Kikwete mteue Rostam kuwa Waziri, Yes I dare you! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete mteue Rostam kuwa Waziri, Yes I dare you!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 4, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Licha ya tuhuma zilizomzunguka Basil Mramba, Kikwete alimteua kuwa Waziri wake. Licha ya tuhuma zilizomkabili Andrew Chenge, Kikwete alimteua mara mbili kuwa Waziri wake. Kama vile mtu asiyejali tuhuma zinazowakabili watu mbalimbali ndani ya serikali yake (Masha mfano mzuri) Kikwete ameendelea kuwazawadia na kutenda kana kwamba yote yanayozungumzwa yanatokea katika nchi ya kufikirika.

  Sasa, mimi ninapendekeza ili yote haya yaishe tujue moja, Rais Kikwete amteue rafiki yake wa karibu na anayesadikiwa kuwa ni mshirika wake pia wa kibiashara na kuwadi wa madeal yake ya kibiashara Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz kuwa Waziri wa Fedha.

  Na kama ikiwezekana anaweza kabisa kumpa Uwaziri Mkuu ili yaishe tu. Ni mara ngapi sasa anatuletea watu wale wa karibu ya Vodacom (72 hours) na kuendelea kutuzuga vichwa vyetu. Nianze tena kuhesabu watu wenye mahusiano na Rostam na Vodacom ambao Kikwete amewasogeza karibu na sekta nyeti kana kwamba ndio wale Yesu aliwazungumzia kwenye hotuba ya Mlimani?

  I mean, pale aliposema "heri wanaohusiana na Vodacom, maana hao watairithi nchi (Tanzania)"!?

  Sasa badala ya kuzugana na kuzungushana ni bora tu waifanye Vodacom kuwa kitengo cha serikali na Rostam kuwa Waziri wa Fedha (au Waziri Mkuu, chochote atachoamua RA).

  Mwanzoni alipoingia madarakani tetesi zilikuwepo kuwa RA angeweza kupewa Uwaziri lakini yeye mwenyewe RA (au kwa ushauri wa wengine) ali decline. Sasa kwa vile muhula wa kwanza ndio huo unakwisha, ni bora kumpa Uwaziri wa Fedha.

  May be not, Nadhani ampe Uwaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Labda hiyo siyo nzuri sana. Pengine Uwaziri wa Biashara na Mipango. Siyo hilo? Vipi kuhusu Uwaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora)?

  Vyovyote vile, mimi nakupigia magoti mheshimiwa Rais mpe Uwaziri Rostam ili hatimaye binafsi nijue umeamua kututukana kwa jumla Watanzania kuliko huu mtindo wa reja reja. Mpe tu, tena ukipenda unaweza kumtengenezea cheo cha "Naibu Rais" or something flashy like "Deputy Prime Minister and Minister of Finance and Special Advisor to the President on Economic Affairs with Special Portfolios"!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Well...that will bring diversity...won't it?
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkulu hapo pekundu nadhani ulimaanisha kitengo siyo kitendo kama nime kosea uta niambia. I like the way you made your point sarcastically & even the title will prompt a lot of interest to this thread. Big up for sending your message in a creative way. As we say wapenda simu, message sent.......
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  asante..yeah.. nilimaanisha "kitengo"..
   
 5. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Cabinet Tanzania inaundwa na regional representantion na CCM appeasement of loyalists.. Merit is a non-existent factor and until that changes kazi tunayo.. Rostam hataki uwaziri wakimaskini... What for! Angetaka angekuwa.
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hivi nyinyi mnataka Rais awe na marafiki masikini wasio na uwezo wa kumsaidia wakati wa kampeni?

  RA ana deal zake halali sema tu nyie mnamchafua. JK analijua hilo.

  Mmezidi WIVU. LOL

  FP
   
 7. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Wana jamiiforums!

  Kwanza nimshukuru Mzee Mwanakijji na wote ambao mnasapoti hii thread!

