VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Walivyoanza ni sawa. Matumaini ya wananchi juu yao ni makubwa. Wote wana mbwembwe katika kusema na kutenda. Mabaraza yao ya Mawaziri yalitangazwa kwa msisitizo kana kwamba hakukuwa yeyote mwenye makandokando.
Waziri Mkuu wa Kikwete alikuwa Lowassa. Waziri Mkuu wa Rais Magufuli ni Majaliwa. Alipoingia tu kazini, Lowassa alizunguka nchi nzima kwa ziara za kupangwa na kushtukiza. Aliwapelekesha watendaji kila alipopita na kuwatimua walioonekana hawafai. Na Majaliwa anayarudia ya Lowassa. Njia moja.
Lowassa hakumaliza harakati zake. Itakuwaje kwa Majaliwa? Rais Mstaafu Kikwete alibadili Katibu Mkuu Kiongozi. Naye, Rais Magufuli amebadili katibu Mkuu Kiongozi. Marais wawili, njia moja. Na hata ushindi wao uchaguzini ulisemwa sana. Ni mambo ya kawaida ya kisiasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam