Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,450
- 12,316
Kwa picha hiyo jinsi inavyoonekana, inaonekana mzee wa mamvi na JK watakuwa 'wamecompromise' ili ampigie debe ili apeperushe tiketi ya CCM kwa nafasi ya Urais mwakani.Bila shaka hii picha itakupa majibu ya maswali uliyo kua nayo kichwani mwako.....yetu macho na masikio kuelekea octoba 2015.
Kwa msaadawa watu wa Marekani kitu kipo!hamna kitu apo
Kwa msaadawa watu wa Marekani kitu kipo!
TB JOSHUA yule aliyewatoa watu kafara au ni mwingine ninayemjua!labda TB JOSHUA
Hakuna kinachoshindikana chini ya jua kwenye utawala wa Kikwete - Hata FaizaFoxy anaweza kuteuliwa kua balozi wa Tanzania nyumba 10/10 nchini China!Tushije kushangaa pia JK akatufanyia surprise ya mwaka, pale atakapomteua mzee wa mamvi kuwa PM mpya, akimreplace mzee wa kutoa machozi!
Ukifuatilia kauli ya Sefue kuwa ripoti ya maazimio ya bunge wameipokea Ikulu, hata hivyo vyombo vya uchunguzi vinaendelea kuchunguza, ili ikibidi kuwaclear baadhi ya watuhumiwa na kuwatumbukiza ndani ya hiyo skandali, wengineo ambao hawakuguswa na maazimio yale manane ya bunge!
Siku 7 zijazo zinaweza kuleta kishindo kikubwa sana cha kisiasa hapa nchini!
Teheeeeteheeee...... Mkuu hapo umeua...Hakuna kinachoshindikana chini ya jua kwenye utawala wa Kikwete - Hata FaizaFoxy anaweza kuteuliwa kua balozi wa Tanzania nyumba 10/10 nchini China!
Ni protocol ipi iliyoandaa kiti pembeni ya Raisi akae pembeni na Lowassa? - Kumbuka ule usemi wa Lowassa MIMI NA KIKWETE HATUJAKUTANA BARABARANI!
Kwa picha hiyo jinsi inavyoonekana, inaonekana mzee wa mamvi na JK watakuwa 'wamecompromise' ili ampigie debe ili apeperushe tiketi ya CCM kwa nafasi ya Urais mwakani.
Hilo likitimia watanzania tutakuwa tunakumbushwa kauli iliyowahi kutolewa na EL wakati ule wa sakata ya Richmond, pale aliposema kuwa yeye na JK hawajakutana barabarani!
JK naye akamjibu mzee wa mamvi kuwa asiwe na wasiwasi kwani historia itamtendea haki na ipo siku yeye EL atakuwa 'huru' kutokana na skandali hiyo ya Richmond!
Nilikaa jukwaa kuu leo sherehe inaanza hadi mwisho,hakuna eneo ambalo JK na EL waliweza kusimama karibu hivyo Zaidi ya salamu tu - tena JK alitaka kumpita EL bila kumpa Mkono isipokuwa alifanya kulazimishwa, anyway angalieni hiyo Picha yenu vizuri mbona EL hana miguu?Hivi hiyo picha ni ya leo leo pale uwanja wa Taifa?
Nauliza hivyo, kwa kuwa taarifa zilizokuwa zimesambazwa mitandaoni, tuliambiwa EL, yupo Ujerumani ambako alikuwa amelazwa hospitalini, akiwa katika 'coma' baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.
Kwa hiyo wenye taarifa 'deeper' (msamiati wa Sefue) tunaomba mtujuze.