Kikwete Na "AU vs Taifa"

Jk Lazima Atunge Safari Ili Kujiepusha Kukwaruzana Uso Na Uso Na Waliompa Cheo.
If U Ask Me I Think This Guy Is Very Diplomatic Because Hes Passively Sturring Up Issues Akijua Wazi Kuwa Itawagusa Moja Kwa Moja Maswahiba Wake.instead Ya Yeye Mwenyewe Kuwapinga,anatumia Watu Wengine.
Sitashangaa Kuskia Ra,el Na Muungwana Hawaivi Tena Chungu Kimoja.
Siku Zote Mwogope Yule Anayekuchekea,ndo Huyo Huyo Akumalizae!
 
(1)Jk Lazima Atunge Safari Ili Kujiepusha Kukwaruzana Uso Na Uso Na Waliompa Cheo.
If U Ask Me I Think This Guy Is Very Diplomatic Because Hes Passively Sturring Up Issues Akijua Wazi Kuwa Itawagusa Moja Kwa Moja Maswahiba Wake.instead Ya Yeye (2)Mwenyewe Kuwapinga,anatumia Watu Wengine.
(3)Sitashangaa Kuskia Ra,el Na Muungwana Hawaivi Tena Chungu Kimoja.
(4)Siku Zote Mwogope Yule Anayekuchekea,ndo Huyo Huyo Akumalizae!

1)Safari (ganzi) zitakapoisha ndio maumivu(uso kwa uso na wananchi 2010) yatakapoanza!

2)Hapo ndio penyewe!

Kwanini atumie wengine kama kweli ni mjasiri na hana wasiwasi kuwa na yeye ni one of the crabs in a bucket?

3)Inajulikana sasa kuwa hawaivi chungu kimoja!

Lakini hili halina manufaa na wananchi unless kina EL waseme ukweli wote mbele za wananchi waombe msamaa then tuanze upya na viongozi wapya mara baada ya haki kutendeka!

4)Hizo za kuchekeana na kumalizana kwao still sio big deal kwetu sisi wananchi at this moment!

Kama wasipoweka wazi kila kitu kilivyoendelea then who cares?

After all CCM inaelekea kaburini!
 
Na ukizingatia kuwa kiongozi wa tanzania si kikwete peke yake

Kazi tunayo sasa ya kuanza kufikiria ni nani mwenye kuweza kutupitisha kwenye wakati huu mgumu kwenye historia ya taifa letu!
 
Inaelekea wewe una data nyingi sana, then prove to me how CCM itakufa

Ndugu yangu mimi si shabiki wa vyama!

Mimi ni shabiki wa wazalendo na Taifa!

Nimeposti thread moja inayosema CCM wafanye marekebisho!

Kama na wewe ni mmoja wa wasioamini..Then be patient hapa JF na i willprove it to you!
 
Ndugu yangu mimi si shabiki wa vyama!

Mimi ni shabiki wa wazalendo na Taifa!

Nimeposti thread moja inayosema CCM wafanye marekebisho!

Kama na wewe ni mmoja wa wasioamini..Then be patient hapa JF na i willprove it to you!

Heshima Mkuu mimi mwenyewe hali kadhalika ila huwa napenda researched data , kabla sijasema kitu.nafikili huo ndo uzuri wa JF
ok tusubiri 2010 tuone kitakachotokea
 
Heshima Mkuu mimi mwenyewe hali kadhalika ila huwa napenda researched data , kabla sijasema kitu.nafikili huo ndo uzuri wa JF
ok tusubiri 2010 tuone kitakachotokea

Ninachoweza kukwambia ni kuwa kuna mpango wa grassroot movement ambao CCM hawataweza kuuzima!

Taifa litageuka na limeshaanza kugeuka!
 
Wale wanaoendelea kudoubt what i am fighting for should look at this...


