Ukimchukia mtu kwa mapungufu yake, usingependa kuona anapata hata sifa kidogo kwani katika siasa mafanikio kidogo ya mtu ni kona ya maficho kujisahaulisha na ubaya wa utendaji wa mwanasiasa husika. Leo nataka kuandika kitu ambacho mimi nimekiona na kushuhudia historia ya nchi yetu na wapenzi wa ukuaji wa tasinia ya habari na demokrasia ya uvumilivu hawapendi kukumbuka na kutukuza.
Nikiwa nimekaa nilipata ndoto ya mchana kwa kufikiri kuwa hivi Rais Kikwete atawachia nini Watanzania baada ya kipindi chake kupita, Nyerere alituachia nini, Mwinyi alituachia nini na Mkapa akawapa zawadi gani watanzania? Maswali haya ni ya kitaaluma na yanahitaji kujibiwa kwa kitabu kwa kila kiongozi, na nafikiria kuishauri serikali kufanya mambo mema waliofanya viongozi hawa wanne kuwa nguzo ya kujenga maadili ya utaifa wetu. Ni budi tuwekeze na kunyambulisha vizuri. Kwa kifupi niyafupishe ifuatavyo:
Nyerere ni baba wa utu, umoja na usawa katika taifa hili na siku zote mapungufu yake yamemezwa na sifa hizi alizojizolea wakati wa uongozi na baada ya kustaafu kwake.
Mwinyi ni baba wa makuuzi ya tasinia ya habari, uchumi wa sekta binafsi, vyama vingi na uvumilivu wa serikali katika kukosolewa na watu binafsi au vyombo vya habari.
Mkapa ingawa hakuishi aliyoyahubiri anakumbukwa kwa utawala bora, uwajibikaji wa serikali na utumishi wenye tija katika serikali
J.Kikwete ni rais ambaye hajamaliza muda wake upo uwezekano akajitambulisha katika mambo mengine katika uongozi wake lakini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita anaonekana kushinda katika sifa kubwa ya uvumilivu wa kisiasa, hata pale ambapo wasaidizi wake wameshindwa kutekeleza majukumu yake kikwete ni raisi ambaye aliwapa uhuru mkubwa kufanya mambo bila kuingiliwa na nguvu za Ikulu, Ni baba wa demokraia ndani ya chama ingawa imetumika vibaya na wasaidizi wake ndani ya chama
Rais hakumbukwi kwa kuiwezesha serikali yake kujenga barabara, kuboresha elimu au maendeleo mengine kwani ndio kilichomsukuma kuomba ridhaa ya kuongoza. Rais anakumbukwa kwa kufanya tofauti kwa masilahi ya watu wake na tofauti na ambavyo watu wengine wengi wangetegemea afanye kutokana na madaraka yake na ndio mambo haya hukumbukwa.