Kikwete na mbinu ya kutumia mashehe na media | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na mbinu ya kutumia mashehe na media

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Plato, Jun 8, 2011.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Leo naona media zinatetea upupu wa blahblah za kikwete kugeneralize viongozi wa dini na dawa za kulevya.huyu shehe basalehe Anapayuka.nzowa anabwabwaja tu.mwandishi haulizi maswali magumu.mfano sakata la mtoto wa mengi,dawa zinazopotelea police,kikwete kutotaja wauzaji wakati anawajua.anauliza maswali ya kijinga ili kikwete atetewe.pumbafuu
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  wenye fikira finyu huwa na mawozo finyu na hoja finyu. KWANINI RAIS AKWENDA MSIKITINI NA KUTOA HOJA HIYO?
   
 3. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wawadanganye wajinga, lakini janja yao yote inajulikana hizombinu chafu. watanzania wa leo si wa miaka ya 47
   
 4. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nimeangalia pia hawa Watu sijui wanatupeleka wapi!!Najiuliza hawa wanaotumika kwenye vyombo vya Habari je serikali inahusika moja kwa moja kuwatuma au nikujipendekeza tu kwa hawa Watu?Kama Serikali inawatuma ukweli nikwamba hawaitakii híi Nchi mema kwakuliingiza Taifa kwenye udini na watajibu wakituingiza kwenye machafuko coz kwakufanya hivyo badala yakusolve tatizo wao ndo wanalikuza haiingii akilini maneno yamesemwa na Rais katika shughuli ya Wakristo kwamba viongozi Wadini wanajihusisha na Biashara ya madawa yakulevya katika context hii Wakristo ndo walengwa kwakuyatumia Mazingira,Wakristo wanataka kuwajua hawa viongozi coz hii ni Biashara haramu na inadhalilisha Ukristo hapa anajitokeza Shekhe anatetea huku akidai kauli ya Rais ililenga Dini zote,je anaweza thibitisha?Huu ndo udini tunaouöngea unaopandikizwa na viongozi wetu.
   
 5. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimeangalia nikagundua kuwa ni mkakati uliopangwa.kwa nini chanel 10 wamemualika sheikh pekee badala ya kualika viongozi wa dini zingine pia?!suala la nzowa kupewa rushwa na YM kutaka kumpakazia mtoto wa mengi hajaulizwa!!na mengine mengiiii...eti anasema suala la kukamatwa madawa pale kabuku alitaka kuhongwa bilioni 1 au 2 lakini akakataa...jamani nzowa akatae bilioni 2 kweli?!!kama alikubali kupewa milioni 40 sembuse bilioni 2?!!!AACHE KUTUDANGANYA PAMBAAAAF!
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe ndiye hujaelewa na kufuatilia hotuba halisi ya kikwete umetegemea media na ndio maana imekuwa rahisi kwako kupotoshwa. Rais alizungumzia wimbi la madawa ya kulevya nchi na hatari yake kwa taifa letu na kisha akaomba msaada kwa viongozi wa dini katika mapambano ya dawa za kulevya lakini mwisho alisema baadhi ya viongozi wa dini wameanza kuvutiwa na bishara hiyo.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Binafsi naamini Rais anaweza kuwa na taarifa za kiintelijensia ambazo hazijakamilika au ziko kwenye ngazi ya upepelezi, naona jambo hili linawezekana na anaweza kujiepusha kutaja majina mapema lakini sio kosa kuifahamisha jamii kwamba taarifa za awali za kiuchunguzi zinaonyesha kwamba baadhi yao viongozi wa dini nao wameanza kuvutiwa na biashara halamu ya madawa ya kulevya. Masheikh, maasikofu,maimam na wachungaji ni binadamu kama sisi na wanaweza kutumbukia zambini kama tulivyo sisi sote.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tukumbuke Rais Noriega alivyojihusisha na madawa ya kulevya na kukamatwa na marekani kwa sasa anatumikia kifungi jela. Madawa ya kulevya hayaangalii nafasi ya mtu lakini pia ni hatari sana kutaja majina ya watu kama hutakuwa umekamilisha kupata ushahidi na vielelezo vya kutosha kuambatisha mbele ya mahakama. Sheria iko wazi mtu akifungua kesi ya kudhalilishwa serikali inaweza kulipa fedha nyingi kama fidia hivyo kila jambo linatakiwa kuenda kwa hatua zenye kukidhi haja na hadhi ya sheria.
   
 9. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kwakeli hali ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ni kazi ya wananchi wote wenye nia njema na taifa hili, lakini hofu yangu ni pale ambapo Mkuu wa nchi anaamua kusema na dhahiri kuonyesha kuwa "ninyi pia mnavutiwa na biashara hii", inamaana kuwa kwa mujibu wa intellignce information anakuwa na uhakika wa anachokisema dhidi ya wale aliowaonyesha kuwa wanajihusisha na madawa hayo, ikiwa mapambano yanaendeshwa kwa kuficha washiriki hatutafika mbali, kwa hiyo binafsi nampongeza Rais lkn bado hajawa wazi na kutokana na uficho alioweka ndio maana "Maaskofu" wameamua kumwambia Mh. Rais awataje wanaohusika ktk biashara hiyo hasa viongozi wa dini, ikiwa kama sisi tunapata taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu kauli ya Kikwete inakuwaje wewe unayesema kuwa "tumedanganywa na vyombo vya habari?"wakati sisi sote na wewe pia unategemea habari kutoka ktk vyombo hivyo, kwa bahati mbaya tena "Channel Ten kwa busara zao waliamua kumuita Muislamu tu ili atoe mawazo yake juu ya kauli ya Rais na akasema kauli ile ililenga dini zotee.......loooooooooh""""
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Rais akiwa mwanasiasa na sio mwanasheria hazuiwi kusubiri mpaka jambo litakapoharibika ndipo atoe tahadhari kwa taarifa kwa jambo ambalo halijakamilika kiupepelezi lakini linaonyesha dhahiri athari zake mbele ya safari. Yeye ndiye dereva wa taifa hili, hazuiwi kuendesha basi tulilopanda na kutuambia tukifika mikumi kuna wanyama wakali tuombee tufike salama na haitakiwa mtu kushuka. Hii haina maana kwamba dereva anajua au ni lazima kwamba mmoja wa abiria ataliwa na wanyama.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Labda tujiulize swali je hapa nchini tangu uhuru hakuna kiongozi wa dini aliyewahi kukamatwa na madawa ya kulezwa, kubaka, kulawiti au ujambazi?????????? kama inawahi kutokea basi viongozi wa dini sio miungu ni binadamu kama sisi.
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Wana JF tusiumize vichwa vyetu kufikiria haya mambo.Kifupi ni kwamba huu ni mkakati wa kumpata mrithi wa kikwete uchaguzi 2015;kwa kujikumusha someni hiki kipande cha habari toka RAIA MWEMA TOLEO NO.188 la 1-7 june2011.Tafadhali read between the lines;
  Wagombea wa Kikwete 2015

  Kwa kufuatilia mambo ya kisiasa yanavyokwenda na jinsi Rais Kikwete anavyoendesha mambo yake, kuna majina mawili ya watu wanaotajwa ambao angependa wachukue urais na umakamu wa rais wa Muungano mwaka 2015. Hii inatokana pia na imani yake kwamba Katiba mpya haitabadili mfumo wa sasa.
  Sababu kubwa ni mbili: Kwanza, kutekeleza ahadi yake ya siri kwamba hawezi kuacha nchi kwa Mkristo; na pili, kuhakikisha uongozi mpya unamlinda yeye na familia yake dhidi ya misukosuko ya hapa na pale ambayo kawaida kote duniani hutokea mtu akishaacha urais. Hakika, naye hatapenda kushambuliwa kama inavyotokea kwa Mkapa.
  Baada ya kufanikiwa kuwaengua pembeni Lowassa na Membe (Prof. Mwandosya kanusurika?) ni nani, basi, ambaye Kikwete anamtaka kwa urais wa 2015 na atachezaje karata zake kuhakikisha jina la mtu huyo linapeta?
  Ili watu hao wawili anaowataka wakubalike, inaaminika kuwa Kikwete atatumia mtindo ule ule wa funika kombe mwanaharamu apite. Atawapendekeza kwa kutumia vigezo vinavyoficha ukweli. Kutokana na hali ya kisiasa itakavyokuwa, anaweza kusema: "Jamani ni zamu ya wanawake sasa, tusitawale akina baba tu, nchi yetu wote."
  Iwapo wazo hili litakwama, basi, Kikwete anaweza kusema hivi: "Jamani sasa wenzetu wa Zanzibar nao, miaka 20 imepita, tuwape nao nafasi jamani." Msemo huu, hata hivyo, hauna mashiko iwapo Katiba haitakuwa na agizo hilo; kwani upande wa Upinzani unaweza kuweka wagombea wote wa Bara. Mbinu hiyo Kikwete ameshawahi kuitumia kwenye kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana ambapo alimpendekeza kijana wa Visiwani, na pia aliitumia kwenye kupata jina la mgombea wa uspika. Anaamini kuwa mbinu hiyo itasaidia kufunika hoja yake ya udini isionekane, na hivyo kufanikisha kupata rais Mwislamu.


  Asha-Rose Migiro na Dk. Mwinyi
  Katika miaka ya karibuni Kikwete amekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na mwanamama mmoja ambaye kila baada ya miezi michache hufika Ikulu, na kisha picha nyingi hupigwa kuonesha kwamba wawili hao wanaelewana na wanashirikiana kisiasa pia.
  Huyu ni mwanamama ambaye ni mmoja wa wanasiasa wachanga waliofaidika na vyeo vya uwaziri wa Kikwete mwaka 2005. Aidha, pale Tanzania ilipopewa mwanya wa kutoa jina la mwanamke wa kushika nafasi ya juu kimataifa, Kikwete hakusita kumtaja mwanamama huyu.
  Nafasi hii ilikuwa baada ya Tanzania kufanya kampeni kubwa barani Afrika kuunga mkono jina la Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Ban ki-Moon, kwenye kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
  Mwanamama huyo pia ana kisomo kizuri kinachokubalika na kinachoweza kuwaaminisha watu wanaotaka kuuliza maswali kuhusu uwezo wake kiutendaji wa kuiongoza nchi yenye matatizo ya uchumi na yenye mipasuko kibao kama Tanzania. Mwanamama huyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye anaelezwa kuanza kujiandaa kurejea nyumbani Tanzania siku si nyingi.
  Kwa upande wa Zanzibar, ni waziri mmoja kijana ambaye urafiki wake na Kikwete huwashangaza viongozi wengine wa Zanzibar; mathalani jinsi wanavyosalimiana kama watoto wa mjini. Katika mtandao wa YouTube Watanzania waliweka picha ya video ya Kikwete akisalimiana ‘kishkaji' na waziri huyu kwenye Uwanja wa Amani, Zanzibar siku ya Januari 12, mwaka huu. Picha hiyo iliibua gumzo kubwa. Hivi karibuni Waziri huyu alipokabiliwa na msukosuko wa kutakiwa na wananchi kwamba ajiuzulu ambao kimsingi ulisababishwa na utendaji dhaifu wa Jeshi la Wananchi uliochukua maisha ya watu kwenye milipuko ya maghala ya silaha, alikataa na Kikwete hakusema kitu. Huyu ni Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi.
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hakwenda msikitini kwakuwa wenye msikiti ndio waliomtuma akataint madhabahu. Ukumbuke tu kuwa wkt wa kuomba urais 2005 aliahidi kuwatumikia waislam na ukumbuke kuwa amewaahidi mahakama ya kadhi ni OIC. BTW: huwa naishia kusikia na kuona kgs kadhaa zimekamatwa sijasikia zikiteketezwa- hivi sasa tuna toni ngapi za madawa ya kulevya.
   
