Kikwete na miujiza ya siasa nchini Tanzania inayomgharimu Lowasa

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,781
2,000
Jamii za kiafrika zamani ilikuwa nikwamba mababu zetu na bibi zetu wakioana kama wamependana vyakutosha walikuwa wanakunywa dawa maalumu ya kulinda upendo wao, ilikuwa nijambo lenye fahari na tunu imara kwa mwafrika wa kweli achana na kizazi hiki cha nyoka kilichobemendwa na ccm maslahi.

Dawa hiyo ilikuwa na nguvu kubwa mpaka ahera kabisa, ilikuwa ni ama Baba akifa ni lazima bibi afute siku hiyo hiyo au wiki hiyo hiyo, kwahakika msiba ulikuwa ni maajuza wawili utake usitake, hiyo ndio nguvu ya dawa hiyo ya kulinda penzi la wazee wetu.

Lowasa aliwahi kuuambia ulimwengu kuwa yeye kala nadhiri na Kikwete, kwamba wale wanaosema wanaugomvi nikuwa hawaelewi tu kuwa Lowasa na Kikwete hawakukutana barabarani. Kwa lugha nyingine nikuwa wawili hawa wamekunywa dawa ya u boys 11 Man, akifa Kikwete basi jiandaeni kuzika na Lowasa kabla hata ya kuanua matanga Musoga.

Hivi ndivyo ilivyo, Kikwete ameugua kansa ya kizazi alimaarufu tezi dume na kufanyiwa upasuaji mkubwa uliokwenda salama salmini,
Sasa Edward Lowasa yuko ujerumani kutibu kansa ya kibofu kwa upasuaji.

Hiyo ni kazi ya dawa hiyo, mambo ya viapo ya urafiki usiokufa hata mmoja aende kaburini basi na mwingine atamfuata huko huko. Viapo hivi hata Ibrahim aliwekeana viapo na Mungu, Musa pia aliwekeana viapo na Mungu alipokwenda kuwaokoa wana wa Israel.

Haijulikana kama Samweli Sitta nae aliwekeana viapo, lakini sasa anapanga kutangaza rasmi kuwania urahisi mara atakapo lamba nishani yake kesho siku ya uhuru.

Bila shaka ni nishani kwa kufanikisha katiba ya uchakachuaji.

Mambo ya viapo vya wanasiasa na gharama ya waendako.

Kwaviapo vyao aminini ccm hawana njia nyingine bali ni kutii viapo vya mabwana hawa wawili waliokula yamini kuachiana urais wa Wadanganyika.

Uhuru wa Tanzania upo chini ya Mtanzania mwenyewe.

CCM yatafuna nchi!!!
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
Nijuavyo mie ni kwamba Lowasa ni fisadi tena aliyekubuhu. Huwezi kumfananisha na rais Kikwete
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Mburula mwingine huyu ukisoma alichoandika utadhani mwanasesele,ukawa bana.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
Kwa hiyo Kikwete hajakubuhu sana kuliko Lowassa! Lowassa kamzidi kidogo mwenzie au! Basi sawa!
Kikwete hana utajiri wowote. Lowasa kakwiba mpaka Watanzania tunaona kinyaa kusikia jina la huyu fisadi likitajwa
 
engijape

Senior Member
Nov 8, 2014
168
225
wewe ulidhibitisha wapi ufisadi wa Lowassa na uaminifu wa Rais wetu. Huwezizuia haki ya mtu kwa vyovyote vile. KAMA MUNGU ALIPANGA LOWASSA KUWA RAIS WA NCHI HII ATAKUWA NA SII WEWE KUMWITA FISADI. KISA KWENU MASKINI NA WENZAKO UNATAKA WAFANANE NA WEWE NA UKOO WENU? UTAANGAIKA SANA NA NJAA ZAKO. FANYA KAZI ACHA KUNG'ANG'ANIA HOJA YA UFISADI ILIYOPITWA NA WAKATI. VIJANA KAMA NYIE HAWAFAI KWA MAENDELEO YA TAIFA HILI. HAMNA VISION NA WALA NDOTO NA PICHA YA BAADAYE YA WATANZANIA. HAKUNA ASIYEKUWA NA HAKI YA KUWA RAISI WA NCHI MAADAM ANA UWEZO KISHERIA. WEWE NI NANI UWAHUKUMU WENGINE NA KUWAKUBALI WENGINE.
 
OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,945
1,225
Jamii za kiafrika zamani ilikuwa nikwamba mababu zetu na bibi zetu wakioana kama wamependana vyakutosha walikuwa wanakunywa dawa maalumu ya kulinda upendo wao, ilikuwa nijambo lenye fahari na tunu imara kwa mwafrika wa kweli achana na kizazi hiki cha nyoka kilichobemendwa na ccm maslahi.

Dawa hiyo ilikuwa na nguvu kubwa mpaka ahera kabisa, ilikuwa ni ama Baba akifa ni lazima bibi afute siku hiyo hiyo au wiki hiyo hiyo, kwahakika msiba ulikuwa ni maajuza wawili utake usitake, hiyo ndio nguvu ya dawa hiyo ya kulinda penzi la wazee wetu.

Lowasa aliwahi kuuambia ulimwengu kuwa yeye kala nadhiri na Kikwete, kwamba wale wanaosema wanaugomvi nikuwa hawaelewi tu kuwa Lowasa na Kikwete hawakukutana barabarani. Kwa lugha nyingine nikuwa wawili hawa wamekunywa dawa ya u boys 11 Man, akifa Kikwete basi jiandaeni kuzika na Lowasa kabla hata ya kuanua matanga Musoga.

Hivi ndivyo ilivyo, Kikwete ameugua kansa ya kizazi alimaarufu tezi dume na kufanyiwa upasuaji mkubwa uliokwenda salama salmini,
Sasa Edward Lowasa yuko ujerumani kutibu kansa ya kibofu kwa upasuaji.

Hiyo ni kazi ya dawa hiyo, mambo ya viapo ya urafiki usiokufa hata mmoja aende kaburini basi na mwingine atamfuata huko huko. Viapo hivi hata Ibrahim aliwekeana viapo na Mungu, Musa pia aliwekeana viapo na Mungu alipokwenda kuwaokoa wana wa Israel.

Haijulikana kama Samweli Sitta nae aliwekeana viapo, lakini sasa anapanga kutangaza rasmi kuwania urahisi mara atakapo lamba nishani yake kesho siku ya uhuru.

Bila shaka ni nishani kwa kufanikisha katiba ya uchakachuaji.

Mambo ya viapo vya wanasiasa na gharama ya waendako.

Kwaviapo vyao aminini ccm hawana njia nyingine bali ni kutii viapo vya mabwana hawa wawili waliokula yamini kuachiana urais wa Wadanganyika.

Uhuru wa Tanzania upo chini ya Mtanzania mwenyewe.

CCM yatafuna nchi!!!
Mkuu katika maandiko yako yote hili ni la ovyo kuliko......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom