Kikwete Na "AU vs Taifa" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Na "AU vs Taifa"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jmushi1, Apr 26, 2008.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Wakati mustakabali wa Taifa haujulikani kutokana na kugubikwa na wingu zito la kashfa za ufisadi..Pamoja na dilema kwenye muafaka na wenzetu wa visiwani...

  Mh Rais ameitisha kikao ambacho hakutokea..(Salva aliwakilisha)..

  kikao ambacho kilitoa ratiba kwa watanzania yenye kuonyesha ni jinsi gani rais wetu mpendwa anavyoyajali majukumu ya uenyekiti wa AU na kupata nafasi ya kushughulikia migogoro na matatizo ya mataifa mengine na kuyapa kipaumbele zaidi ya yale ya Taifa lake!

  Na ni jinsi gani alivyo busy and dedicated kulitumikia baraza hilo badala ya Taifa!

  Hilo siyo baya!

  Baya ni kwamba kuna mustakabali muhimu wa taifa anaokabiliana nao at this moment!

  Je ni wakati wa watanzania kuliangalia hili?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Mimi kwa maoni yangu nchi imekwishamshinda huyu jamaa. Hivyo hakuna cha kunishangaza tena.

  Katiba yetu ingekuwa ni kwa maslahi ya Watanzania basi kungekuwa na kipengele cha Bunge kupiga kura ya maoni ya kutokuwa na imani na Rais aliye madarakani na hivyo kumuondoa ili kuruhusu uchaguzi mwingine.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Kama majukumu ya AU yamemkinga kiasi cha kwamba hawezi kuwatumikia wananchi then kweli what else should we think?
   
 4. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Matatizo yaliyopo sasa hivi tanzania yanahitaji moyo. JK anakwenda kupumzika yeye mwenyewe atakuwa ameisha ona kuwa mambo ni mazito.

  Nafikiri baadhi ya watu wanavunja katiba na kuwa MAfisadi wakifikiria pesa zinaweza kuwalinda milele bila kuangalia historia. Mara nyingi mambo yakikugeuka unaweza kutafuta pa kwenda na usipapate. Zile Richmond na mikataba yote ya kifisadi ni jambo la muda. Kuna Watanzania Wenye akiri mzuri tu zaidi ya hao MaFiSADi

  Sheria zipo ni nguvu tu ya umma itakayowezesha kufuata sheria na taratibu za nchi. Hatimaye kuwafikisha ktk vyombo vya dola.

  Hakuna mtu atakaye waletea watanzania maendeleo. Maendeleo yataletwa tu na watanzania wenyewe kwa kushirikiana na viongozi waadilifu.

  Viongozi waadilifu wapo wengi tu kinachohitajika ni kuondoa MAFISAdI na viongozi waliochaguliwa kwa kutumia RUSHWA
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kikwete akirudi tu tokea huko ethipia sijui wapi, kati kati ya mwezi Mei anaelekea Japan.

  kweli atakaa nchini kutatua matatizo ya wananchi wake huyu? sidhani
   
 6. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Banadugu,
  Sometimes we need to be fair. I think this was not a bad idea, to let the country know of their prez's tasks, especially after we became angry of his travelling habits.

  Africa needs Tanzania probably just as much as Tanzania needs Kikwete. It is up to him to stike the right balance. TZ is more experienced and well positioned to solving African crisises, as long as we don't overstreach our limited resources. If we stop helping Congo, Burundi, Rwanda, Somalia etc., their conflicts might spillover to our borders in the form of refugees etc., and instead of trading with them, we might end up sharing the little bread we have with them. I wouldn't mind seeing him doing some African diplomacy as long as he still keep a close eye on all the issues that Tanzanians entrusted him for. Mungu ibariki Tanzania.
   
 7. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kwani Kikwete atakuwa Mwenyekiti wa AU kwa kipindi chake cha Urais?Mwaka mmoja anamaliza muda wake!Sasa ikiwa inaonekana huo Uwenyekiti unampunguzia muda wa lulitumikia Taifa .angeukataa tangia mwanzo alipo petengezwa!Angewaambia viongozi wa AU "jamani na majukumu mengi sana huko nyumbani siwezi kuwa mwenyekiti wa AU mtafute Rais asiye kuwa na majukumu kwenye nchi yake"
   
 8. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nani huyu?? Kikwete au,
  Hawa watu wanapenda sifa jamani na sio kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wao jamani!
  Mimi nashindwa kumuelewa huyu Fisadi na mbadhilifu wa pesa zetu, mbona safari za nchi za nje ni nyingi sana kuliko za kuwatembelea wapiga kura wake jamani???
  sasa kweli huyu naweza hata kuelewa hali halisi ya watanzania??
  anasubiri kampeni ndio hajifanye kuzunguka Tanzania nzima, wakati akiwa president anazunguka dunia nzima sio??

  Haya bwana, na tusubiri, iko siku tu
   
 9. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2008
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kikwete anampa Pinda nafasi ya kushughulikia mafisadi waliomsaidia kupata Urais maana Pinda hana soni nao! Dawa ya siasa za CCM ni kupata mtu atayewageuka waliomweka madarakani kwa maslahi ya Taifa (issue ya Chenge inathibitisha hili). Huyu sasa hivi mwenzetu kumkoma fisadi...!!!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na ukizingatia kuwa kiongozi wa tanzania si kikwete peke yake
   
 11. M

  Mutu JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh hata mimi nimekuwa nikipinga sana safari zake za nje ,ila kwa hili naona yuko makini safi tu anatimiza wajibu wake kama mwenyekiti.Na ukizingatia kama ujumbe ameuacha na umewakilishwa na msemaji wa ikulu/whatever inamaanisha hata angekuwepo ujumbe ni ule ule.Na ndio maana wakawepo wazaidizi na hawa wasemaji lisilo budi hutendwa.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Inategemeana na uzito wa issues!Mjukumu yake ya AU hata mimi nayasupport!Lakini haina maana kwamba hana wasaidizi huko kwenye baraza la Umoja wa Afrika!
  Anao wasaidizi pia kwenye uongozi wake wa taifa letu!
  So point hapa ni which of the assignements matter the most!
  Mh Rais binafsi pamoja na wewe naona mmeamua kuwa kikao ama vikao kadhaa vinavyokuja kwenye ratiba yake ni muhimu kuliko vile vinavyoliliwa na watanzania kwenye kipindi hiki kigumu cha mpito!?
   
 13. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  JK anafikiri mpaka anapagawa,hebu afanye nini mpaka watanzania wamuelewe? kila akiruka na hili mnaibuka na lile, daa!!!! ngoja asafiri apunguze machungu.Da!!watanzania wanalia naye!!! , sijui 2010 watakuja na sera gani, labda watasema wamejenga mashule mengi, kumbe watanzania wamechangishwa
   
 14. M

  Mutu JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Wewe kama unashindwa ku-balance mambo ni wewe,kwa hoja yako inaonyesha kwamba asitumike kama M/kiti au unasema nini?Kwani mimi au yeye kakwambia Bongo ndio arudi tena au kwa kusema pia anawajibu pia wa kutumika kama M/kiti wa africa sio sahihi.Jua ku balance mambo ndugu sio ukiambiwa umeweka chumvi nyingi kesho ndio huweki kabisa.Mimi sipendi ziara zake nyingi za nje ila sio kwamba asiende kabisa!

  Jambo jingine kunichanganya mimi na uyo mkwere JK unakosea sana maana I don't admire the guy ,he seem to me to be very weak !Ila hainifanyi nipinge kila jambo lake hata ile ambalo naona hajakosea .
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa ndugu yangu!Ama labda kwa maana nyingine hatujaelewena bado!
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Mambo yaendelea kuwa mambo! Highlights pekee zinatosha kukupa ujumbe kamili wa makala hii!