  JMK aka Matonya should come in the open na kumuunga mkono mentor wake Rostam Aziz amateue awe Waziri Mkuu ili kieleweke kama alivyofanya Mkapa! Yeye alimteua kuwa Mweka Hazina wa CCM na hapo ndipo mafisadi wakawa na full and un- impeded access to the CCM na wakaibinafsisha. Ukiwa mweka hazina vikao vyote kwenye top brass vya ndani na nje unahudhuria and that is a power base!!

  Mali zote za CCM wamegawana mpaka na mali za serikali ndiposa akajiuzia Sehemu ya Bandari in the name of TICTS , Migodi ya madini etc.na ndio maana huwezi ukaiondoa pale as long as Matonya ni Rais.

  Just to water down what I have said the late Salome Mbatia RIP alipochukua kofia ya uweka hazina alipata access ya mipango yote ya Epa and other CCM SCAMS za kuchukua pesa kwa wafadhili wa CCM.

  That lady alikuwa na damu kali ya kichaga wakajua kuna siku atawabadilikia !! Kwa kuwa Rostam hakuwa na Imani nae ndiposa ikasukwa mipango na we all know she is long dead just a simple road accident!!! Hakuna uchunguzi uliofanywa kama ule wa Wangwe kwa sababu we all stupidly believed it!!

  Kwa hiyo sitashangaa kama atamteua kuwa waziri and under his instructions ndio maana akina Sofia na Mkuchika wakamkingia kifua RA katika bifu lake na MENGI plus TBC and mpaka leo hajasema kitu as if its something very cheap!! I HAVE smelt a rat kuna kitu kitatokea very soon and Mengi atakuwa historia the Mafia wa CCM hawatakubali aendelee kula ndizi!!! Yes!!!
   
 8. B

  Bobby JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mimi naendelea kuchoka kwa kweli.

  Jamani ninauza uraia nasikia aibu sana kuongozwa na rais ambaye ameweka pamba masikioni na kuifanya hii nchi ni ya kwake na rafiki zake regardless of what they have done, kama wametuibia na kutudhalilisha yeye hajali kabisa.

  Watz hivi kweli hatuwezi kujifunza ili 2010 tusirudie upuuzi tuliofanya 2005?

  KIKWETE HII NCHI SI YAKO NI YA WATANZANIA TUMECHOKA KUDHALILISHWA KIASI HIKI.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Teuzi za Rais wetu tumwachie mwenyewe kwa mujibu wa KATIBA ya NCHI yetu.
  Kama unamchukia RA chukua tu "sumu" ya panya unywe.
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ukishampa mtu uraisi umesha mpa mamlaka juu yako na juu ya nchi. Cha kufanya ni kuchagua mtu bora kuendesha nchi. He is exercising the power we freely gave to him, whether it's in a good way or not.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  haya mambo 'yana misho wake'
  wanaharakati tusife moyo
   
 12. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Kinacho nishangza Kwa mwanakijiji mara nyingine post zake huwa hazina maana kwa mtazamo wangu.

  Lakini yeye mwenyewe amethibitisha kuwa katika tuhuma zote hizi RA jina lake halipo hivi unataka Rais atumie sheria ya kuweka watu kizuizini ambayo ilifutwa hapa nchini.

  Unataka RA afikishwe mahakamani kwa tuhuma ambazo atashinda. Lawama bila uthibitisho ni zilezile anazotoa mzee Mengi. Anapotakiwa atoe ushahidi na vyombo vya Dola anadai anasakamwa.

  Unajua watu wa aina ya Mengi wanaweza kuwa na mambo mawili. Moja kutaka kuitenganisha serikali na wananchi kwa maslahi yake hakuna asiyejua kwamba mengi anataka U-rais lakini hajui njia ya kuitumia. Pili inawezekana anamatatizo ya akili. You never know, kwa sababu wimbo wa mafisadi amekuwa akiuimba bila kuonyesha ushahidi. Achukue hatua kwanza aeleze ushahidi, anaweza hata kuchukua hatua ya kuwashitaki mafisadi. Kwa kutumia haki ya yeye kuwa mwananchi.

