Kikwete na hitoria ya kukua kwa tasinia ya habari na uvumilivu wa kisiasa tanzania

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Ukimchukia mtu kwa mapungufu yake, usingependa kuona anapata hata sifa kidogo kwani katika siasa mafanikio kidogo ya mtu ni kona ya maficho kujisahaulisha na ubaya wa utendaji wa mwanasiasa husika. Leo nataka kuandika kitu ambacho mimi nimekiona na kushuhudia historia ya nchi yetu na wapenzi wa ukuaji wa tasinia ya habari na demokrasia ya uvumilivu hawapendi kukumbuka na kutukuza.


Nikiwa nimekaa nilipata ndoto ya mchana kwa kufikiri kuwa hivi Rais Kikwete atawachia nini Watanzania baada ya kipindi chake kupita, Nyerere alituachia nini, Mwinyi alituachia nini na Mkapa akawapa zawadi gani watanzania? Maswali haya ni ya kitaaluma na yanahitaji kujibiwa kwa kitabu kwa kila kiongozi, na nafikiria kuishauri serikali kufanya mambo mema waliofanya viongozi hawa wanne kuwa nguzo ya kujenga maadili ya utaifa wetu. Ni budi tuwekeze na kunyambulisha vizuri. Kwa kifupi niyafupishe ifuatavyo:

Nyerere ni baba wa utu, umoja na usawa katika taifa hili na siku zote mapungufu yake yamemezwa na sifa hizi alizojizolea wakati wa uongozi na baada ya kustaafu kwake.

Mwinyi ni baba wa makuuzi ya tasinia ya habari, uchumi wa sekta binafsi, vyama vingi na uvumilivu wa serikali katika kukosolewa na watu binafsi au vyombo vya habari.

Mkapa ingawa hakuishi aliyoyahubiri anakumbukwa kwa utawala bora, uwajibikaji wa serikali na utumishi wenye tija katika serikali

J.Kikwete ni rais ambaye hajamaliza muda wake upo uwezekano akajitambulisha katika mambo mengine katika uongozi wake lakini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita anaonekana kushinda katika sifa kubwa ya uvumilivu wa kisiasa, hata pale ambapo wasaidizi wake wameshindwa kutekeleza majukumu yake kikwete ni raisi ambaye aliwapa uhuru mkubwa kufanya mambo bila kuingiliwa na nguvu za Ikulu, Ni baba wa demokraia ndani ya chama ingawa imetumika vibaya na wasaidizi wake ndani ya chama

Rais hakumbukwi kwa kuiwezesha serikali yake kujenga barabara, kuboresha elimu au maendeleo mengine kwani ndio kilichomsukuma kuomba ridhaa ya kuongoza. Rais anakumbukwa kwa kufanya tofauti kwa masilahi ya watu wake na tofauti na ambavyo watu wengine wengi wangetegemea afanye kutokana na madaraka yake na ndio mambo haya hukumbukwa.
 

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,666
3,097
Kikwete alitupa uhuru wa habari kwa 30%
watangulizi wake walikuwa below 20%
 

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Atakumbukwa kwa ubunifu wake wa kuwawezesha wananchi kujitambua, kukosoa watawala kwa uwazi na kuweza kuondoa umagimeza katika watendaji wa serikalini.

Atakumbukwa kwa utawala bora na uwajibikaje..katika historia ya nchi mawaziri na makatibu wakuu kupelekwa mahakamani ilikuwa utamaduni usiowezekana walikuwa mungu watu..huo utamaduni umeondolewa katika utawala wake...

Mpole na mkarimu kwa wabaya wake..hata waliomkataa kwa uwazi kabisa amebaki akibaki kuwakumbatia kwa kuamini kuwa ni watanzania
 

Mess

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
661
180
Hana jinsi maana wafadhiri wake Wamarekani wanataka hivyo.....Pia nguvu ya umma imezidi kupamba moto. Kuna changes ambazo huwezi kum compare aliyepita na aliyepo maana kila kitu kinabadirika. Huyu mimi binafsi namhesabu kuwa ni failure katika kila jambo. Kila chocholo anayotaka kujificha anaonekana
 

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Atakumbukwa kwa ubunifu wake wa kuwawezesha wananchi kujitambua, kukosoa watawala kwa uwazi na kuweza kuondoa umagimeza katika watendaji wa serikalini.

Atakumbukwa kwa utawala bora na uwajibikaje..katika historia ya nchi mawaziri na makatibu wakuu kupelekwa mahakamani ilikuwa utamaduni usiowezekana walikuwa mungu watu..huo utamaduni umeondolewa katika utawala wake...

Mpole na mkarimu kwa wabaya wake..hata waliomkataa kwa uwazi kabisa amebaki akibaki kuwakumbatia kwa kuamini kuwa ni watanzania
Mengi ya uliyoyaandika si sifa alizonazo ingawa wewe ungependa awe nazo. Kwenye bluu hapo ni ubunifu gani alililetea taifa hili? Kwenye njano wako watu wanasema wle aliowapeleka na kuwashughulikia ni wle ambao hawakuwahi kuwa wanamtandao wake. Hapo kwenye red unakazi kwelikweli kudadambua
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,879
9,832
Pia atakumbukwa kwa kuimarisha upinzani hasa CDM. Wakati anagombea Urais kwa mara ya kwanza na baada ya matokeo kutangazwa na kupata zaidi ya asilimia 80 watu wengi walisema amekuja kuua upinzani. Lakini baada ya miaka mitano upinzani ulipanda chati hadi sasa CDM inaifanya CCM isilale usingizi!! Atakumbukwa kwa kuwa Rais aliyerusuhu vyombo vya habari kuwa na uhuru wa kupindukia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom