Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,604
- 3,163
Kinacho nishangza Kwa mwanakijiji mara nyingine post zake huwa hazina maana kwa mtazamo wangu.
Lakini yeye mwenyewe amethibitisha kuwa katika tuhuma zote hizi RA jina lake halipo hivi unataka Rais atumie sheria ya kuweka watu kizuizini ambayo ilifutwa hapa nchini.
Unataka RA afikishwe mahakamani kwa tuhuma ambazo atashinda. Lawama bila uthibitisho ni zilezile anazotoa mzee Mengi. Anapotakiwa atoe ushahidi na vyombo vya Dola anadai anasakamwa.
Unajua watu wa aina ya Mengi wanaweza kuwa na mambo mawili. Moja kutaka kuitenganisha serikali na wananchi kwa maslahi yake hakuna asiyejua kwamba mengi anataka U-rais lakini hajui njia ya kuitumia. Pili inawezekana anamatatizo ya akili. You never know, kwa sababu wimbo wa mafisadi amekuwa akiuimba bila kuonyesha ushahidi. Achukue hatua kwanza aeleze ushahidi, anaweza hata kuchukua hatua ya kuwashitaki mafisadi. Kwa kutumia haki ya yeye kuwa mwananchi.
Vinginevyo tutaiangamiza nchii kwa manufaa ya mafisadi au madiktea wangine. Watanzania lazima tuwe waangalifu watu aina ya Mengi. Hivi toka lini tajiri akawa msafi? Hivi toka lini mtu anayefanya biashara ya kawaida akawa na fedha za kumwaga hovyo kwa kisingizio cha kusaidia wananchi.
Mwanakijiji hebu chunguza wote waliomwaga faedha zao kwa mambo ya mpira utajiri wao uko wapi? Ambao hadi sasa matajiri wachunguze kama walilipa kodi kihalali. Kama hawana uhusiano wowote na mihadarati kisha uje na post tuijadili.
Mkuu Saidsabke,
Nimekusikia na nimekupata vizuri lakini nafikiri ama uwezo wako wa kupambanua mambo ni mdogo au umeandika kwa kutetea tu maslahi ya waliokutuma kwani kwa sasa inaeleweka forum ina vimeo kibao.
Hivi wewe unaamini kwamba Mengi ni mpumbavu kiasi hicho? Ni vyombo gani hivyo ambavyo ulitaka Mengi apeleke ushahidi wake? Takukuru, Polisi, au wapi? Hivyo vyote ni vyombo vya serikali na serikali ni ya kifisadi. Hakuna mtu mwenye akili Tanzania ya leo anayeweza kupeleka eti ushahidi wa ufisadi kwa Mwema au Hosea. Jambo la msingi ungewashauri hao waliotajwa hadharani kwamba ni mafisadi waende mahakamani wamshitaki Mengi kwa kuwakashfu and then Mengi angepeleka ushahidi mahakamani wakati wa kujitetea na si vinginevyo.
Endelea kula hizo pesa za ufisadi lakini mwisho wake hauko mbali. Tumechoka!!!!!!