Ubelgiji yamuonya JK
MPASUKO ZANZIBAR
na George Maziku



SERIKALI ya Ubelgiji imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua za haraka kuumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar, kwa kuwa unatia doa na kuhatarisha utulivu wa kisiasa nchini.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Balozi wa Ubelgiji nchini, Peter Maddens, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika ofisini kwake, Upanga, jijini Dar es Salaam.
Balozi Maddens alitahadharisha kuwa, kama hatua za makusudi na madhubuti hazitachukuliwa na watu wenye mamlaka juu ya mgogoro huo, hususan Kikwete, basi Tanzania inaweza kushuhudia machafuko, ghasia na mauaji kama ilivyotokea hivi karibuni nchini Kenya na hali tete ya kisiasa inayoinyemelea nchi ya Zimbabwe.
“Hali ya kisiasa ya Zanzibar inatutia mashaka wote. Kuna kila dalili kuwa mambo yanaweza kuharibika wakati wowote kama hatua madhubuti za kumaliza mgogoro wa kisiasa uliopo hazitachukuliwa, na katika hili tunaamini Rais Kikwete anawajibika moja kwa moja kutokana na madaraka aliyonayo kiserikali na katika chama chake,” alisema Balozi Maddens.
Alisema kuwa kwa tathmini yake, baada ya sherehe za Krismasi za mwaka jana, Tanzania ilikuwa inaongoza kwa uthabiti na utulivu wa kisiasa kuliko nchi zingine zote katika ukanda wa mashariki na kusini mwa Afrika, na hata Afrika nzima kwa ujumla.
Lakini alisema kwa sasa hali ya kisiasa nchini ni ya mashaka makubwa, baada ya kushindikana kwa mazungumzo ya muafaka kati ya vyama vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
“Kwa tathmini yangu, baada ya Krismasi, Tanzania ilikuwa inaongoza kwa uthabiti na utulivu wa kisiasa katika ukanda wa Afrika Mashariki, kusini na hata Afrika yote kwa kuangalia yaliyokuwa yanatokea nchini Kenya na Zimbabwe, lakini leo siwezi kusema hivyo, sababu ipo wazi, mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar unatia doa na kusababisha mashaka makubwa,” alisema Maddens.
Kauli hiyo ya onyo kutoka moja ya nchi wafadhili wa Tanzania, imekuwa ya kwanza kutolewa, baada ya kuwepo dalili za wazi za kurudia kuchafuka kwa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, kutokana na hatua ya hivi karibuni ya kukwama kwa mazungumzo ya kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Balozi huyo anatoa kauli hiyo wakati tayari kukiwa na tamko la baadhi ya wanachama wa CUF waliodai kuwa wako tayari kuanza kujitoa mhanga, kupigania haki zao Zanzibar.
Dalili za mgogoro wa kisiasa wa hivi sasa Zanzibar zilianza zaidi ya muongo mmoja uliopita, hususan baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, ambao matokeo yake yalikataliwa na CUF, ikidai kuporwa ushindi wake na CCM.
Kufuatia kuibuka kwa mgogoro huo, juhudi mbalimbali za kuleta mapatano zilifanywa na watu na taasisi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania, ikiwemo Jumuiya ya Madola ambayo ilifanikisha kufikiwa muafaka mwaka 1999, ambao hata hivyo, haukutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Ulipofanyika Uchaguzi Mkuu wa pili wa vyama vingi mwaka 2000, mgogoro ulizidi kukua baada ya matokeo ya uchaguzi huo kukataliwa tena na CUF.
Wakati huo, mgogoro ulichukua mkondo mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa ule wa kwanza, ambapo makumi ya Wazanzibari wafuasi wa CUF, waliuawa wakati wa maandamano ya Januari 2001 walipokuwa wakikabiliana na vyombo vya usalama.
Tukio hilo lilikwenda sambamba na uamuzi wa baadhi ya Wazanzibari na hususan Wapemba kukimbilia eneo la Shimoni, Mombasa nchini Kenya, walikoishi kwa muda kama wakimbizi wa kisiasa.
Kupuuzwa kwa utekelezaji wa muafaka wa Oktoba 10, 2001, kati ya vyama vya CUF na CCM, kulisababisha mgogoro huo kuendelea hata baada ya uchaguzi mkuu wa tatu wa vyama vingi visiwani humo mwaka 2005.
Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania mwishoni mwa mwaka 2005, Rais Jakaya Kikwete, aliahidi kuutafutia ufumbuzi wa kudumu mgogoro wa kisiasa Zanzibar, na akamwagiza Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kuwasiliana na mwenzake wa CUF, Seif Sharif Hamad, ili waanze rasmi majadiliano ya kutafuta muafaka.
Mwezi Februari mwaka juzi, Makamba na Hamad wakiongoza kamati ya muafaka iliyoundwa na wajumbe kutoka vyama vyao, walianza rasmi majadiliano ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar.
Julai mwaka jana mazungumzo hayo nusura yavunjike, baada ya kuwepo kauli za kutatanisha zilizodaiwa kutolewa na Makamba na viongozi wengine wa CCM.
Katika hatua hiyo, Kikwete aliyanusuru mazungumzo hayo kwa kuwasihi CUF kurudi katika meza ya majadiliano, huku akiahidi mazungumzo hayo kukamilika mapema iwezekanavyo.
Mapema mwaka huu, CUF ilitangaza kukamilika kwa mazungumzo na kusema kuwa vyama hivyo vimekubaliana kuunda serikali ya mseto visiwani Zanzibar, kama njia ya kuutibu mpasuko wa kisiasa.
Hata hivyo, mambo yaligeuka wiki chache baadaye, pale Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, zilipokutana Butiama mkoani Mara na kuibuka na pendekezo la kufanyika kwa kura ya maoni kabla ya kukubalika kwa pendekezo la serikali ya mseto kuanzia mwaka 2010. Hilo liliwafanya CUF wahamaki na kuwaona CCM kama watu wa hadaa na chama hicho kikuu cha upinzani visiwani kikatangaza kujitoa katika mazungumzo hayo. Hivi sasa, wakati CCM ikiwa inahangaika kuwarejesha CUF katika meza ya mazungumzo, chama hicho cha upinzani kimekuwa kikiendesha maandamano nchi nzima, kuishinikiza CCM iyasaini makubaliano hayo.
 
