Kikwete na ccm: Tunahoji utu na ubinaadamu wenu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na ccm: Tunahoji utu na ubinaadamu wenu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Azimio Jipya, Oct 27, 2010.

 1. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Utu ni taasisi pana! Taasisi ambayo ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya mtu na jamii yake.

  Alikuwa JK Nyerere peke yake na sasa, Dr W Slaa ... aliyekuwa anadhubutu Kuusemea Utu na kuuweka kama kigezo cha ustawi wa Taifa!

  Bila Utu, ambao ndiyo asili ya Mtu, maendeleo yote hayana maana yoyote! Yanakuwa ni maendeleo ya vitu! Ni utu kwanza...uwe chimbuko la demokrasia na maendeleo ya Taifa.

  Utu ni Uungu ndani mtu, hatuwezi kuusaliti tukabaki salama kama watu... lazima utu kutangulia kila nyanja ya jamii bila hivyo hicho kinachoitwa ustawi, maendeleo na demokrasia vinakuwa havina maana.

  Maendeleo ya Utu ndio yatawale maendeleo na ustawi wa jamii na taifa, na si maendeleo ya vitu bila kuujali, kuujenga na kuuendeleza utu.

  Kitaalam: Utu unanyaushwa, kuharibiwa na kuangamizwa na UFISADI.

  Kiua Utu ni Ufisadi. Kauli mbiu ni Utu Kwanza na Si ufisadi Kwanza.

  Utu unarutubishwa na haki, upendo, maadili ya uongozi bora, kuheshimiana, haki na usawa wa pato la taifa, matumaini, ukweli, ujasiri na si ukatili, uimara wa kusimamia na kutetea sauti ya umma, utambuzi wa dhana nzima ya utu na kuwaongoza watu kuelekea kilele cha utu wao kama ukombozi wa mwandamu.

  Ni Kweli na hakika: CCM na Kikwete wameutupilia mabali Utu ulioasili ya Mtu na kukumbatia kwa kiwango cha kutisha cha Ufisadi. Nani mwenye utu kamili anabishia hili?

  Baada ya CCM na Kikwete kusaliti asili ya mtu, kinachofuatia nchini ni Mgawanyiko na Matabaka kwa Taifa. Mgawanyiko na mtabaka hayo vinazaa Udini, ukabila, kuimarisha, ujinga, dhuluma, maradhi nk. Kisa? Utu umewekwa kando, tumeutwika Ufisadi na sasa tumeisaliti asili yetu kama binaadamu. Na kama utu haupo ...ina maana tunatawaliwa na kinyume cha utu...ambacho ni unyama ndani ya Mtu, yaani ufisadi... Na usiombe kuishi ndani ya jamii au Taifa kama hilo! Nani haoni kiama kinachoweza kufuatia hapo?

  CCM na Kikwete wana Utu na misingi yake ya kujibu hoja hii? Labda kwanza wawafilisi Mafisadi Papa Kumi (Kumi na Moja) waliowekwa hadharani tayariÂ… Vinginevyo wakati wa kuichai nchi ni sasa!

  Kwa kuwa CCM badala ya kupunguza maadui wa ustawi wa maendeleo ya jamii ya watanzania kutoka kuwa wa nne, sasa wanawajenga na kufikia sita. Yaani Ujinga, Maradhi, Umasikini, Ufisadi(Dhuluma), Ukabila na Udini.


  Tunahoji: CCM na Kikwete wanacha kujitetea kwenye hili? Mna Utu na Ubinaadamu wa kuhitaji kuliongoza kwa hekima, utulivu na amani Taifa hili kwa kipindi kingine cha miaka mitano? ....Tuwasikie!!!!
   
Loading...