Kikwete na kikao cha mawaziri Dodoma! Serikali yatikiswa na mtukio? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na kikao cha mawaziri Dodoma! Serikali yatikiswa na mtukio?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  • Mnyika: Kikwete ni dhaifu, serikali ni dhaifu.
  • Bajeti vurugu tupu
  • Mgomo wa Madaktari
  • Jaribio la Kumwua kiongozi wa Madaktari - Ulimboka
  • Mabilioni ya fedha yanayomilikiwa na vigogo serikalini yafichuliwa Uswiss.
  • Chadema wazidi mtandao nchi nzima
   
 2. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanx keep on updating us comrade
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizi agenda umezipata wapi?
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu ataacha kucheka Cheka Kama bulicheka
   
 5. cement

  cement JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Dah imebidi aingilie kati maana hali ni mbaya!
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  amekimbia ikulu tu. Kaona kitanuka
   
 7. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  wewe meza acha kuuliza JF ni zaidi ya wewe uijuavyo
   
 8. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuirudisha ccm madarakani ni janga la taifa! - Dr. Wolbroad Slaa 2010
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilimeza ya simbachawene mwishoni ikawa sumu mkuu kwi! Kwi! Kwi! Kwi ha ha ha lemutuz
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  imekula kwao. Madhaifu hayo. Oovyo
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani Dhaifu si alishawahi kukutana na Ma-Dr Ikulu na kuwapa ahadi za kimagumashi? Leo anakwenda kuwaambia nini Madhaifu wenzake? Ana jipya kweli? Nchi ilishamshinda aende tu akawe ngariba jandoni.
   
 12. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Anakufa maji huyo
   
 13. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kikwete=pinda=ccm=janga la kitaifa
  Narajia madudu leo
   
 14. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  mkuu hii issue ya ma dr. Inaweza kuwaingiza manesi ktk mgomo!
   
 15. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hakuna jipya! Baada ya hapo utasikia anakurupuka kuwahutubia wazee wa Dar es salaam! Ndizo zake hizo. Tusubiri tuone!!!
   
 16. D

  Detector New Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unauliza nini wakati Mawaziri wenyewe wamo humu humu JF.....?
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huyu KJ inabidi atahiriwe kwa shoka maana uvundo wake unanuka!
   
 18. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kauli ya "liwalo na liwe" ni nzito sana na imetolewa na kiongozi wa ngazi ya juu sana. Nahisi wamemwambia afute kauli hiyo amegoma na serikali haikujiandaa kwa lolote na pengine si maazimio ya serikali, sasa ndo wanatafakari nini wafanye!
  Ee Mungu wapunguzie maumivu wagonjwa wote wakati madaktari wakikaza kamba.
   
 19. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kikwete si dhaifu tu, ni dhaifu sana


  [​IMG]

  • [​IMG]  Ingawa mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) aliposema rais Jakaya Kikwete ni dhaifu alitolewa nje ya bunge hivi karibuni, ukweli unabaki pale pale kuwa Kikwete ni dhaifu tena sana. Leo sitazungusha mjadala huu ili kuepuka kumchosha msomaji.
  Nitaanza kumuunga mkono Mnyika kuwa Kikwete ni dhaifu tena sana kwa sababu za kisayansi zifuatazo:

  Mosi anapenda kukwepa majukumu yake na kwa kupenda kusafiri hovyo hovyo na kutumia pesa yetu hovyo. Rejea alivyokimbilia Davos Uswisi wakati wa mgomo wa madaktari uliogharimu maisha ya watanzania wengi wasio na hatia zaidi ya kumchagua yeye.

  Pili ni mwoga kuchukua maamuzi kwa mfano, kama si bunge kumtimua waziri wake mkuu wa zamani ambaye pia ni mshirika wake, Edward Lowassa asingeweza kufanya hivyo. Rejea alivyokuja na mkwara wa kujivua gamba. Alipotolewa ukali na Lowassa na watuhumiwa wengine kama Andrew Chenge aliishia wapi kama siyo kuchomoa hoja kinamna huku akiendelea kuaibika na kuonekana wazi alivyodhaifu.
  Tatu, hakushindwa tu kuwawajibisha akina Lowassa, ameendelea kumlipa Lowassa pesa ya ustaafu ambayo hastahili. Pia Kikwete ameshindwa hata kumkemea Lowassa kuacha kukigawa chama kwa matamshi yake yenye kupingana na maazimio ya chama chake. Ameunda chama ndani ya chama kupitia mtandao wake. Rejea, kama mwenyekiti wa chama chake, kumtumia Nape Nnauye kuwananga akina Lowassa na baadaye kuchomoa na kumwacha Nnauye na maadui wa kuundiwa na Kikwete
  Rejea kuwahi kudaiwa kuridhia ongezeko la posho ya wabunge, Kwa udhaifu wake umma ulipokuja juu akawatupia mzigo waziri mkuu Mizengo Pinda na spika Makinda

  Nne Kikwete si msafi kimaadili maana alitajwa wazi wazi kuwa urais wake ulitokana na wizi wa EPA uliotikisa uchumi wetu ambao Kikwete hajawahi kutolea maelezo wala kujitetea. Ukitaka kumpa taabu Kikwete mtajie wizi wa EPA. Nimeshaandika mara nyingi juu ya hili na kilichofanyika ni kwa watu wa Kikwete mara kutishia gazeti kwa kutafuta kasoro ndogo ndogo bila mafanikio. Na hili limemfanya Kikwete ashindwe kupambana na ufisadi kwa sababu naye ni sehemu ya tatizo ukiachia mbali kuwa mshirika mkuu. hii ndiyo sababu iliyomfanya ashindwe kuwachukulia hatua mawaziri walioboronga akina Ibrahim Msabaha (Bangusilo), Nazir Karamagi na wengine waliotimuliwa kutokana na shinikizo la bunge ambalo siku hizi limegeuka nyumba yake ndogo baada ya kuwa na spika asiye na udhu wala uchungu na nchi kama ilivyokuwa kwa mzee wa viwango.

  Tano, Kikwete hupenda kufanya mambo yasiyo ya muhimu kuwa muhimu na ya muhimu kwa ya hovyo. Rejea alikvyowenda Brazil mwezi Aprili mwaka huu kwenye mkutano wa maendeleo ya kiuchumi akaishia kupoteza muda mwingi na aliyekuwa kocha wa mpira wa miguu, Maxio Maximo.
  Sita Kikwete tangu aingie madarakani ameanzisha na kulea mitandao ambayo licha ya kukigawa chama imekidhoofisha hata kumdhoofisha Kikwete mwenyewe. udhaifu huu umetumiwa na watu mbali mbali kuanzia mkewe hata mwanae kujihusisha na siasa hata kwa kuonyesha mgongano wa maslahi wa wazi kati ya ikulu na umma.

  Sita, Kikwete anasifika kwa kuwa rais aliyeshuhudia kudhoofika kwa uchumi tokana na mipango, usimamizi na matumizi ya hovyo. ni rais aliyesimamia serikali inayofanya mambo kiholela kiasi cha kuonekana kama mhimili wa ubadhirifu. Ameshindwa kusimamia uchumi kiasi cha kushindwa hata kuangalia raslimali kama madini na wanyama. Kutokana na hili Kikwete ameshindwa hata kutangaza mali zake ajabu serikali yake eti inawataka watumishi wa umma kutangaza mali zao wakati mkuu wake anaendelea kujifanya hili halimhusu!

  Saba, kushindwa kusimamia na kuimarisha muungano. Rejea kuendelea kuwa kimya wakati taifa likikabiliwa na changamoto ya Uamsho. Je Kikwete anawaunga mkono uamsho nyuma ya pazia kama ilivyokuwa mihadhara wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi aliyefuga kila aina ya kashfa kwa jina la mihadhara?

  Nane, ukimya. Rejea Kikwete alivyokaa kimya wakati wa mgomo wa madaktari kiasi cha kumuachia mzigo waziri mkuu huku yeye akikwepa lawama na kusubiri kusifiwa kama tatizo lingetatuliwa. Hata madaktari wanapotishia kugoma tena bado Kikwete ni kama hayupo wala hili halimhusu. Baba gani anaacha mambo yaharibike ndipo atoe sauti yake? Pia ukimya wa Kikwete unaweza kuuona kwenye mgongano baina ya taarifa zinazotolewa na watendaji wake. Kila mtu anasema lake na hakuna anayewajibika. Rejea maneno ya waziri wa mambo ya Nchi za Nje Bernard Membe alipoamua kuwamwagia sifa CHADEMA kuwa wajiandae kuingia madarakani huku waziri wake Stephen Wassira akisema vingenevyo.

  Tisa, Kikwete ni dhaifu sana katika kutoa maamuzi. Makala ya wiki jana niliongelea uteuzi wa hovyo. Hata baadhi ya mambo anayofanya kama kubembea alipokwenda nchini Jamaica ni vitu ambayo vingeweza kuepukwa kama rais angekuwa jasiri.
  Ukiachia Hilo hata baadhi ya maamuzi kama kuunda mikoa na wilaya mpya wakati uchumi wetu uko taabani ni ushahidi kuwa rais wetu ni dhaifu sana.
  Kumi, Kikwete ni mgumu wa kujifunza. Rejea kurudia makosa yale yale karibu kila mwaka. Kwa mfano ripoti ya kila mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa pesa za Serikali (CAG) imekuwa ikionyesha wizi wa kutisha kwenye mawizara na serikali za mitaa. Kikwete hajawahi kuchukizwa na hili na kutoa tamko hata karipio.
  Ukiamua kuandika udhaifu wa Kikwete wote, unaweza kujaza kitabu. Kwa leo tunaishia hapa kwa kuungana na mbunge Mnyika kuthibitisha udhaifu wa rais Kikwete.
  Chanzo: Tanzania Daima Juni 27, 2012.
   
 20. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu Kumbe hata ile skendo ya simbachawene ndiye aliye iandika mwenyewe
   
Loading...