Pamoja na kukuta Mzee Mkapa kauza mashirika yote ya uma mabenki Viwanda vyote Wewe ulipoingia tu pale White House, Watanzania tulianza kula bata mpaka Siku unaondoka. Mpaka ulipoondoka tukabaki na Chenchi Mifukoni,
Mzee wetu Kikwete Mungu Akubariki Pamoja na Uzao wako, mwenye hakuwa na Nyumba alijenga, mwenye alikuwa analala barabarani alipanga nyumba, kwa kifupi Mzee, Kwa hii Tanzania kila Siku ilikuwa ni sikukuu,
Ila Mzee Nina swali moja tu kwako. Ulifanyafanyaje mpaka Wananchi karibu wote Tukawa matajiri?. Nakumbuka kuna Siku uliona wapinzani wanaletaleta kelele, yaani wewe badala ya kuwafunga Jela, ukawaita wote Ikulu halafu ukagonga nao Mvinyo hapo Ikulu, na baada ya hapo wakapoa na mambo yakaendelea, hivi mzee hizi mbinu ni nani alikuwa anakusaidia au ulikuwa ni utashi wako? Ww ni Nomaa,
Yaani Enzi zako, kwa jinsi ulivyokuwa na hekima na Roho safi, ulikuwa hata unao uwezo wa kusafiri na ikulu ukamwita hata Mbowe au Hashimu Rungwe na ukamwambia, Bwana mdogo Mimi nasafiri kidogo ila nakuacha hapa Ikulu uniangalizie mpaka nirudi, tena bila presha, kwa sababu Kwako wewe hukuwahi kuwa mtawala Bali kiongozi mahiri, mcheshi uliyewapenda Watanzani wote bila kuwabagua kwa Rangi Chama au Kabila.
Sasa hivi Mzee wetu wewe mwenyewe unaona kila Siku ni Kama Tanzania tunazidi kuzama, basi Tunakuomba umfate huyu Mzee wetu mpya Kwa upole na Busara zako umwambie na umwelekeze nini Siri ya mafanikio yako, Pengine tunaweza kuokokaa, maana Mzee huku Tunakoelekea siko kabisa. Wananchi kila ukitizama sura zao ni Kama hawana tena matumaini, Hapa kazi tu, kazi zenyewe ziko wapi ili watu wafanye?. Yangu ni hayo tu Mzee.