 14. frozen

  frozen Senior Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayepinga kwamba viongozi wa dini ni binadamu kama wengine, shida ni unafiki wa msemaji, tangia mda mrefu alisema anafahamu wahusika wakuu wa dawa za kulevya nchini,mbona hawataji wachukuliewe hatua?badalayake ana bwabwaja tu kila siku.haeleweki
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nina wasiwasi sana na strategies anazotumia Rais Kikwete kuongoza Taifa. Anaonekana kutumia mbinu za kizamani mno bila kuzingatia zama tunazoishi. Tuko kwenye karne ya science & technology, zaidi ya nusu ya wananchi anaowaongoza Kikwete wana umri chini ya miaka 20! na uelewa wao ni mkubwa kulinganisha na kipindi yeye rais alipokuwa let's miaka 18. Hii tabia ya watu fulani fulani kuwa kama tarumbeta lake itamletea matatizo. Huyo shehe aliyeenda channel ten ana ujuzi gani kuhusu madaya ya kulevya? yeye yuko kwenye kamati ya kutokomeza madawa ya kulevya? anatoka ufisi hata ya mufti au Bakwata? Kwa nini yeye?
   
 16. T

  The GreatMwai Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh!!! Kwani wewe umeshaanza kuuza madawa ya kulevya?
   
 17. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tutajenga hoja sana kumtetea rahisi kikwete. Lakini tukubaliane kimsingi ya kuwa rahisi wetu hana busara. Angeweza kusubiri siku ya kuadhimisha athari za madawa ya kulevya ndipo akatoa kauli yake, tena kwenye mkutano wa hadhara. Hapo ndio viongoz wa dini zote wangekuwepo na wote wangelengwa na kauli hiyo. Pale kanisan hapakuwapo na mashehe ambao wanaonekana kushadidia na kutetea kauli hiyo. Natoa wito kwa viongoz wa dini hasa wakristu, kutomwalika rahisi huyo ktk hafla zenu kwani hana busara wala hekima. Jueni ya kuwa mtu huyu hawapendi na anaamiki kupotea kwa umaarufu wake na chama chake ni kwa sababu yenu. Ukweli wenu mnaousema juu ya tanzania unatafasiriwa kama udini. Endeleeni kuusema ukweli huo. Watu wa nchi hii ni masikin sana, fedha zinaibwa kila kukicha na maovu mengi.
   
 18. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wewe ndio hujafuatilia alisema 'baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na madawa ya kulevya na akasema baadhi yao amewakamata" ndo maana wanataka ataje....tatizo kikwete anaropoka bila research au inawezekana wasaidizi wake ni mazezeta vile vile,probably hata wewe unayetetea upuuzi huu upo naye
   
 19. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wauza madawaya kulevya ni viongozi wakuu serkalini,makanisani misikitini na wafanyabiashara wakubwa.
  tushikamane pamoja kwani hata rais hayuko salama sana na hii biashara kwa sababu ya marafiki zake.
  wanaoharinikiwa ni watoto wetu, wa kikwete na wateule wenzake hawahusiki.
  kwa jumla serikali ya ccm ndiyo iliyobariki hii biashara kwa kuruhusu biashara na siasa kufunga ndoa.
  ni hayo tu.
   
 20. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Swali hapa ni je kusudi hasa la rais kusema hili, wakati na mahali aliposema lilikuwa ni nini? Tunahitaji watu wanaotumia vichwa vyao kufikiri kabla ya kutamka na mdomo!!!
   
Loading...