Kikwete mwanauchumi na uchumi wa Tanzania

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,535
Jakaya kikwete rais awamu ya 4 katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania kitaaluma ni mchumi shahada ya kwanza.Kuwa rais wa nchi yoyote ile sio lazima use umesomea uchumi,cha muhimu ni kuwa na wataalamu wa uchumi wenye kutoa ushahuri sahihi kwa rais.

Washauri wa uchumi wa sasa wanazidi kutuchanganya zaidi,na washindwa kutoa muelekeo ulio sahihi kwa taifa kiuchumi.Wachumi wetu msitumie faida ya rais kutokusomea masomo ya uchumi,tukajikuta tumeanguka kiuchumi sisi kama taifa.Kwa awamu ya 4 kikwete alikuwa na faida(advantage) ya kusomea uchumi ,kwa hiyo ndondooo mbambali kuhusu uchumi alikuwa anazijua.

Sio kwamba awamu ya 4 ilifanya cha ajabu saana katika uchumi wetu(licha ya kuwa na rais mchumi) kinachotisha kwa sasa ni maono na mbinu wanazotumia wataalamu wetu wa uchumi kufikia malengo talajiwa.Tunaweza kuona ni jambo dogo lakini inapofikia hatua adi vyombo vikubwa kama TRA na BOT vinapingana kwa kauli,si dalili njema kabisa.

Ni vyema pia wizara ya fedha ijue ya kwamba sio lazima kufikia malengo yote ya kibajeti katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji.Wizara ya fedha msiishi kwa shinikizo la kutaka kutekeleza kila jambo wakati kiukweli kuna mambo bado ni ngumu kuyatekeleza kutokana na ufinyu wa bajeti.

Huwezi tekeleza kila kitu ndani ya mwakawa 1,elimu bure,viwanda,ndege mpya,ajira mpya,reli ,mahakama ya mafisadi,etc.Licha ya mafanikio machache ya kiuchumi awamu4,lakini bado kulikuwepo na matatizo kadhaa ya kiuchumi,tunaomba wachumi wetu msituludishe nyuma.

Ni mda wenu kufanya kazi bila hofu yoyote mwisho wa siku tufulaie matunda ya Kazi yenu.Ni wakumbushe tu watanzania walio wengi sio watu wa kupenda maisha ya anasa,maisha ya wengi wetu ni kupata japo chakula (milo3) na maji ya kunywa.Tusijejikuta ata uhakika wa mlo1 haupo kwa mwananchi wa kawaida uku tukishangilia ununuzi wa ndege 3,na ujenzi wa viwanda.

Mwisho kabisa kuimarika kwa uchumi wa nchi kunategemea sana wasomi kutumia taaluma yao ktk utengenezaji wa sera na kupendekeza njia bora ya kuzisimamia.Kikwete licha ya kuwa mchumi na pia kuwahi kuwa waziri wa fedha sio rahisi kuonyesha uhusiano wa taaluma yake iyo na uchumi wa tanzania wakati wa awamu ya 4.
 
Back
Top Bottom