kwa mujibu wa sheria? Kitendo cha Magufuli kuwatuma wafanyakazi wa TANROAD kuweka alama ya X katika nyumba zilizoko katika upana wa MIta 8 kimekiuka sheria, tena alizojitungia mwenyewe?.
Ibara ya 27 (3 na 4 ) inamataka Waziri wa Ujenzi baada ya kufanya mawasiliano na Waziri wa Ardhi atahakiksha ananunua ardhi hiyo kutoka kwa wananchi hao. Je Mhe John Magufuli alifanya hivyo? Badala yake Mhe Magufuli alitumia ubabe na kuwatuma kwa lazima na vitisho vya kufukuzwa kazi wafanyakazi wa TANROAD kuvamia nyumba za wananchi na kuweka alama za X katika Mita 8 zilizoongezeka 2009, huku kulikuwa ni kukiuka sheria ya barabara.
Ibara ya 27 (5) inatamka kuwa baada ya siku 60 tokea wananchi kulipwa fidia Wizara wa Ujenzi kupitia TANROAD atawataka wananchi husika kuhama au kutoendeleza chochote. Je wananchi ambao nyumba zao zilizowekewa alama za X wamewahi kuarifiwa chochote na Wizara ya Ardhi, sembuese kulipwa fidia? kwakuwa wananchi walioko ndani ya Mita 8 hawajalipwa fidia hawakutakiwa kubughudhiwa kwa lolote hadi hapo watakapokuwa wamelipwa fidia. Na Magufuli anafahamu hivyo ndio maana alijibu hivyo bungeni, lakini akafanya tofauti alipotoka bungeni.
Ibara ya 27 (6) inatamka kuwa baada ya wananchi kuarifiwa kuhusu ardhi hiyo kutwaliwa na Serikali watalipwa fidia. Kwa kuwa hakuna fidia zozote zilizolipwa ndio maan Waziri Mkuu Pinda na Raisi Kikwete wakamkaripia.
Kwa hali hii ni lazima tukubaliane kuwa Mhe John Pombe Magufuli ni mbumbumbu wa sheria, aidha ameshindwa hata kutafsiri na kutekeleza sheria alizojitungua mwenyewe. Je atawezaje kutekeleza sheria zingine?
Kwa hali hiyo Mhe JohnPombe Magufuli alistahili kufukuzwa kazi kwa kukiuka sheria za barabara na kuiletea aibu serikali.