  Vinginevyo tutaiangamiza nchii kwa manufaa ya mafisadi au madiktea wangine. Watanzania lazima tuwe waangalifu watu aina ya Mengi. Hivi toka lini tajiri akawa msafi? Hivi toka lini mtu anayefanya biashara ya kawaida akawa na fedha za kumwaga hovyo kwa kisingizio cha kusaidia wananchi.

  Mwanakijiji hebu chunguza wote waliomwaga faedha zao kwa mambo ya mpira utajiri wao uko wapi? Ambao hadi sasa matajiri wachunguze kama walilipa kodi kihalali. Kama hawana uhusiano wowote na mihadarati kisha uje na post tuijadili.
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Haya maneno wanayoandika watu humu usiyafanyie mchezo kwani hasira za umma haziogopi mtutu wa bunduki; Jeuri ya Jakaya ya kuweka pamba masikioni inaweza kuifikisha nchi yetu pabaya kwani vitendo na maamuzi yake yanaonesha kuwa yeye hayuko upande wa wananchi waliomchagua bali yuko upande wa mafisadi wanaowanyima watanzania kuwa na maisha bora! Inawezekana isiwe leo wala kesho lakini siku ya siku nyie mafisadi wote mlio madarakani mtajijutia na itakula kwenu!!
   
 14. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nasita kidogo, kwani sioni andishi lako hapa lina maana gani, kwani kilichoandikwa kwenye andishi la mwanakijiji silo ulilojadili bali mambo ya Mengi. Bila shaka post zako ndizo hazina maana na inakufanya usione maana yoyote kwa MM. Tangu lini kipofu akaona macho ya mwenzie?
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Rostam, Manji na wengine wengi kama Balali walitumiwa tu na CCM. Kama ambavyo wengine wanaendelea kutumiwa akina Dau wa NSSF, Mutalemwa wa DAWASA, ......Ichukieni CCM sio WATUMWA wake.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Bulesi,
  Mimi pia fisadi? Ndugu yangu hata baisikeli sina. Ninachosisitiza hapa nikuiheshimu Katiba na mamlaka zilizopo.
   
 17. S

  Sauti ya Simba Member

  #17
  Jun 4, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mzee Mwanakijiji kwa post hii. Ni kweli huyu bwana ni afadhali amhalalishe tu rafiki yake RA katika nafasi mojawapo serikalini kuliko alivyomuachia hivi sasa akiingilia kila idara kwa jeuri ya p├ęsa chafu na urafiki wake na mkuu wa nchi.
  Ningependa kumfahamisha wazi JK kwamba ANGUKO lake litatokana na kumdekeza RA na kumuacha afanye atakavyo katika nchi yetu. Hivi sasa, tangu atajwe kuwa fisadi papa amekuwa akifanya mambo mengi ya chini chini kwa kuwatumia viongozi wetu mafala na mbumbumbu kwenye kila idara. Sasa anapanga njama ya kumkomoa Mengi kutokana na kumuumbua. Sisi Watanzania halisi tunasema hatutaweza kuendelea kuvumilia upuuzi huu. CHIWONEKE CHIWONEKE!
   
 18. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama hukubaliani na uongozi wa sasa fanya uchaguzi mzuri 2010.
   
 19. C

  Cool Girl Member

  #19
  Jun 4, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  msijifanye mnaishi katika nchi ya kufikirika!!!!!mzee mwana kijiji hii thread yako inaonyesha umeandika kwa hasira,unaweza kutengeneza territory yako if you wish,mara nyingi nasoma thread zako ni za kizushi na za uchochezi unatamani sana watz wakusupport hayo unayoyafikiria is impossible ,hiyo ni wewe tu na roho yako,kama haumpendi RA na kama haukipendi chama cha mapinduzi hama nchi au chimba shimo ujifukie!!!!mbaya kwako ni mwema kwa wengine!!!na kama una tatizo na vodacom ni kivyako si lazima upande chuki kwa watu kwa chuki zako wewe binafsi!!!
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huwezi kuchukia parasites wa malaria bila kuchukia mbu. Wote ni shida tu ya malaria.
   
Loading...