  CUF bado yalia na safari za JK

  na Kulwa Karedia  SIKU moja baada ya Ikulu kutoa taarifa ya mafanikio ya safari za nje zilizofanywa na Rais Jakaya Kikwete, Chama cha Wananchi (CUF) kimeitaka serikali kutangaza pia gharama zinazotumiwa na Rais katika safari za nje.
  Akizungumza na ‘Tanzania Daima’ jana, kiongozi Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, alisema gharama zinazotumiwa na Rais Kikwete kwa safari za nje ni kubwa, hivyo zinapaswa kuwekwa dharani kila mtu azijue.
  “Nimesikia kwamba Ikulu inasema ziara za Rais Kikwete nje ya nchi zimekuwa na mafanikio makubwa. Haya ni yapi? Tunapaswa kuelezwa ukweli kwanza wa gharama anazotumia,” alisema kiongozi huyo.
  Alisema Ikulu imekuwa ikifanya siri kubwa ya gharama zinazotumiwa na Rais wakati ni kodi ya wavuja jasho, hivyo kabla ya kufurahia mafanikio, wananchi wanapaswa kuelezwa gharama zilizoleta mafanikio hayo.
  Alisema kwa vile Rais amechaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia, anapaswa pia kuwa wazi na kupunguza safari za nje, ili kushughulikia masuala ya ndani zaidi.
  “Rais tumemchagua kwa ajili ya kushughulikia zaidi masuala ya ndani…sasa inakuwaje kila leo unasikia yuko safari tena nchi za mbali. Hii inatupa picha gani tunao mtegemea?” alihoji Hamad.
  Alisema kitendo cha kuwa na safari nyingi kimesababisha Rais Kikwete kushindwa kushughulikia kwa kina suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar, ambalo sasa linaekea kuchukuwa sura mpya baada ya mazungumzo ya kusaka mwafaka kuingia dosari.
  “Tuliamini kwamba Kikwete kama alivyowahi kuahidi kama anageshughulikia suala hili kwa kina, sasa imebaki mvutano tu, huku hatima ya mazungumzo baina ya CCM na CUF yakibaki kitendawili,” alisema Hamad.
  Safari za Rais Kikwete nje ya nchi zimekuwa nyingi lakini faida yake imekuwa kidogo, tofauti na Ikulu inavyodai kupata mafanikio makubwa.
  “Hata zile fedha zilizosainiwa na Rais Gorge Bush wa Marekani hazikutokana na ziara ya Rais Kikwete, bali ni mpango wa Serikali ya Marekani katika kampeni yake ya kusaidia nchi masikini…hata hapa pia tunapaswa kuelezwa ukweli,” alisema Hamad.
  Alisema hali hiyo imekuwa ikichangia kila mwaka bajeti ya serikali kuongezeka huku ikitegemea zaidi wafadhili. “Nakwambia kwamba hivi sasa serikali imeelekea kuelemewa na mzigo huu mzito, wakati serikali ya Mwalimu Nyerere haikuwa tegemezi kiasi hiki, licha ya kukabiliwa na matatizo mengi ya uchumi enzi hizo na alikuwa akitegemea asilimia 6 tu kutoka kwa wafadhili,” alisema Hamad. Juzi Ikulu kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Salvatory Rweyemamu, ilitoa taarifa kuwa ziara za Rais Kikwete nchi za nje zimekuwa na mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na msaada wa dola milioni 698 kupitia Mpango wa Milenia (MCC) kutoka Serikali ya Marekani.
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mtakufa Nacho Roho Mbaya Na Choyo
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Our Coutry needs him more than anybody else!

  Hata kwenye zama hizi za "Secured video conferences"

  mnataka kutufanya wapumbavu?
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Choyo ya nini ndugu yangu?

  Kwani hukumbuki keshasema sisi ni masikini?

  Wapi taarifa za matumizi yao ya kitajiri na safari za kila kukicha?

  Once again uje na data ili kuendelea kuipa heshima JF!
   
 20. Gigo

  Gigo JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2008
  Joined: Aug 6, 2006
  Messages: 455
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  ni kazi yetu sote...acheni usenge,,,
   
Loading...