Alisingizia sana majukumu ya AU na sasa tumeshajua kauza nchi na makubaliaono mengine si mazuri na sasa tunajua yeye ni FISADI!
 
Kwasababu Watanzania HAWANA MATATIZO YOYOTE KABISA...INABIDI TUMPE DON KIKWETE MOYO WA KUHAMIA HUKO ZIMBABWE MARA BAADA YA KUMUONDOA MUGABE MADARAKNI ILI ASIBANWE NA MATAIFA A MGHARIBI...MWENYE MACHO AONE NA MWENYE MASIKIO ASIKIE....

Na. M. M. Mwanakijiji

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

YAH: Iongoze Afrika kupinga utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe

Naomba husika na kichwa hicho cha habari;

Hivi hadi nini kitokee ndipo viongozi wetu wataona kuwa kinachoendelea Zimbabwe ni aibu ya bara letu, na udhalilishaji wa utu, hadhi, na tunu ya mwafrika? Ni mpaka nini kifanyike ndipo tutaweza kuchukua msimamo wa kupinga uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, na kuchukua msimamo ulio dhahiri dhidi ya Robert Mugabe? Kwanini Tanzania nchi ambayo inadai katika Katiba yake kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" ifumbie macho utu wa wana wa Zimbabwe ambao wanateswa katika mikono ya utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe?

Inakuwaje wanasiasa wetu na wabunge wetu wanashindwa kutoa msimamo wa kulaani kauli za kidikteta ambazo zimekuwa zikitolewa na utawala wa Robert Mugabe? Hivi kweli tunahitaji wazungu kutuonesha kuwa kinachotokea Zimbabwe hakina mfano wa haki za binadamu? HIvi kweli tunataka hadi Amnesty International na Human Rights Watch waje na kutuambia kuwa ya Mugabe ni uovu uliokithiri?

Je tumekuwa watii na wenye kuheshimu sura za watu kiasi hiki hadi tunaogopa kumwambia kuwa "tunashukuru kwa mchango wako lakini kwa hili tunakukana"? Je hakuna watu waliofanya mambo mazuri huko nyuma na katika maisha yao ya baadaye wakaharibu na historia zao zikatajwa na nyota pembeni?

Wale wanaolalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu kule Palestine, Iraq na Afghanistani, walioandamana ujio wa Bush na ambao wakitetea haki za watu wa huko wako wapi leo hii wakati ndugu zetu wanaishi maisha ya wasiwasi na hofu kubwa chini ya mkono wenye kucha ndefu zichomazo wa Robert Mugabe?

Wakati umefika kwa viongozi wetu kuacha mazingaombwe ya diplomasia ya ukimya ambayo kimsingi ni ukimya wa kidiplomasia. Ni ukimya ambao unaendelea kutoa kibali kwa Utawala haramu wa Robert Mugabe kuendelea kutesa wananchi wa nchi hiyo. Je sisi Tanzania ambao tuliwahi kukiri katika imani zetu kuwa "binadamu wote ni sawa, na Afrika ni moja" leo hii tuko wapi?

Mch. Martin Luther King alipoandika barua yake kutoka Jela ya Alabama alisema wazi kuwa "udhalimu mahali fulani, ni udhalimu mahali pote" Je tunaweza vipi kukaa katika "kisiwa cha amani" wakati ndugu zetu wanateseka na kufanywa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Kwanini kina Morgan na wenzao waonekane si wananchi wa Zimbabwe kweli kwa sababu tu wanataka kuiokoa nchi yao?

Nini ambacho utawala wako unaogopa kusema na kufanya mbele ya Robert Mugabe? Hivi tukimtolea uvivu na kumuita kwa jina lake kuwa ni dikteta na kusema kuwa yanayofanyika Zimbabwe hayana nafasi katika bara la Afrika Mugabe atasema nini? Atatufanya nini? Hii heshima ya wazee ni heshima kweli wakati mzee anasimamia ubakaji na utesaji wa watu wake?

Naomba kutoa wito wa wazi, wa moja kwa moja na usio na utata kwako uwa Mhe. Kikwete kama Rais wa Tanzania, nchi ambayo imetoa na kulipa kwa damu ili nchi hizi za kusini mwa Afrika ziwe huru, asimame sasa na kusema "kama kutosha inatosha". Rais Kikwete ukiwakilisha mawazo ya kizazi kipya uungane na Botswana kwa kumwita Balozi wa Zimbabwe nchini na kuonesha kutokufurahishwa na yanayoendelea Zimbabwe.

Zaidi ya yote, Rais Kikwete akiwa ni Mwenyekiti wa AU aitishe mkutano wa haraka kati ya Morgan na Mugabe Jijini Dar (na si mtu mwingine nje yao) ili kujadiliana na kukubaliana jinsi uchaguzi wa marudio utakavyokuwa na kupata uhakika kuwa kila mmoja wao ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo. Kikwete anaweza kufanya hivyo kwa kutumia kivuli cha NEPAD ambamo ndani yake kuna "African Peer Review Mechanism". Huu ni wakati wa kuonesha uongozi.

Na endapo Mugabe hatokuwa tayari kusikiliza ushauri wa rafiki, basi wakati umefika wa kuvunja uhusiano wetu wa kidiplomasia na Zimbabwe. Itauma, lakini inabidi.

Nikukumbushe maneno ya Rais Nyerere kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa miaka ya sitini ambapo hoja ya kukubali kuiingiza Afrika ya Kusini katika jumuiya hiyo. Nyerere alisema wazi kuwa kwa kadiri ya kwamba siasa za kibaguzi zilikuwepo Afrika ya Kusini basi Afrika ya Kusini haiwezi kuwa mwanachama. Na akatamka yale maneno mashuhuri ya msimamo wa kiongozi mbele ya Malkia "Mkiwapigia kura kuwaingiza Afrika ya Kusini, mtakuwa mmepika kura kututoa sisi". Na hoja ya Mwalimu ikashinda.

Na ni Mwalimu huyo huyo ambaye alizungumzia suala la "uraia" baada ya Idi Amin kuanza kuhoji uraia wa waasia wa Uganda na kuanza sera zake za kibaguzi kule. Mwalimu alizungumza siku ile August 21, 1972 pale Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Mwalimu alisema hivi "Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa moyo huo huo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wengine. Ni lazima tutende siyo maneno tu".

Mhe. Rais, Afrika inadhalilishwa na vitendo vya Mugabe na mashabiki wake. Afrika inafanywa duni kwa viongozi kama yeye. Ni kweli tuna matatizo yetu Tanzania, nafahamu tuna kashfa zetu za mambo ya fedha nchini na uongozi wa kishkaji; nafahamu wazi kabisa ndani ya CCM na serikali kuna kubebana na kulindana. Lakini ukweli ni wazi kuwa hatujafikia walipofikia Zimbabwe, hatujafikia mahali pa kufanyana vibaya kiasi cha Zimbabwe. Ni kweli tuna matatizo yetu lakini tukiyaweka ya Zimbabwe upande wa pili, ya kwetu yanaonekana ni kheri tupu!

Sisemi upuuzie matatizo yetu, sitoi ushauri kuwa ya kwetu kwa vile ni madogo basi usiyafuatilie. La hasha, ninachosema ni kuwa chukua msimamo kama kiongozi na kwa niaba ya wale waliotangulia mbele ya haki, kwa niaba ya wale waliomwaga damu yao kukomboa bara letu, usimame na kumwambia Mugabe inatosha na saa na wakati wake umepita aamue kujiuzulu na kustaafu kwani yeye kama wanadamu wengine, atakufa tu, na Zimbabwe itatawaliwa na mwingine. Mugabe hana ubavu wa kuzuia hatima ya nchi hiyo, na siku moja wengine watasimama mahali pake.

Akiamua kuachia ngazi sasa na kufanya mapatano ya kisiasa na wale walioumia chini yake, labda historia itamuonea huruma. Lakini Zimbabwe haiwezi kuendelea jinsi ilivyo, huku sisi rafiki zao na ndugu zao tukikaa nje kuangalia. Mhe. Rais, onesha msimamo sasa, na uliongoze Taifa letu kuchukua msimamo dhidi ya Mugabe ili tuwape nafasi ya ndugu zetu wa Zimbabwe ya kuishi katika nchi ya amani, utulivu, na mshikamano.

Sijaomba vingi, lakini hilo nakuomba kwa machozi.

Nimalizie kwa kukumbusha maneno haya ya baba wa Taifa tena alipozungumza mwaka 1959 kwenye mkutano ule uliofanyika Uingereza Juni 26 (karibu miaka 50 kamili iliyopita). Katika mkutano huo uliokuwa unazungumzia Afrika ya Kusini na utawala wa Makaburu Mwalimu alisema maneno haya "Serikali ya Afrika ya Kusini inapigana na historia, ni wao watakaoshindwa. Tunafahamu harakati za ukombozi zitafanikiwa katika Afrika ya Kusini. Kama tunajiamini tutashinda".

Mheshimiwa, Mugabe anashindana na historia na kwa hakika atashindwa; harakati za mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea yatafanikiwa, na kama sisi sote tunajiamini kwamba tuko sahihi basi tutashinda. Tuongoze katika hili kwani bwana mdogo kutoka Botswana ameshaonesha njia.

Wasalaam katika Kuliinua Bara letu

M. M. M.
 
Kwasababu mmenifungia hapa JF...Nataka nione kama facebook watanifungia pia!
Huko na Kikwete mwenyewe yupo na profile...Sasa tuone ni kivipi kwenye dunia ya leo watu wanafungiwa kwa kuwatuhumu watu!
 
Kwasababu mmenifungia hapa JF...Nataka nione kama facebook watanifungia pia!
Huko na Kikwete mwenyewe yupo na profile...Sasa tuone ni kivipi kwenye dunia ya leo watu wanafungiwa kwa kuwatuhumu watu!

Sorry Mimi Nimeshatoka Kutoka kwenye Kufungo kule Jamboforums...Kosa langu ilikua ni kutukana!!... Sasa naona Niki kufuata fuata..nitafungiwa tena hapa Jamiiforums...
 
Kikwete anampa Pinda nafasi ya kushughulikia mafisadi waliomsaidia kupata Urais maana Pinda hana soni nao! Dawa ya siasa za CCM ni kupata mtu atayewageuka waliomweka madarakani kwa maslahi ya Taifa (issue ya Chenge inathibitisha hili). Huyu sasa hivi mwenzetu kumkoma fisadi...!!!

Pinda mwenyewe mbona ni kama Mbwa anayebweka bila kung'ata? ama nakosea husiana na hilo.?
 
Kwasababu mmenifungia hapa JF...Nataka nione kama facebook watanifungia pia!
Huko na Kikwete mwenyewe yupo na profile...Sasa tuone ni kivipi kwenye dunia ya leo watu wanafungiwa kwa kuwatuhumu watu!

Hahaha...politics za Tanzania ndani ya Facebook....

Ntaomba unikaribishe katika jukwaa la Siasa utakalokuwa nalo huko mwana...

Godspeed.
 
Wakati mustakabali wa Taifa haujulikani kutokana na kugubikwa na wingu zito la kashfa za ufisadi..Pamoja na dilema kwenye muafaka na wenzetu wa visiwani...

Mh Rais ameitisha kikao ambacho hakutokea..(Salva aliwakilisha)..

kikao ambacho kilitoa ratiba kwa watanzania yenye kuonyesha ni jinsi gani rais wetu mpendwa anavyoyajali majukumu ya uenyekiti wa AU na kupata nafasi ya kushughulikia migogoro na matatizo ya mataifa mengine na kuyapa kipaumbele zaidi ya yale ya Taifa lake!

Na ni jinsi gani alivyo busy and dedicated kulitumikia baraza hilo badala ya Taifa!

Hilo siyo baya!

Baya ni kwamba kuna mustakabali muhimu wa taifa anaokabiliana nao at this moment!

Je ni wakati wa watanzania kuliangalia hili?

For once jmushi umenigusa penyewe.actually i dont have anything against prezo kwa kushughulikia matatizo ya africa lakini kweli kabisa huyu mtu ameignore matters of national interest.anakazana kujitafutia umaarufu kwenye international arena.this is too bad kwa kweli ameshasahau kuna inflation rate ya juu mno na ufisadi upo kwenye peak.
 
For once jmushi umenigusa penyewe.actually i dont have anything against prezo kwa kushughulikia matatizo ya africa lakini kweli kabisa huyu mtu ameignore matters of national interest.anakazana kujitafutia umaarufu kwenye international arena.this is too bad kwa kweli ameshasahau kuna inflation rate ya juu mno na ufisadi upo kwenye peak.

I sincerely hope that mwaka 2010 Mheshimiwa Kikwete atakuwa anategemea kura za Wananchi wa nchi wanachama wa AU ili kuweza kurudi tena Katika kiti ya Urais.

Kwa mwenendo huu Muungwana ana wakati mgumu sana... Boriti la kwenye jicho lake hataki lishughulikia... ni uongozi wa aina gani?
 
Tusubiri plan B wakuu!
Hawana pa kwenda!
JF NI CHOMBO KILICHOWEKWA MAKUSUDI KWA WAKATI HUU!
I TRULLY BELIEVE KUWA HAKUNA COINCIDENCE!
Kikwete alikataa kusikiliza ushauri wa kina OBASANJO!
Sasa shauri hilo eti linarudishwa bungeni kwa niaba yake!
Kama kikwete kweli analiamini bunge...Then kwanini hakuliruhusu liunde kamati ya madini na akaingingilia kazi zake?
Wananchi macho DODOMA LAKINI YEYE ANAENDELEZA LIBENEKE!
Toka mwanzo nilijua!
BUSH-BLAIR-SINCLAIR-KIKWETE NA ASSOCIATES WAKE NI HATARI SANA KWA MASLAHI YA WANADAMU WAPENDA UHURU NA HAKI!
HAWA WATU HAWANA TENA QUALIFICATIONS ZA KUIONGOZA DUNIA!
 
Kuna habari kuwa jk anataka tz ipeleke majeshi yake Zimbawe!
TUSIKUBALI KWA WAKATI HUU!
TUPEWE HAKI YETU KWANZA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom